Urithi wa Kikwete na haiba iso sababu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urithi wa Kikwete na haiba iso sababu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pundit, Aug 28, 2008.

 1. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Urithi wa Kikwete na haiba iso sababu

  Binadamu kwa kawaida hupenda kukumbukwa, hususan kukumbukwa kwa mazuri, au yale wanayotaka yaonekane kuwa mazuri. Nimekuwa nikifikiri kuhusu uongozi wetu, hususan rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete na anavyofikiri mchango wake ulivyo seuze atakumbukwaje katika taifa letu.

  Kama wana JF wengi wanaosoma michango yangu wanavyojua Kikwete si mtu niliyemtaka kuwa rais wa Tanzania, si mwaka 1995 wala muda mwingine wowote. Lakini katika kudekeza falsafa ya kupenda kuwa mtu wa matumaini na kulazimisha kuwa kila binadamu ana haiba, haiba ambayo hata mtu asiye na uwezo wa kuongoza au mfisadi inamfanya asiweze kuachia mambo yaendelee kutapanywa bila maangalizi, na hivyo kusababisha maangamizi. Haiba hii, kwa maneno mengine ikijulikana kama haya, soni, adabu na amneno mengine kama hayo ni moja kati ya vitu vinavyomtofautisha binadamu na mnyama.Kwa bahati mbaya kabisa, naona rais wetu hana haiba, woga, heshima, adabu wala haya juu ya hili.

  Kwamba ameweza kusimama "uso mkavu" (nataka kuamini alikuwa hajajidunga kabla ya kuhutubia bunge, ingawa mara nyingine inaniwia vigumu) na kwa masaa takriban matatu kutoa hotuba iliyojaa upuuzi, na si upuuzi tu bali upuuzi unaojikanganya na kukinzana inaonyesha ni jinsi gani anavyojiamini kwamba hata akijikojolea mbele ya kadamnasi washairi na watunga tenzi watamsifia kuwa "Rais Kikwete aleta maji kwenye ukame". Kabla sijatulia vizuri nasoma ripoti kwamba kweli, bila utani, kuna watu wanataka kuandamana kumuunga mkono, kwa kipi kikubwa alichosema? Kukataa kuwashitaki watuhumiwe ambao ushahidi wa kuwafungulia kesi upo? Kushindwa kutoa uongozi katika suala la muungano na Zanzibar? Kuonyesha kutokuwa na imani na mfumo wa mahakama wake yeye mwenyewe?

  Unahitaji ngozi ya mamba na upofu wa macho ili kuwa Kikwete.Kama uongozi ni kuwa kichwa ngumu basi rais tunaye.Hivi Kikwete anawezaje kuwaangalia watu machoni? Au kama alivyosema mwenyewe katika hotuba yake, kwamba anaweza kuamuru chochote kifanyike na kikafanyika, anajua kuwa karibu kila mtu anajua ukweli lakini yeye kwa sababu ni rais ana nguvu ya kuupindisha ukweli? Hili alilosema linaweza kuonekana dogo lakini linaweza kuwa ni njia nzuri ya kutuonyessha jinsi gani Kikwete anaamini katika ubeberu wa mabavu ya "Mshindi anachukua chote" na "Ninyi raia tu hamna usemi, mimi ndiye rais mwenye uwezo wote!"

  Hili linatuleta katika swali lingine. Hivi kwa nini Kikwete atake kuupindisha ukweli? Huu ulikuwa ni wakati mzuri sana kwake wa kuonesha Watanzania milioni kadhaa waliomchagua kuwa hawakufanya makosa.Lakini badala yake anaendelea kuficha ugonjwa huku akijua mauti yatamuumbua (this is sadly true literally and metaphorically, a president with a nature to hide his own auilment will carry that into his functions and sweep wrongdoings under the carpet, burying his head in the sand like that naïve Australian Ostrich, hoping that what he does not see will not harm him!).Kwa kweli mimi sikutegemea mengi kutoka kwa Kikwete, lakini bado ningependa kuona mimi ndiye niliyekosea katika kumhukumu Kikwete mapema kuliko kumuona Kikwete anakosea katika swala linalohusu kukubalika kwake na imani ya wananchi kiujumla, mali ya umma na hata usalama wa taifa letu.

  Kwa nini wananchi tusiamini kuwa Kikwete pamoja na rafiki zake wa karibu kabisa wanahusika na uozo huu wa EPA? Hivi kweli unataka kuniambia kuwa kama wanaohusika wangekuwa wakalamba wa kawaida tu walioweza kujua ujanja wa kufyonza hela BOT Kikwete angekuwa na simile hii? Kwa nini Kikwete hataki kufanya mkondo wa sheria ufuatwe? Katika nchi inayompa rais madaraka makubwa sana kama alivyosema yeye mwenyewe, kuna nafasi kuwa hata kama haya mambo yakifika mahakamani (if ever) basi hatua hizi za rais kutetea sana hawa watuhumiwa zitafanya hata vyombo vya sheria vifanye kazi kwa kuogopa.Nina mashaka kwamba hata kama sarakasi hizi zitafika mahakamani watakaoshitakiwa watakuwa wapambe tu na "wakubwa" wenyewe wataendelea kutanua katika mahekalu na mashangingi yao.


  Rais Kikwete anatuachia urithi gain? Hana hata uwezo wa kufikiri na kuona kwamba atakuja kuwa rais asiyekuwa na lolote la kukumbukiwa? Nyerere pamoja na mapungufu mengi ni muasisis wa Tanzania, Mwinyi pamoja na laisez-faire yake alisaidia nchi kutoka katika kufunga mkanda na akasimamia mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa. Hata Mkapa na ufisadi wake anaodaiwa aliurudisha mfumuko wa bei chini na kuanza kukusanya kodi.
  Kikwete atatokaje kama mwanzo ndio huu? Wengi wa waliokuwa na matumaini wanaanza kuishiwa na sababu za kuendeleza kutumainia zinabaki miujiza.

  Ngoja tumuweke Kikwete katika mizani ya uongozi bora kama walivyoiweka wajuzi tangu enzi. Hivi Kikwete anaweza kusema ana- inspire watu? Kwa kazi gani anayoifanya? Sana sana anavunja matumaini yote ya Watanzania juu ya uongozi wao.

  Hivi Kikwete anaweza kusema kuwa hayumbishwi na tamaa jitaihada ya power? Nikimuangalia naona kama kuna kitu pekee alichofanikiwa katika maisha yake ni kutafuta na kuipata hiyo power, ingawa inaonekana hiyo haikuwa njia yake katika kufanya vitu vikubwa zaidi, alichotaka ni kupata uongozi mkubwa kabisa katika Tanzania, power, baada ya hapo hakujua na wala hana mpango afanye nini! Ukiwa unataka kuwa kiongozi tu, bila ya kuwa na ajenda, unataka ukubwa tu, ni vigumu kuwa na principle za kukuzuia kuchukua rushwa za WaIran na kina Rostam Aziz, ni vigumu kuiba hela benki kuu kwa kisingizio cha "usalama wa Taifa" ni vigumu pia kuwashitaki watuhumiwa ambao ushahidi wa wazi upo. Unaopgopa kuwa ukitingisha hili jahazi unaweza kukosa usukani na mlo wako ati!

  Kuna watu wamesema kwamba moja ya matatizo ya mifumo ya demokrasia changa ni kwamba uchaguzi wa nani anakuwa kiongozi unatoka juu kuja chini. Watanzania hawamchagui rais, watu wachache wa CCM wanamchagua mgombea urais kwa tiketi ya CCM ambaye kwa hali ya kisiasa ya sasa ndiye anakuwa kama tayari rais hata kabla ya uchaguzi.Kwa hiyo ukiweza kuwafanya watu wachache wa CCM wakuchague unakuwa rais hata kama wewe ni bongolala ambaye hujafanya chochote kama Kikwete.

  Kikwete amejionyesha kuwa na tabia hizi hatari kwa kiongozi yeyote kama zilivyotajwa na Van Hooser.

  1. Kukosa nidhamu

  Ni wazi hana nidhamu. Anakosa nidhamu katika kitu kidogo kama kutumia Kiswahili fasaha katika hotuba ya bunge. Kuna Member ameanzisha thread kuhusu hili. Sitegemei rais awe na nidhamu katika mambo makubwa kama hana nidhamu katika mambo madogo. Ukimsikiliza anavyosema kwamba rais anaweza kuamua mtu yeyote afungwe na kafungwa bila sababu unamsikia mtu asiye na nidhamu kwa Watanzania. Hili jambo la rais kuwa na nguvu sana ni la aibu, na si la kujivunia na kulitangaza, wenzake wote kina Nyerere mpaka Mkapa, ambao walikuwa na nguvu kuliko yeye hawajawahi kulisema wazi wazi hivi. Kikwete hana nidhamu.

  2. Kutokuwa na maamuzi mazuri

  Kuanzia anavyo mishandle maswala ya ufisadi mapaka teuzi zake Kikwete anajionyesha hana maamuzi mazuri.Ni kama mtu ambaye amezoea kufanyiwa maamuzi makubwa nay eye ni mtekelezaji tu na siku moja amejikuta yeye ndiye muamuzi. Atakalia maswala bila maamuzi, atakapofika sehemu ambapo ni lazima kufanya maamuzi ataongeza muda (EPA) au kutoa kauli zenye kutokuwa na maana kwa sababu zinakinzana (Zanzibar)

  3. Kutojali shida za wenzake / wananchi.

  Mtu anayeweza kuachia wezi wa mabilioni wakae kwa raha mustarehe kwa kisingizio cha "Haki za Binadamu" wakati wananchi wako hohehahe, na wengine wanafungwa katika jela zisizo za kibinaabamu na wala hajasema kitu kuhusu "Haki za binadamu". Inaonekana hizi "Haki za binadamu" si za binadamu wote ni za wakubwa na wenye hela tu.

  4. Kuwa mkuda sana au mpole sana.

  Kikwete anabwaka sana lakini hana matendo.Kila siku anatoa maonyo na makaripia bila ufuatiliaji.Mwisho wake anakuwa ni kama yule mzazi ambaye wanawe wanajua wazi kuwa baba/ mama akikuona unafanya kitu asichopenda atakwambia tu "hii iwe mara yako ya mwisho" bila lolote kutokea. Kwa nini watu wasigide bila kuogopa. In a way this is bigger than ruksa.

  5. Kuwa myabisi,mjivuni na kutojali.

  Kikwete anasema wazi kuwa Watanzania nyie maskini hamna hela, serikali haihitaji michango yenu tutakuja kutafutana lawama tu. Huu ni mfano mmoja tu ambapo amechanganya uyabisi (being cold).Myabisi kwa sababu hakuguswa na jinsi gain maneno yale yangewafanya Watanzania wafikiri. Kutojali (aloofness) hakujali kwa sababu kama angejali asingesema maneno yaliyokosa hekima na heshima kama hayo.Mjivuni (arrogant) kwa sababu anajiona yeye ndiye yeye na nyie wengine hamna kitu, akisahau kuwa kawekwa pale kwa dhamana tu ya wananchi.

  6. Kufanya mengi na kuongoza kidogo.

  Kikwete yuko kila sehemu, AU, Comoro, Uingereza, Marekani, anzindua tume hii au ile kila siku, lakini ukiangalia anachoongoza ni nini unakuta karibu kabisa na sifuri. Anafungua shule nyingi lakini hazina walimu. Anaenda kufungua daraja ambalo halijakamilika. Anaunda tume ya kuwashikisha adabu mafisadi halafu analeta siasa na pardon ambayo hata haijaombwa. Anafanya mengi lakini haongozi hata kidogo.

  7. Kuleta picha ya upendeleo.

  Kuanzia habari ya mtandao vs the rest of CCM, CCM vs wapinzani, mafisadi wakubwa vs vibaka wadogo, you name it. Kikwete anapanda mbegu ya mgawanyiko kwa kudekeza picha ya upendeleo.

  8. Kuhadaa imani ya Watanzania

  Kikwete amekuwa mtu ambaye ameweza kufuja imani kubwa aliyoonyweshwa na Watanzania baada ya kuchaguliwa kwa ushindi wa "Tsunami" sasa anafanya mambo tofauti na alivyotegemewa, tofauti na ahadi na kiapo chake, tofauti na ahadi zake, ilani ya uchaguzi, miiko ya uanachama na uongozi wa CCM.

  9. Kutokuwa na uwezo wa kufikiri mpango mkubwa

  Kikwete hana "master plan" wala "strategic thinking". Kila kitu kinakwenda ama kwa ulimbwende tu au kwa mtindo wa zimamoto.Watu wanaotegemea kupata uongozi kutoka kwake serikalini wanabaki kushangaa na sarakasi kavu anazopiga kila kukicha.

  10. Kuweka wafanyakazi wasioweza/ stahili kazi.

  Viongozi wazuri wote wanajua umuhimu wa kuwa na timu nzuri katika kufanikisha mambo.Kikwete inaonekana kama at all anataka kufanya vizuri basi anataka kufanya hivyo kwa bahati nasibu. Teuzi zake zinachekesha sana, kuanzia vihiyo walioibia vyeti kutoka vyuo vya kubabia na "vinu vya stashahada" mpaka rafiki zake waliomsaidia katika kampeni zake chafu za urais. Watu hawana integrity na hawana hata nguvu za kumshauiri vizuri, matokeo yake kila mtu anayemzunguka ni "Yes man" ambaye hawezi kuwa tayari kuingiza kitumbua mchanga, au kufanya kibarua kiote majani kwa kumwambia ukweli rais, matokeo yake ndiyo utasikia "Kikwete anatisha" au watu wanarubuniwa na wapambe wake kuanzisha maandamano ya kumsifu. Mfalme yuko uchi lakini kila mtu anasifu joho lake, panya wanabishana, nani amfunge paka kengele. Labda Spika Sitta, ambaye naye hayuko above reproach kwenye ufisadi, kwa kumsema juzi baada ya hotuba atakuwa ameleta chachu mpya.

  11 Kutotaka kubadilika.

  Inawezekana wakati wa kina Nyerere Tanzania rais alikuwa ni mungumtu na chama kilishika hatamu.Mambo haya hayapo tena na si ajabu kwa mwendo huu wa shingo kavu na kichwa ngumu wa Kikwete, si watu wa mijini tu na wasomi watashtuka. Wanasema ukila na kipofu usimshike mkono, uinaonekana Kikwete anajisahau sana na kufikiri watanzania hawawezi kufanya lolote nay eye ataendelea kula bila kujali kama anawashika mkono au la. Ile hotuba yake ya kuwakingia kifua mafisadi ilikuwa ni kuwashika mkono hata wale vipofu wasiojua nini kinaendelea.Kwa kutokubali kubadilika, Kikwete anasaidia maendeleo ya vuguvugu la mapinduzi Tanzania.Si haba ndugu yangu Mchungaji Kishoka alisema "Thank God for Kikwete". Ni kauli tata kidogo, lakini kama unapata rais fisadi anayejificha ficha inawezekana kabisa watu wasijue na akaendeleza ufisadi bila matatizo, uzuri wa Kikwete anakwenda bungeni na kuwakingia kifua kabisa mafisadi watu wote muone. Anawaambia mafisadi wake "Msiogope kuitwa mafisadi". Kwa nini wasiompenda wasishukuru mungu kwa kuwapa **** majununi?

  12. Kutoheshimu utawala wa sheria, taratibu za uongozi, manifesto na katiba

  Kikwete anajionyesha kufanya mambo kiholela bila kufuata misingi ya uongozi bora na utawala wa sheria.Kutokana na kujiona "mshindi" anayeweza kufanya chochote bila backlash yeyote kutoka kwa Watanzania, Kikwete anashindwa kuonyesha uongozi wa sheria.Kutokana na mfano huu auonyeshao, na pia kutokana na teuzi zake dhaifu, baraza lake la mawaziri limejaa misuguano ambayo inaleta picha mbaya kwa wananchi.Ikiwa mawaziri na kiongozi wao wanashindwa.

  13. Kuweka mipaka na misimamo isiyo wazi.

  Kikwete hakupanda ngazi kwa uchapa kazi au uwezo.Kikwete si kipanga au "policy wonk". Huyu rais wetu wa sasa amepanda ngazi kwa hadaa, kujifaragua na kujipendekeza kwa wakubwa wake. Mtu anayepanda ngazi kwa jinsi hii hawezi kuwa mtu wa "principle", mtu wa aina hii ni mtu wa kuficha makucha na kwenda na upepo.Kwa sababu hii Kikwete amejenga tabia ya kuwa vague, anataka kuila keki yake halafu abaki nayo mezani.Hii ndiyo sababu ameshindwa kulitolea msimamo swala la Zanzibar na kutoa kauli tata ambayo inataka kuwafurahisha watu wote.Kikwete hafahamu kuwa kwa kutaka kuwafurahisha watu wote atakuwa hajamfurahisha yeyote. Ukiongelea Zimbabwe au Zanzibar rais wetu hawezi kuwa kiongozi kwa sababu hayuko tayari kuwa na msimamo.


  14. Kutoweza kuchukua hatua pale anapotakiwa.

  Pengine zaidi ya swala lingine lolote hili swala la EPA limeonyesha rais asiyeweza kuchukua hatuapale inapotakiwa.Kikwete ni sawa na baba mwenye nyumba alieambiwa na watoto "Baba, tunasikia harufu ya gesi, inawezekana mtungi wa gesi ya kupikia unavuja" akaendelea kulala, akaambiwa "Baba, kuna cheche kwenye nyaya za umeme jikoni" bado akaendelea kulala, akaambiwa baba sasa zile cheche zimechanganyika na gesi na kufanya moto mdogo, bado akalala, na sasa hatima yake moto umeshaanza kuwaka jikoni, bado amelala. Anasubiri nini? Anasubiri moto umuwakie mbele ya mikono yake? Rais wetu kutoweza kuchukua hatua pale anapotakiwa na pacha wake kuachilia matatizo kuendelea kutatugharimu sana.


  15. Kulewa madaraka

  Kikwete anaonekana wazi kuwa mlevi wa madaraka, sio tu anayeweza kufanya lolote bila kuogopa, bali pia anayeweza kusema mbele ya bunge, Watanzania na dunia nzima kwamba anaweza kufanya lolote bila kuogopa. Huu ni wakati mzuri wa kuanzisha kampeni ya kupunguza madaraka ya rais, yale yaliyo rasmi na yasiyo rasmi. Haifai kuwa na urais wenye madaraka mengi kwa sababu hatujui kama kila siku tutapata rais mwenye uwezo wa kutoyumbishwa na vishawishi vya kutumia madaraka vibaya. Noblese Oblige, to whom much is given, much is required, responsibility to protect.Wenye nguvu wawe tayari kuhakikisha hakuna loopholes zitakazoruhusu matumizi mabaya ya madaraka, hii inajumuisha wenye nguvu, na rais yupo juu kabisa katika hawa, kuwa tayari kupunguza nguvu zao, siyo kuja ku "lord it over us" katika hotuba za bunge. Cheo ni dhamana, rais Kikwete anaonekana kusahau hili.

  16. Umangimeza

  Kama unaongelea kuhusu tume za kuchunguza tume, safari zisizoisha, hotuba za masaa matatu zisizo na mantiki wala kitu kipya na upuuzi mwingine unaofanana na huo, rais Kikwete amejidhihirisha kuwa ni bingwa wa umangimeza, anayejua sana kusema, hapana, anayejua kusema sana bila kutoa msimamo au kuwa na lolote jipya.Amejizolea majina lukuki kutoka "Muungwana" (hataki kuchafua mikono yake kwa matope ya kazi) mpaka kiongozi wa "Ze Comedy" kutokana na jinsi anavyoiendesha nchi.


  Ninapomuangalia Kikwete ninajiuliza sana tena na tena, inawezekana kweli Kikwete ana nia nzuri lakini anashindwa kutokana na vitu vilivyo nje ya uwezo wake? Nikimuangalia Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown, naona ana matatzo kama ya Kikwete, Gordon Brown kama Kikwete, alikuwa anajiandaa kuwa rais kwa miaka 10.Baada ya miaka yote hiyo inaonekana kama Brown alikuwa mzuri sana katika kujiandaa kuwa Waziri Mkuu lakini baada ya kuupata uwaziri mkuu, hajui cha kufanya.Kikwete anaonekana alikuwa anasubiri kuwa rais kwa miaka kumi, lakini baada ya kupata urais hajui cha kufanya. .Lakini tofauti kubwa kati ya Brown na Kikwete ni kwamba Brown alifanya kazi nzuri sana alivyokuwa Waziri wa Fedha, na ingawa ana matatizo kisiasa, haandikwi vizuri, opinion polls ratings ziko chini sana, lakini Brown hajapata nafasi ya kuwa mbele ya goli na kushindwa kufunga kama alivyo Kikwete. Inawezekana kabisa matatizo ya Brown yanatokana na Waingereza kuchoshwa na chama chake cha Labor na "zero tolerance" ya Waingereza, Kikwete hana tatizo la "zero tolerance" kutoka kwa Watanzania, kama kuna tatizo basi ni "maximum tolerance".

  Kwa nini Kikwete anaonekana kutofanya mambo yatakayopalilia ustawi wake kisiasa?

  Itaendelea
   
 2. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu ndiye Kikwete bwana
  na hizo ndizo sifa zake, lakini wala hana shida lakini wako ambao bado wanamuona kama yeye ndiye mwisho na wanaandamana kwa njia yoyote ile ili waweze kuonekana na kupewa kidogo dogo
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pundit, this is a Great Staff, nashauri kuwa utoe idhini na wahariri wa jarida lile waweze kuihariri na kuichapisha na haswa kwenye hizo sifa za JK kwani ndio ukweli halisi wa huyu jamaa.
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu kweli nimekubali huyu ndie rais...katika lugha kwa kweli inaonekana kiti hiki alikwa anakitamani sana...

  Huwezi sema kuwa unaweza funga mtu bila sababu...japokuwa baba wa taifa alikuwa na Joke zake katika hotuba ambazo naona na huyu bwana mkubwa anataka ku adopt katika hotuba zake...yaani anataka fanta nyao...ila kwa sasa sio kama zamani anzania haikuwa na matatizo mengi katika kichwa chake.Ndio maana mzee alikuwana wasaha wa kuweza kuweka JOKE katika hotuba.

  Tuna mambo mengi sana kwenye nchi hii ya kuzungumzia katika part zote hizo alizoweka joke...tanzania imepoteza mwelekeo...katika matumaini ya raisi tuliye mchangua kwa nguv zote...harafu anaweka na joke?Kweli jamani...

  Am out..
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 28, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  Pundit,

  ..kazi nzuri sana sana.

  ..sikijua kama unaandika kiswahili fasaha kiasi hicho.

  NB:

  ..nimependa ulivyobainisha kwamba Kikwete hakupanda ngazi kutokana na uchapa kazi wake bali kwa kujikomba kwa wakubwa zake.
   
 6. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  pundit nimekuwa nikiwambia watu mbalimbali kwamba as far as kikwete is concern is done, yeye alitaka jina lake liadikwe kama moj wa maraisi wa tanzania basi, huyu ni sawa na wanaume wengi ambao dunai imeshuhudia wanacho taka ni kutongoza mwanamke na kumtoa bikira baada ya hapo hana anachojua,ndugu zangu huyu ndiye raisi wetu hatuelezi kwa nini watu asshitakiwe,hajui basi na wezi wajao watomba the same treatment hivi wakati anagombea urahisi mama yake hakumwambia na kazi ngumu,alijua vingora tu,jamani from before niliwaeleza we are fucked up, with this boy.yani nilisikiliza hotuba ile 3hours nothing,lazima nchi yetu tutafute utalatibu mwingine wa kupata raisi au viongozi hivi tutakwenda na watu kama hawa hadi lini,lakini thank god for kikwete he makes our ball to grow big, oooh i have a dream one day our poor mother tanzania will get some body who have head to lead us ahead, hivi huyu atachukua form tena kwa term ya pili, na atagombea tena ooooooh god wakati wa kampeni akianguka kifafa asisimame tena.
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Dec 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Inaendelea lini mkuu?
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Dec 20, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundit,
  For the sake of this Thread mkuu mimi sikubaliani na mambo mengi uliyoandika!....
  Kwanza sioni mapungufu zaidi ya maelezo ambayo yanajirudia kwa ujeuri, kiburi na kadhalika bila kuelezea hasa mapungufu ni yapi na kiongozxi bora angefanya nini..
  Ninarudi baadaye....
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Dec 21, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundit,
  Kwanza nakupongeza sana kwa kuchukua muda ukaweka kitu kama hiki ambacho kinanipa kufikiri nje ya sanduku..Na kama kawaida yangu nimeona mengi ambayo kusema kweli yamenifanya kuguna na kusema mhnnnn! hii ni lugha ya mitaani ..Maneno kama kukosa Nidhamu, Mkuda, Mjivuni, Mnyambisi na kadhalika kisha inafuatiwa na Hotuba zake kidogo hainipi picha kamili ya Kikwete kama rais alitakiwa kufanya nini..

  Binafsi nikitazama swala la EPA, kwanza ni swala ambalo limeanza toka zamani na lilishamiri wakati wa Mkapa, tuzo nyingi zimetolewa kabla ya uchaguzi 2005 Kikwete akiwa waziri ambaye hana madaraka zaidi ya rais aliyekuwepo. Na bila shaka walioweza kufanya hayo machafu ni Viongozi wenzake, watu wenye uwezo na nafsi ya kimadaraka kuyafanya hayo na sio Wakalamba..watu ambao waliwekwa madarakani na kiongozi aliyemtangulia.

  Mkuu kuna wakati ni muhimu tukubali reality, swala la EPA ni lazima waliochukuwa walikuwa watu wa juu, mimi na wewe na wakalamba wote tusingeweza kufika huko na ndio maana wizi atakao kamatwa Mkandara utahusu zaidi wizi wa kuku maanake nina njaa na huyo kuku naweza kukualika wewe kwa chakula, ukawa mshirika. tatizo la hukumu ya kuku ni kwamba hata huyo Lowassa na Sitta umekuwa umeiba kitu kinachowahusu hata wao (chakula) watakumaliza! hiyo EPA wengine tunasikia tu habari jinsi inavyomuathiri Mkalamba wengi wetu hatufahamu isipokuwa tunashangilia tu ushindi.

  Kuna tuhuma ziliendelea mijini kabla ya Bunge kuwa Kikwete hana uwezo, nguvu wala ubavu wa kumsimamisha mtu..Sasa mimi sioni ubaya kwa Kikwete kuwakumbusha watu kuwa yeye ni rais na anaweza kufanya yasiyokuwa na sheria.. hiyo power anayo na anaweza kuwa jeuri kwa vitendo isipokuwa amechukua mkondo mwingine wa sheria ktk matendo yake hivyo msiweke dharau kuwa hawezi.
  Nadhani matendo ndio bora kutuonyesha mazuri/mabaya yake badala ya hotuba zake.. Kwa mfano kauli ya kusema anaweza kutumia Rule by Law (kuonyesha ana Ubavu) sio kosa ikiwa mwenyewe anafuata rules of Law na kuachia vyombo vinavyohusika kufanya kazi yake. Hatukuona hata wakati wa Nyerere, Mwinyi wala Mkapa ni mara ya kwanza Tanzania tumeshuhudia nguvu ya mahakama pamoja na kwamba ndio mwanzo. Kwa mara ya kwanza tumeona Tanzania nguvu ya Kikosi cha kuzuia Rushwa badala ya rais na Waziri wake mkuu kama alivyofanya Nyerere na Sokoine, sasa hapa kuna kiburi gani cha kutojali wananchi tukiacha nje hizo hotuba zake.

  Turudi nyuma kidogo labda wenzangu mnifahamishe vizuri Kikwete alitakiwa kufanya nini?.. Iwe kisheria ama kama kiongozi bora ni hatua gani alitakiwa kuzivuata ikiwa sisi wenyewe na vyombo vyetu vya sheria tulishindwa kuwasimamisha watu hao mahakani tukisubiri AMRI ya rais. nakumbuka hata kina Salim, Mwinyi, Warioba na wengine wote waliomba na kusubiri rais atasema nini kuhusiana na swala la EPA..Bado sote tunamtegemea Kikwete kuhusu maswala ya mengi yaliyotangulia ikiwa ni pamoja na Rada, Ujenzi wa BoT, Ndege ya Rais, Kiwila, na kadhalika yaani kwa pamoja hatuwezi hata kuyahesabu...WHY only him, kwani sheria inasema hivyo!
  Miaka yote tumekaa kimyaaa hadi Kikwete alipokuja na UWAZI ambao sasa inaonyesha pia kuwa yeye mwenyewe Kikwete ndiye anatakiwa kutoa hukumu. Kwa nini iwe yeye wakati tunafahamu kwamba Lowassa na Rostam ni marafiki zake.. Je, hawa watu wana kinga ya sheria yoyote kufikishwa mahakamani hadi rais (Kikwete) atoe dole!
  Binafsi mara nyingi huwa najiuliza kwa nini sisi wadanganyika tunasubiri hadi rais afanye kitu fulani ndipo tunaanza kunyoosha vidole! hatukuyaona haya wakati Nyerere alipokuwa hai hadi kafa ndio tunasikia mabaya yake yakitangazwana kina Mwinyi na Mkapa..Mwinyi, Mkapa wote ni yale yale hadi leo tumetoa tongo ndani ya Utawala wa Kikwete, huo Upofu ulitokana na kitu gani hasa..

  Kikwete kama kiongozi anayo mapungufu mengi sana hasa hiulo la kuweka viongozi wasioweza kazi..lakini again tutazame picha nzima.. Sikumbuki mbali na Nyerere kama kuna kiongozi Tanzania aliyeweka watu wanaofaa...
  Na hii inakwenda hadi ngazi za ajira ktk Mashirika ya watu binafsi..Leo hii Tanzania unakuta Wakenya wanachukua kazi kwa sababu wanazungumza kiingereza!.. yaani talk the talk ndio qualification kubwa sana nchini..Ukijua kuzungumza wewe mjanja, iwe ktk kutafuta kazi, mchumba na hata nyumbani utaonekana wewe una akili sana kwa sababu ni msemaji mzuri..

  Kuhusu swala la Zanzibar, sidhani kama kuna mtu yeyote anaweza kutoa hukumu leo hii.. Hata hao viongozi waliotangulia walishindwa na nina hakika hakuna mgombea yoyote mwenye jawabu linalokubalika na wengi kuhusiana na mgogoro wa Muungano!..
  Matatizo mengine ya ndani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule, mkuu wangu kusema kweli pamoja na makosa mengi kufanyika lakini nakumbuka zile picha za mwaka 2002 hadi 2005 jinsi watoto wetu walivyokuwa wakisoma chini ya miti inatisha zaidi... taratibu majengo yamesimama hatua nyingine zitafuata ingawaje sio mpangilio mzuri kuwa na shule bila walimu wa kutosha..Kumbukeni tu kwamba wakati Mkapa anaondoka kuna walimu walikuwa akidai hata mishahara yao ya nyuma!..
  Mambo nimengi sana na sidhani kama kweli Kikwete ana jeuri ambayo umeizungumza!..
  Kifupi mimi namwona yeye kama ni mtu anayeogopa kitu, mtu anayejaribu kujipendekeza zaidi ili apendeke badala ya kufanya mazuri wananchi watampenda!..Na bila yeye kuvuruga CCM na Mtandao yote haya tunayoyajua leo yangebakia chini ya uvungu.. Ni kikwete ndiye aliyekuja haribu kabisa Plan ya viongozi mafisadi ambao lengo lao kubwa lilikuwa kugawana mali ya Ya Umma kwa makundi..Mtandao umepatikana baada ya kundi moja (La Mkapa) kuwazidi karata kundi jingine..nao wakajipanga kujiandaa kuchukua zao lakini Kikwete amewageuka, hakuna kula tena.. Scandal kubwa iliyotokea ndani ya Utawala wa Kikwete ni Richmond na tumeona waziri mkuu, mawaziri na wahusika wengine wakiondolewa...Swala la kuwafikisha mahakama sidhani kama ni swala la Kikwete kutoa maamuzi.. Yaani atupikie, tupakulie na kutulisha jamani!..Sidhani kama ni kazi ya Kikwete hata kuondoa kadi ya uanachama wa Lowassa CCM ni kazi ya wanachama, viongozi na watu wengine wote ndani ya CCM ambao tunategemea kesho watachukua nafasi ya Kikwete au kuwa waziri..
  Viongozi ambao wanaweza kupambana na Kikwete ktk uchaguzi wote wako Bungeni wanashindwa nini kuonyesha ushujaa wao kuwasimamisha wadhalimu hawa makahamani..
  Huo ni mchango wangu!..
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pundit na Mkandala michango yenu imetulia mda tuu umenibana otherwise tungekwenda kipengele kwa kipengele.
  Mkandala kumbuka mtu anapokuambia weakness zako ana maana you work on them and embark on a u turn strategy kama wazani weakness pointed are trully in ua midst.
  Suala la kusema JK alitakiwa afanye nini-apo common sense tuu inatumika.
  Mfano "kuteua wafanyakazi wasiostaili" apo JK lazima alaumiwe kwa kuteua watu kwa miadili ya kulipa fadhila na ushikaji bila kusahau mtandao.
  Wakati kazi ya kuijenga Tz ni yetu sote hayo makundi yanatoka wapi.
  Mfano 2 "kutotaka kubadilika" Seriously speaking JK is very conservative mbaya zaidi hafikilii mbali issue yaweza kuwa yeye mwenyewe na wasidizi wake.
  Kitu mpaka wananchi walalame weeeeeee ndo anakifanyia kazi ie proactiveness ZERO.
  To me weaknesses za JK highlighted by Pundit ziko straight forward kwa mwenye akili timamu to work on them.Sio kila kitu tumtafunie uyo JK kwani hana ubongo?
  I know JK can do more than what he has done kwa watanzania.He only needs to play his part and it can be done as well as embark on a U turn strategy aaachane na uswahiba,mtandao etc TUIJENGA TZ YETU SINCE MAISHA TUNAYOISHI HATUSTAILI KABSAAA NCHI YENYE NEEMA KAMA HII.
  After all Pundit kasema ataendelea any you may come up na izo suggestions as a way forward kwa JK ambayo to me ni Spoon feeding
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,584
  Likes Received: 18,567
  Trophy Points: 280
  "Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni" . Kwa vile jina la Kikwete linatanguliwa cheo, nashauri hata kama hatumpendi, hata kama anaboronga lakini ukweli unabaki kuwa yeye Jakaya Mrisho Kikwete ndiye rais wetu, basi tumwadress kama Rais Kikwete kila tunapotumia sir name yake.Kumwita Kikwete tuu bila neno Rais ni utovu wa nidhamu na dharau.

  Tunaweza kuamua kumuita jina la kwanza la Jakaya au lile la mtaani la JK, tukimaanisha tuko level moja, then its ok kumuita bila neno rais kwa vile hili ni nick name. Namna ya kumuadress mtu pia ni namna ya kuonyesha heshima kwa aina fulani kama Mr, Mrs, Dr, Prof etc inavyotumika na sir name, halafu ukitumia fast name sio lazima kuweka heshima.Take note rais Bill Clinton, walikuwa wakimwita President Clinton. Alipoboronga na Monica Lewinsky baadhi ya waandishi walimuita Bill. Hili Bill ni nick name jina kamili ni William Jafferson Clinton. Hivyo tumuite Rais Kikwete tukitumia sir name yake aut tumuite Jakaya au JK bila neno rais.

  Nikija kwenye maoni yangu naona Pundit ameandika kwa hasira hivyo ameandika mengi yanayojirudia jirudia. Kuna wakati nilichangia mahali kuhusu Rais Kikwete kwa mtazamo wangu nikasema ni rais mwenye degree ya chuo kikuu lakini ukimtazama usoni na kumsikiza hotuba zake haonekani kama msomi. Bado anaonekana kama mjinga mjinga fulani. Yaani ni kama ignorant, hotuba zake ni kama simulizi za hadithi za Alfu Lela Ulela. Kuna mtu anafika chuo kikuu anasoma na anaelimika na kuna anafika chuo kikuu anatoka kapa japo degree anayo lakini hakuelimika bali alipitia tuu. Hivi ndivyo ninavyomuona mheshimiwa rais wetu. Kutokana na hii ignorance hawezi kuwa hata na chembe ya busara. Ilifikia wakati nikauliza hivi hana waliosoma nae waseme alitoka na GPA gani hapo Mlimani, nadhani degree yake ni PASS tuu ndio maana hana Masters yoyote
  Zaidi ya hizi Doctrate za heshima. Msimsakame sana Rais Kikwete, mambo mengine ni mambo ya I.Q.
   
 12. M

  Mama JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kwani hicho cheo chake kinamwongezea au kupunguza nini hasa? Kwani lazima aitwe kwa surname yake? Kwa nini asiitwe Jakaya ambalo ndilo jina lake halisi?
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Kanali Mstaafu Dakta Mtukufu Rais Jakaya Mrisho Halfani Kikwete
   
 14. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ...Kuweza KUANDIKA na YAKASOMWA bila ya misukosuko yoyote kwa waandishi na wasomaji hao,...i'm some times proud of being Tanzanian...
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Dec 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Njowepo,
  Mkuu mimi naheshimu sana mawazo ya mtu yeyote na mara nyingi napotazama upande wa pili sina maana aloandika ni maneno ya Uongo ama makosa matupu isipokuwa najaribu sana kuangalia kitu kwa rangi mbili - Black and white..Na kuna wakati hujikuta mimi mwenyewe naangukia ktk ile grey color in between kuzungumzia..
  Maelezo ya Pundit mengi yana uzito sana isipokuwa (nilichochambua mimi) ni lugha iliyotumika ambayo nimeiona kuwa ni ya mtaani..Na kusema hivyo sina maana Pundit kakosea isipokuwa ndivyo alivyopendelea kuonyesha mapungufu ya RAIS Kikwete..
  On the other hand nimejaribu kutazama hasa kinachoongelewa kama mapungufu ya kiongozi wetu lakini zaidi nimeona ni swala la TABIA yake kuwa mashakani zaidi ya UONGOZI BORA..Pundit kaliweka kama jibu la Hoja ya Mjengwa kuhusiana na Sifa alizopewa rais Kikwete kama rais wa nchi..sifa ambazo pia nimeziweka zaidi ktk Tabia ya rais Kikwete kuliko sifa za Uongozi bora kama rais. Bila shaka Mugabe anaweza kuwa na sifa zote za tabia inayotakiwa lakini haina maana ni kiongozi bora!..
  Na kama unakumbuka mara nyingi nimezungumza mengi sana humu kukashifu Uongozi wa rais wetu kutokana na kukaa kimya muda mrefu kuhusiana na swala la HUJUMA za UCHUMI wetu kwani mwaka 2007 nilipoenda Bongo linigundua kwamba bila kuondoka kwa Hujuma hizi hatuwezi kamwe kuendelea Kiuchumi..
  Rais Kikweyte pamoja na mapungufu yote kwangu mimi ka deliver kila swala ambalo limekuwa likitutatiza sana Watanzania sema tu bado hesabu ya wahusika ndiyo inatukwaza. Na Nikitazama jinsi rais Kikwete alivyorithi utawala wa Mkapa naweza kusema kwamba hakuna kiongozi Tanzania aliyefanya mengi mazuri KISHERIA kuliko yeye kwanza nikitazama swala la Majambazi..Wakati wa Mkapa ilikuwa unasubiri tu gazeti la kesho usikie Benki gani imeingiliwa, nyumba gani imeingiliwa na majambazi wenye Mapanga.. Askari wetu pia walianza kuwa majambazi, Kodi zilikuwa zikipangwa mezani Rose garden na Chef pride, mali zikiingia nchini na kutoka kama vile hakuna serikali..Sinema ya Darwin's Nightmare ilitushtua wengi na wengine tulitokwa na machozi..Kisha kubwa kuliko yote kwangu mimi binafsi Uhuru wa waandishi,leo hii JF tunabamiza tu na tunamkoma nyani gledi kisawa sawa! - jamani mara mmesahau yale ya Ukonga!.. Yote haya kaweza kuyasimamisha kuhakikisha utawala bora unafanya kazi na leo hii ana deal na most important (kikwazo) issue inayoweza kurudhisha heshima ya nchi yetu - KUONDOA HUJUMA za UCHUMI wakati kasimamisha vizuri thamani ya shilingi kwa miaka 3.. Never dreamed of!

  Kwangu mimi kiongozi kuwa na priorities ndiyo muhimu zaidi, kuhusiana na elimu ama tabia yake hainishtuwi sana kwa sababu sio mtu nayekutana naye mtaani ama kazini. Kisha anaweza kuweka wasomi ktk utekelezaji wa hivyo vipaumbele ambavyo mimi navi support..Kusema kweli, kwangu mimi kajitahidi sana kuziba tobo ambazo Mkapa aliziacha na pia tobo zinazotokana na makosa yake kuwaweka watu kama Lowassa na baraza lake la kwanza la mawaziri..Ninaweza kuona turn around ya rais Kikwete niliyeamchukia mwaka jana kutokana na kuchukua muda mrefu kuziba tobo hizo..Maadam kaweza kuona wapi tunakosea na wapi anataka kulipeleka Taifa hili akianza na Utawala bora nadhani yupo ktk right track hadi sasa hivi kiutawala.

  Sasa Kifupi ni kwamba mkuu Pundit kaandika mapungufu ya rais wetu (BLACK) ambayo nayakubali lakini wakati huo huo mimi nimewakumbusha mazuri ya rais Kikwete (WHITE) hivyo tunapoweka vitu hivi ktk mzani ni rahisi kwetu kuona huo mzani umeelemea upande gani ili tupate kuona hiyo Grey color ktk kupata balance!..

  Tatizo linakuja kwamba wengi wetu humu JF tunapenda sana kuweka jiwe la uzito upande mmoja bila kuweka upande wa pili kitu tunachojaribu kupima..Sikupendelea Mh. rais wetu Kikwete uzito wake uwe pumba tupu wakati nina hakika kafanya mengi mazuri kuliko mabaya hadi sasa hivi.
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mh. Mkandara,

  1. Hapo kweli umenena- shilingi ina pande mbili siku zote Mkuu! Pundit ameangalia upande mmoja tu! A fair and just judgememt of JK ni kuweka mizania ya mapungufu na mema aliyofanya!

  2. On a serious note...if we compare JK na maraisi wa nchi jirani..je hao jirani have they done any better? Angalieni Mutharika, Gwebuza, Banda, Kabila, Nkurunziza, Kagame, M7 na Kibaki: Ktk hawa may be Kagame tu wa Rwanda ndo naona yuko makini zaidi ya JK kwa mabadiliko ya haraka yanayotokea Rwanda sasa hivi!
  Actually ukikaa na majirani zetu..wengi wanatuona Tz na JK kuwa tunaenda vizuri! Sii mmeona Kenya juu ya ufisadi..hata waziri wa fedha alikuwa ankataa kujiuzulu hadi shinikizo kubwa? Mmeona Idara ya Magereza Kenya- Mtu, Mkewe, watoto wawili, wajomba n.k wameajiriwa ktk Idara moja kwa Upendeleo?

  Ingekuwa vema tukapata opinion ya ya jirani over JK pia wana JF!
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2008
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi napata shida sana kuamini kuwa suala la EPA pamoja na kuwa lilianza wakati wa awamu ya tatu (3) lilifanywa na viongozi wa awamu ya tatu (3). In fact tunatakiwa tuelewe hivyo wakati hiyo sio kweli. fedha za EPA zilianza kutolewa kipindi cha mwisho kabisa cha awamu ya tatu (3) kwa mashinikizo mbalimbali ya viongozi wa awamu ya nne (4). Na hata ukiangalia waliofaidika na fedha hizo, sio waliokuwa viongozi wa awamu ya tatu. Uchunguzi ukifanyika sawasawam, utagundua hili.

  Nitashukuru kukosolewa kama siko sahihi.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Dec 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Recta,
  Mkuu naona kama unachanganya vitu hapa.. Ebu rudia kusoma list ya wahusika wa EPA utaona kuwa ni viongozi awamu ya Tatu na kile kikombe kilichofunikwa kinawahusu CCM as a party..
  Fedha zilichotwa kuwapitisha wabunge ktk chaguzi mbali mbali, na hatuwezi kusema hawa walikuwa watu wa rais Kikwete. hata kama angesimama Mwandosya ama Salim bado fedha hizo zingetumika kwa minajiri iliyokusudiwa..
  Ni under Mkapa's watch, fedha hizo zimechukuliwa ktk meza ya mchezo mmoja na aliyelamba dume alikuwa mh. Kikwete..
  Sasa tunapomtazama Kikwete na kutaka kumbebesha lawama zote wakati ukweli ni kwamba CCM (mwenyekiti akiwa Mkapa) ndio waliopanga mechi nadhani tunajaribu kuficha madhambi..
  Wewe unafikiri kwa nini swala la EPA limekuwa gumu zaidi kushughulikiwa kiasi kwamba kina Makamba wanasema mjadala ufungwe!..
   
 19. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe. Ila nadhani kuna mchanganyiko mkubwa zaidi.

  Swala la EPA ni gumu kwa kuwa wahusika ni watu wa karibu wa hao wanaotakiwa kuwashughulikia. Pia swala hili linazidi kuwa gumu kwa kuwa linavipa vyama vya upinzani nguvu Ujiko. Kwa maana linashikiwa kidedea na upinzani zaidi. Kwa maana hiyo, ushughulikiaji wa EPA unakwenda kwa makini, vinginevyo, nguvu ya chama itakwisha, na watakaofaidika sio CCM. Hata kama CCM haikufaidika moja kwa moja na fedha hizo.
   
 20. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Heshima kwako mkuu Pundit;

  Tathmini ya utendaji wa Jakaya Kikwete is up to the mark!! Huyu kiongozi wetu hulka yake ni mvivu wa kufanya kazi na hata kufikiri, wewe uliona wapi kiongozi kila siku yuko barabarani hiyo kazi ya kusoma, kufikiri na kutoa maamuzi ataifanyaje?

  Mambo magumu yanaoyohitaji maamuji yanahitaji taarifa sahihi na ubongo uliotulia. Kiongozi anatakiwa awe up to date kwa kusoma vitabu na hii inanikumbusha thread moja iliyouliza vitabu if any anavyosoma muungwana akifananishwa na wakina Obama.

  Kama anavyosema Pundit teuzi zake nyingi zinaonesha lack of seriousness isipokuwai cronyism. Kwa kutambuakuwa uwezo wake ni mdogo [intellectual dwarfness] angeteua washauri wenye uwezo lakini because of his lack of confidence amezungukwa na vitoto ambavyo vikimuona vinajificha!!

  Angejaribu hata kuiga basi aone mwenzie Obama anavyoteuwa wapambe wake; professionalism ndio key na sio ushikaji. Pundit tunashukuru kwa kazi makini tunangojea muendelezo wa makala yako.
   
Loading...