Wazazi wengi huwaandikisha watoto shule za awali wakiwa na umri wa miaka mitano

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Inawezekana ni kukosa hela au sababu nyingine suala linalofanya wazazi wawapeleke watoto shule wakiwa na miaka mitano ili wakiwa na miaka sita waingia Darasa la kwanza. Hii ni sababu ambayo nimeitoa mimi kwa kuwa Shule za awali nyingi zinamilikiwa na serikali, i.e katika shule 18,554 zilizosajiliwa 89.48% zinamilikiwa na serikali. Hivyo sababu inaweza kuwa kweli wazazi wanapenda kukaa na watoto wao au hawataki kuwapeleka shule mapema ili wapate muda wa kuishi nao nyumbani
1638536443596.png


Hii sio kusema kuwa walio chini ya miaka mitano au zaidi hawaandikishwi shule ya awali angalia graph hii


1638536580403.png


Kwa Idadi hiyo utaona watoto wanaoandikishwa zaidi ni wenye miaka 5, ambao hukaa mwaka mmoja na kuingia darasa la kwanza wakiwa na miaka 6 wazazi wanaopeleka watoto wakiwa na miaka 3 ni wachache sana, huku wengine wengi wakiwapeleka watoto shule za awali wakiwa wamechelewa


Data zilizotumika ni kutoka TAMISEMI

 
Kwani ukimpeleka na miaka 3, unategemea aanze la kwanza akiwa na miaka 4? Thubutu! Ukimpeleka ana miaka 3, maanake ni kuwa atakuwa shule ya awali kwa miaka 2-3 kabla ya kuanza la kwanza.
 
Nchi inaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni. Kuna umri wa kuanza la 1, kuna umri wa binti kuruhusiwa kuolewa kisheria, kuna umri wa kuruhusiwa kupiga kura, kuna umri wa kuruhusiwa kugombea ubunge, kuna umri wa kuruhusiwa kugombea urais (miaka 41), nk, nk.
Hiv mtoto hawezi kuanza darasa la kwanza na miaka minne?
 
Sahihi ni miaka 4. Angalau mtoto ana uwezo wa kuweza kujieleza pale anapokutana na ukatili. Kumbuka watanzania wengi uwezo wa kupeleka watoto TIS haupo wengi wanapeleka shule zetu hizi ambazo waangalizi wengi hawajali. Kweli mtoto wa miaka 3 anapewa kichapo kama vile mtoto wa form 4 na uangalizi hakuna. Chini ya hapo ni kumfanya mtoto amuone mzazi kama katili asiyejali.
 
Safi. Za siku? Vipi mjomba hajambo? Na mke mwenza wako (yaani mke wa uncle)?
Sahihi ni miaka 4. Angalau mtoto ana uwezo wa kuweza kujieleza pale anapokutana na ukatili. Kumbuka watanzania wengi uwezo wa kupeleka watoto TIS haupo wengi wanapeleka shule zetu hizi ambazo waangalizi wengi hawajali. Kweli mtoto wa miaka 3 anapewa kichapo kama vile mtoto wa form 4 na uangalizi hakuna. Chini ya hapo ni kumfanya mtoto amuone mzazi kama katili asiyejali.
 
Inategemea na mtoto mie nilitofautiana vikali sana wajinga waliokuwa wanapinga mwanangu wa miaka 5 kuanza class 1 japo like la awali hakuliudhuria sawasawa pia hakuwa fiti kutoka na situation za KORONA Ila next year anaingia class 2 na yupo fresh tuu.

Muhimu kumshape mtoto ajue anafanya nn nyumbani na shuleni pili watoto wasikuhz wanakuwa mapema Yan wanajua vingi kwa uharaka hvyo kuwahi Shule n muhimu to me 4-5yrs class 1 inawezekana
 
Wanawaishwa wengine hadi miaka miwili. Kuwahi kumpelela mtoto shule haimaanishi unampenda saana na kumtakia mema bali ni kukwepa majukumu yako kama mzazi. Wazazi wengi hawana muda wa kuwalea watoto wao hivyo kuendelea kukaa nyumbani ni mzigo kwao hivyo option nzuri ni kumpeleka shule. Umri sahihi wa mtoto kuanza darasa la kwanza ni miaka saba, basi angalau 6 kwa wale wenakua haraka(kimwili na kiakili)
 
Back
Top Bottom