Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,514
Habari wakuu,
Husika na kichwa cha habari,
Niende moja kwa moja kwa mada yetu ya wazazi wengi wa Sasa kuwa na umri mkubwa na wana watoto wajukuu.
Ukikutana na wababa au wamama wengi wa Sasa wanawatoto wadogo sana, hii imepelekea na hali ya maisha ya kuchelewa kuoa au kuolewa.
Moja kati ya sababu kubwa ya kuchelewa kuoa na kuolewa ni kwakuwa watu wengi Sasa wamekuwa waoga kuoa.
Hii ni kutokana na kuona vitimbi vinavyowasibu baadhi ya wanandoa na kupelekea kuchelewa sana.
Hivyo wanakuwa wanakaa kwanza kusubiria kwanza jua likuchwe ndio wanaingi kwenye ndoa.
Pia sababu kubwa sana ni hali ya maisha kwa ya watu, maisha yamekuwa magumu, hivyo wanaume wanasaka pesa kwanza ndio waingie kwenye ndoa.
Sasa hali hii ya kuchelewa inapelekea kuoa na kuolewa umri ukiwa umeenda na wanazaa watoto ambao kwa umri wao wanaonekana kama wajukuu.
Swala la malezi nalo linakuwa gumu kwao kwakuwa umri umewatupa mkono, wanaona kama wapo na wajukuu.
Hivyo inakuwa ngumu kuwakemea watoto, wanakuwa wanawadekeza, si ndo washakuwa bibi na babu.
Watu wanaochelewa kuoa na kuolewa ndio chanzo Cha mmomonyoko wa maadili kwa watoto waliopo mtaani huko.
Wazazi wao hawajali watoto kwakuwa umri umeshawatupa mkono.
Ni vyema kuzaa watoto mapema ili kupata muda wa kuwalea vizuri.