Habari,
Nina mchumba wangu ambaye nimepanga kwenda kujitambulisha kwao mwezi huu August lakini kwa sasa niko kwenye hali ngumu kwa kuwa wazee wangu wa huku Meru hawataki nioe Mchaga na wanasema ni bora ningeoa Mmeru kuliko Uchagani wakitoa sababu tofauti tofauti.
Mchumba wangu huyu ni mchanganyiko wa Mkibosho(mama) na Mmachame(baba) ingawa nilishakuwa na uhusiano na binti wa Kimeru na ndio wamekazia hapo?
Nifanyeje? Hivi ingawa ni tabia ya mtu binafsi lakini nani zaidi kati ya Mmeru na Mchaga?
Duuh kwa style hii mwishowe itafika hata sisi watanga tutakosa mume/mke kisa Mmbondei, Mdigo,Msambaa, Mungu tusaidie.
Pole kwa yaliyokukuta . Ila naomba ukae na wazazi wako tena dear ... Waeleweshe mapendekezo yako na ulichokiona tofauti kwa mchumba wako mpaka unatamani na kutaka kumuoa huyo my Wifi ... Pole sana. Ukiona bado hawataki hebu jaribu tena kama tunavyoendaga kumuomba Mungu . But kama ikiwa bado hawataki dear wasikilize tuu your parents because wao wanaona mbali , wana wisdom and they are your Parents aliyekuchagulia Mungu .... Again pole sana...Thanks..