Kabila linaweza kubadilika kutoka kabila moja hadi jingine?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Huwa ninawashangaa watu wanaojisifia makabila yao katika msingi wa damu. Naamini, kama vipimo vya DNA vingefanyika, kuna watu wangejishangaa kufahamu kuwa hawana uhusiano wa damu na kabila analojinasibu nalo.

Kabila, kwa mtazamo wangu, msingi wake ni utamaduni na si damu.

Miaka ya nyuma, nilikutana na watu kadhaa ambao makabila yao yalikuwa na asili ya kabila jingine.

Mmoja aliniambia kuwa yeye ni Mchaga wa Marangu, lakini babu yake na bibi yake walikuwa ni Wamasai kutoka Arusha. Babu yao aliamua kwenda kununua ukoo kwa Wachaga baada ya kutokea ugomvi baina yake na ndugu zake na kupelekea kulikana kabila lake. Kipindi babu yake anaenda kuomba ukoo kwa Wachaga, tayari baba yake msimuliaji alishazaliwa. Hiyo inamaanisha Mmasai alihamia uchagani na watoto wake aliowazaa Arusha Umasaini, hivyo uzao wake uliopatikana Uchagani ni wajukuu.

Mwingine aliniambia yeye ni Mnyakyusa lakini babu na bibi yake walikuwa Wapare.

Mwingine ni familia moja ambayo japo walikuwa wakijitambilisha kuwa kabila lao ni Waarusha, asili yao ni Wameru. Udadisi wangu uliniwezesha kufahamu kuwa japo kwa damu wao ni Wameru, kabila la Waarusha walilipata kupitia babu yao aliyehamia kwa Waarusha.

Miaka ya nyuma, mtu alipotaka ardhi kutoka kwa Waarusha, akiuziwa au kupewa bure, anakuwa sehemu ya hiyo familia iliyompa ardhi. Kwa sababu huyo Mzee alipewa ardhi na Mwarusha, alijihesabu kuwa yeye ni ukoo mmoja na mtu aliyemwuzia/ aliyempa shamba (sikumbuki kama aliuziwa au alipewa bure).

Huyo Mzee japo aliaga dunia mwaka 2006, mpaka sasa uzao wake (watoto, wajukuu, vitukuu) wanajitambulisha kuwa ni kabila la Waarusha japo wana ndugu zao wa damu Meru ambao kabila lao ni Wameru.

Kwa mifano hiyo michache, ni wazi kuwa kabila la mtu si damu pekee, bali utamaduni. Mtu anaweza akawa na damu tofauti na ya kabila analojinasibu nalo

Inafahamika kuwa chimbuko la Mzee Lowassa ni Wameru. Hata sasa anaweza akawa ana ngmdugu zake wa damu kule Meru ambao ni WA kabila la Wameru. Lakini Mzee Lowassa yeye na familia yake kwa sasa kabila lao ni Wamasai.

Hata Wachaga, inasemekana ni mchanganyiko wa Wamasai, Wakamba, Wakahe, Wasambaa, na Wataita.

Kwa sababu hiyo basi, hata ikitokea umeamua kumuasili mtoto mchanga ambaye katelekezwa na kabila lake haijulikani, usione tashwishwi kumwita kabila lako.

Kabila si damu. Ni utamaduni.

Makabila yanaweza kubadilika!
 
Ni muingiliano wa kijamii tu,
Kuna wsnyasa wengi tu walizama mwakaleli huko na kyela wengi tu wakatengeneza familia,tena wengine waliharibu kwa machifu kabisa wanatafutwa waliwe kichwa wakakimbia kwingine mbali huko wakajificha.
Hamna jipya.
 
nafikiri ni kikundi cha watu kinaweza kujimega na kujiunga na kabila jingine

kama pale meru kuna wamachame walijimega na wamasai wote wakajichanganya na kua wameru mbaya zaidi wakazaliana wao kwa wao kwa wingi sana
 
Ni muingiliano wa kijamii tu,
Kuna wsnyasa wengi tu walizama mwakaleli huko na kyela wengi tu wakatengeneza familia,tena wengine waliharibu kwa machifu kabisa wanatafutwa waliwe kichwa wakakimbia kwingine mbali huko wakajificha.
Hamna jipya.
Wanyasa ni kabila? Bado wanajitambulisha kwa hilo kabila?
 
Huwezi kubadili kabila, hiyo ni kama ngozi ya mwili
Ila unawesa kujifunza na kuishi kama makabira mwengine
Inawezekana sijakuelewa mkuu. Unamaanisha nini kusema hivyo?

Unataka kusema kila mtu anayejulikana kuwa ni Mnyakyusa ana damu (DNA) ya Kinyakyusa?

Chukulia mfano, mwanamke wa Kihehe kazaa na mwanaume wa Kimakonde lakini mwanamke, kwa maslahi yake binafsi, akamdanganya mtoto kuwa baba yake ni Mfipa. Huyo mtoto akijiita yeye ni Mfipa atakuwa sahihi?
 
Mimi nilishauliza hapa je naweza kubadili kabila?

 
Kama DNA zitafanyika watu wengi either ni wachagga au wasukuma ama wamasai,sababu ya msingi ni kuwa haya makabila ni ya watu wanaohama hama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.mfano ni rahisi kumkuta mchanga yupo songea ama rukwa na kwenye hiyo mikoa akizaa na mwanamke huko ni wazi mtoto atapewa kabila la mama.kwa hiyo Kwa nyakati hizi hakuna kabila lolote lenye purity yake ya asili
 
Back
Top Bottom