Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26. Nipo ktk mahusiano ya kimapenzi na binti wa kichaga kwa zaidi ya mwaka 1, bint ni mrefu kidogo kwangu na ni mwembamba afu maji ya kunde, ni mkristo na mpenda Mungu. Huyu bint nampenda sana nae ananipenda na kunijar, amekuwa mshauri wangu. Lakini jambo linalotesa akili yangu ni kwamba familia yetu hawawapendi kabisa wachaga kwa madai kwamba wachaga wanapenda sana kuwashika maskio wanaume (kuwatawala) , pia wachaga wanatabia ya kutaka mume ajenge na kupeleka pexa uchagan na sio kwa mama ake mzazi. Mpaka sasa nipo njia panda, mtoto namuelewa sana nae ananielewa sana lakn mtihan upo kwenye familia yangu. Mnisaidie wadau, nifanye nini ktk hili suala?