Kwanini vijana wa sasa hawataki uhusiano wa muda mrefu

jastertz

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
392
743
Utafiti unaonyesha kuwa mitazamo ya vijana wa kizazi cha sasa cha milenia kuhusu uchumba na ngono ni tofauti na watangulizi wao.

Watu waliozaliwa kati ya mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 wanaitwa Generation Z kwa lugha ya kingereza, wanatafuta njia ya kupenda na kufanya ngono. Lakini hawatoi kipaumbele cha kuwa na uhusiano rasmi na imara wa kimapenzi, kama vizazi vilivyopita.

Ingawa hii haimaanishi kuwa hawapendi mapenzi na urafiki. Badala yake, wanatafuta njia mpya za kutimiza matakwa na mahitaji ambayo ianafaa zaidi katika maisha yao. Mabadiliko haya yameunda dhana ya 'Situationship'. Inayoelezea kati ya urafiki na uhusiano.

'Situationship' ni nini?
Wataalamu wanasema neno 'Situationship',imetolewa kuelezea hatua isiyoelezeka ya uchumba, ni maarufu sana miongoni mwa Kizazi Z (Generation Z) cha vijana wa sasa. "Sasa, ni ngono, urafiki, ukaribu, chochote kile kinachokidhi aina fulani ya hitaji. Sio lazima kudumu kwa muda mrefu," anasema Elizabeth Armstrong, profesa wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani ambaye natafiti jinsia na uhusiano.

Baada ya kupata umaarufu Mwishoni mwa 2020, Armstrong anasema neno hilo lilitafutwa kwa kiwango cha juu kwenye utaftaji wa Google mwaka huu. Kuanzishwa kwa neno hili na kuongezeka kwake kati ya wachumba wachanga kunaonyesha jinsi Kizazi Z (Generation Z) kilivyo tofauti na watangulizi wao. Pia inafichua mengi kuhusu jinsi wanavyounda upya mapenzi na ngono.

Uhusiano huu si lazima 'ufike mbali'
Situationship kwa kawaida ni uhusiano usio rasmi kati ya watu wawili. kuna vipengele vya mawasiliano ya kihisia na kimwili. Lakini inafanya kazi nje ya dhana ya kawaida ya kuwa katika uhusiano rasmi na wa pekee wa kimapenzi.

Katika baadhi ya matukio, 'Situationship' ni mpangilio wa kawaida unaofaa kwa hali ya sasa. Kwa mfano, hii inaweza kutumika kwa wanafunzi wawili wa mwaka wa mwisho wa chuo kikuu ambao hawataki kuendelea na uhusiano imara wa kimapenzi kwa sababu kazi mpya baada ya kuhitimu zinaweza kuwapeleka kwenye miji mipya.

"'Situationship' ni maarufu kwa sababu inapinga 'vichochezi vya uhusiano," anasema Armstrong. Uhusiano wa kimapenzi unapaswa kuwa safari ya moja kwa moja yenye malengo ambayo yanavuka hatua muhimu za uhusiano kama vile kuishi pamoja, uchumba na ndoa. "Dhana ya 'Situationship' ni kinyume cha wazo kwamba kuwa na mtu ambaye atageuka katika uhusiano rasmi ni 'kupoteza muda'," anasema.

Generation Z inaipenda sana. Badala yake watu katika uhusiano wa aina hii huchagua hali hii isiyoeleweka ya uhusiano usiobainishwa kwa hiari yao wenyewe. 'Situationship' inafaa kwa mazingira ya sasa. Haijalishi uhusiano unafika wapi.

Baadhi ya tafiti zinakubaliana na hili. Lisa Wade, profesa mshiriki wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Tulane nchini Marekani, alisema katika mahojiano aliyofanya na wanafunzi 150 wa shahada ya kwanza katika mwaka wa masomo wa 2020-2021, Generation Z inasitasita zaidi kufafanua uhusiano au hata kukubali hamu ya kuendelea.

"Si jambo geni kwa watu kuficha mawazo na matamanio yao. Lakini utafiti wake unaonyesha kuwa kizazi cha leo hakitaki hata kushirikishana hisia zao," anasema. Kwenye mitandao ya kijamii, watumiaji wa TikTok na Tweeter, haswa Generation Z, huchapishai sana simulizi kuhusu Situationship.

Kwenye TikTok, video zilizowekwa alama ya #situationship zimetazamwa zaidi ya mara milioni 83.9. Neno hili pia huonekana kwenye vipindi maarufu vya kuchumbiana kama vile Love Island UK na katika nyimbo kama vile Situationship za mwimbaji wa Uswidi Snow Allegra.

"mimi na marafiki zangu, sote tunaishi maisha sawa," anasema Amanda Human, mwenye umri wa miaka 26. Human, iliyoko Texas, ameandika uzoefu wake wa uhusiano wa situationship kwenye TikTok.

Anasema uhusiano huu ni wa kawaida anapoangalia watu anaokutana nao na wanaomzunguka. "Nadhani imekuwa sehemu maarufu sana ya utamaduni wa kuchumbiana. Angalau kwa kizazi Z na vijana wa milenia, unaweza kuona hilo."

Kwa nini Situationship inaongezeka?
'Generation Z' inapoingia katika ulimwengu wa uchumba, kuna changamoto za kisasa za kutafuta mapenzi. Kwa mfano, zama za Corona zimebadilisha kabisa jinsi watu wanavyokutana na kuchumbiana. Na uchumba mtandaoni umekuwa na athari kubwa.

Zaidi ya hayo, vijana wengi hawatii mkazo sana katika uchumba kama walivyofanya zamani. Kukabiliana na mgogoro wa hali ya hewa, kupanda kwa mfumuko wa bei, msukosuko wa kisiasa na kijamii na uchumi unaoyumba, vijana wanazidi kujishughulisha na maendeleo binafsi na kitaaluma ili kuwa na hali nzuri ya kifedha.

"Vijana wanasema kuwa mahusiano yanawavurugia malengo yao ya kitaaluma na kazi. Na ni bora kutojihusisha sana kwa sababu sio lazima kuyatoa maisha yako kwa ajili ya mtu mwingine," anasema Wade.
Matokeo yake, uhusiano wa Situationship unawafaa. Hii inawaruhusu kutoacha malengo mengine kwa sababu ya kimapenzi na ngono. Jambo hilo "linapanua chaguzi za watu," Armstrong anasema. Watu wengi huichagua badala ya kuikwepa.

Je, kuna hatari gani katika Situationship
Hii haimaanishi kuwa hakuna hatari katika uhusiano huu unaodaiwa kuwa haueleweki. Wade anasema 'situationship' inaweza kinadharia kutumika kama chombo cha "uaminifu mkubwa." Hili linawezekana ikiwa watu wawili watazungumza waziwazi juu ya kile wanachotaka na kukubaliana juu ya masharti ya uhusiano huo.

Lakini kwa vitendo inaweza kuwa vigumu kulinganisha vipaumbele vya watu wawili. Ikiwa pande zote mbili hazitakuwa na maelewano juu ya kile wanachotaka, 'situationship' inaweza kuisha vibaya.

Anasema mara nyingi hii hutokea wakati mtu yuko tayari kuendelea na uhusiano rasmi, lakini hofu ya mabadiliko huwazuia wote wawili kuijadili. Kuongezeka kwa mapenzi ya 'situationship' katika ulimwengu wa kisasa wa uchumba kunaonyesha mabadiliko ya jinsi vijana wanavyochukulia mapenzi na ngono.

Kizazi cha leo kinachukua njia ambayo watu wengi wa vizazi vilivyopita waliepuka. Hooman anasema ameridhika na mtindo huu wa maisha. "Ni chaguo langu. Ni uamuzi wangu. Nina furaha kwamba inanifaa," anasema. "Mradi watu wanajisikia vizuri na wanaona ni sawa, hawajali kuhusu matarajio ya badaye yatakuaje," aliongeza.
 
Aliesoma gazeti atupe tips!
Nlianza kusoma Kwa umakini lakn gafla nkaanza kuscroll chap chap kuokoa mda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom