Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Wazanzibari kuwasilisha petition UN

sasa bwana wewe unadhani ni kwanini wenzetu kila siku ni kulalamikia kua huu muungano hauwafai!? kwann sisi ndio pekee ambao tunakomalia kua unamanufaa!? hapo suala la situation kabla ya muungano halina mashiko cha msingi ni wote turidhie bas..... kwa inavyoonekana huu muungano ulikuwepo kwa ajili ya kulinda maslah mapana ya wakubwa huko ughaibuni thats why hakuna rais ambae hua anajihusisha kwa lolote na process zinazoweza kupelekea kuvunjika kwa hii ndoa.
Kunywa kreti moja ya bia nakuja kulipia popote ulipo bro na nauli ya tax nalipia [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenye madai ni wazanzibar lakini cha ajabu hapo hapo mnatokea na nyie wadanganyika kutoa madai yenu bila ya kuyapeleka popote zaidi ya kuwapigia makelele wazanzibar wanaofata sheria kudai mamlaka yao yalioporwa na kiini macho cha muungano.
Madai ya Tanganyika ni yapi? Tofautisha madai na hoja

Sina tatizo na wznz kufuata sheria, sina tatizo na kiti chao UN.
Ni tatizo na sababu za wazanzibar ambazo kila uchao hubadilika.

Zile za kunyonywa kiuchumi zimefilia mbali, zimefinyangwa finyangwa hakuna tena.
Sasa zimeiubuka za hati, kwanini hakuna hiki znz hakuna kile

Sababu za misaada nazo zimefilia mbali, kisema misaada unapaswa kuzungumzia madeni
Pamoja na hayo kuna hoja isiyojibiwa, katika muungano znz inachangia nini na kwa kiasi gani

Tafuteni sababu nzuri na kila la kheri, si kughilibu umma kuhusu muungano ambao basically una faida kwenu kuliko kwa Mtanganyika.
 
Kwani mandela au afrika kusini ilipata uhuru kwa siku moja?ni wazi walihangaika sana,kwa hiyo msiwe mnapiga makelele wakati wazanzibar wakitafuta mamlaka yao kwa njia za kisheria.
 
Kujifurahisha kisheria kwa vijikesi kesi na vijipetition rukhsa, hala hala msije kuwachangisha watu pesa za wakili, kwa sababu hakuna kesi hapo!.

  1. Tanzania is one country, URT, a sovereign state, hakuna anayeweza kuingilia mambo yetu ya ndani, sio mahakama yoyote ya nje sio UN.
  2. Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania.
  3. Jamuhuri ya Tanganyika is dead, haiwezi kufufuliwa, na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pia is dead, haiwezi kufufuliwa.
  4. Zanzibar iliyopo sio nchi, ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani, hakuna sehemu yoyote ya JMT, inayoweza kwenda popote, kudai kutaka kujimega toka JMT!.
  5. Muungano wetu sio wa merger, yaani sio wa kuunganisha, kiasi utasema tutaumega, muungano wetu ni wa fussing, kama chemical reaction ya two chemical zika undergoes a chemical reaction na kuunda a new compound, hakuna tena process ya kuirudisha into its original forms.
  6. Muungano wetu ni wa milele, zile articles of union, zili provide kuungana tuu na hakuna kuachana!.
  7. Kwa vile muungano haukufanyiwa ratification kwa upande wa Zanzibar, then jengeni hoja ya kufanya ratification sasa kupitia BLW, ndipo likatae ku ratifying mseme Zanzibar wamekataa.
  8. Kwa vile muungano ni wa watu, na Zanzibar wana sheria ya kura ya maoni, wawaulize Wanzanzibar, wakisema hawautaki muungano, then watumieni wawakilishi wenu kupitia BLW litoe azimio, mlilete kwenye Bunge la JMT, lijadiliwe, na sisi Tanzania tuulizwe, tukikubali, ndipo sasa itungwe sheria ya kuuvunja muungano, tugawane fito.
  9. Muungano unaweza kumalizwa kwa kuundwa mahakama ya katiba ndio yenye uwezo wa kuuzungumza muungano wetu na sio UN.
  10. Kwa vile kiasili Zanzibar, ni sehemu ya Tanganyika/Tanzania iliomegeka miaka mingi nyuma, then ni Tanzania pekee ndie mwamuzi wa mwisho, airuhusu Zanzibar iende au la sio UN.
Rejea.
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!. - JamiiForums

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. - JamiiForu
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani? - JamiiForums

P.
Wale ma sheikh wa uamsho walikua wanaweza kufanikisha ila ndo habari yao kwisha. Kwa viongozi tulionao afrika,njaa kali.(matumbo yao na familia zao kwanza)
 
Kwani mandela au afrika kusini ilipata uhuru kwa siku moja?ni wazi walihangaika sana,kwa hiyo msiwe mnapiga makelele wakati wazanzibar wakitafuta mamlaka yao kwa njia za kisheria.
Hakuna anayelalamika, tunawashauri tu kuwa huko UN kiti ni cha Tanzania sasa suala limeshajadiliwa nyumbani? Hapo ndipo patakuwa na swali, kwamba mambo ya ndani yameshindikana? Kama yameshindikana ni kwa jitihada zipi, bungeni, vikaooni au vipi

Tunawatakia kila la kheri katika kuitafuta haki, hata hivyo haki inaambatana na ukweli

Madai ya kupata kiti ni madai ya kuvunja muungano. Hilo sina tatizo kama litaamuliwa na wananchi
Tatizo ni sababu zisizo na kichwa wala miguu ambazo nyingi leo tunajua ni uzushi tu dhidi ya Tanganyika
Kwamba, ZNZ inanyonywa kiuchumi! upi huo na nani anaweza kumkamua ng'ombe asiye na ndama
 
Huna haja ya kumtukana,hii mbinu ya kuwagawa(ubaguz) wazanzibar kwa upemba na uunguja ililetwa kwa makusudi ili kuwatawala wazanzibar.
kama unaweza kufundishwa kumchukia nduguyo, mpuuzi ni wewe unayefunzwa si mwalimu
 
Kanisa linalinda sera zake,kinachoogopewa kuvunjika kwa Muungano ni kuipa Zanzibar nguvu za kisiasa na za kidini,...kanisa linafanya kila hila kitu kama hicho kistokeee,..Serikali ya Tanzania haina dini,lakini kwa hili la kadhi serikali imekuwa na dini

Unakumbula mjadala wa kutaka Kadhi ulivyoibua mambo ya ajabu ajabu ya kidini,...wakati upande mmoja wa Mungano kuna Ofisi ya Kadhi lakini upande wa Tanganika umekataa kata kata jambo hilo lisiwepo, wanawanyima waislamu haki yao ya kiiimani..
Haya yana uhusiano gani na petition ya UN?
 
Muungano ni wa kulazimisha sana, ni muungano wa kibabe ndiyo maana hata idadi kubwa ya wanajeshi waliopo Zanzibar wanatoka Tanganyika ili kuzuia mapinduzi, waache Zanzibar ijitawale kila mmoja akae kwake, tuwe Nchi Jirani kama Comoro, Madagascar na Nchi zingine.
Na pengine ndio sababu ya Wazanzibar wengi kuishi bara
 
Zanzibar tuacheni ubaguzi tunafikiri tukitenganisha zanzibar na tanganyika ndio tutapata maendeleo...wala! Hatutapata hamtaweza ndio maana rais wenu karume aliona kuwa kuna haja ya kuungana

Umoja ni nguvu kama kuna mahali hapako sawa tuparekebishe na sio kuua muungano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna anayelalamika, tunawashauri tu kuwa huko UN kiti ni cha Tanzania sasa suala limeshajadiliwa nyumbani? Hapo ndipo patakuwa na swali, kwamba mambo ya ndani yameshindikana? Kama yameshindikana ni kwa jitihada zipi, bungeni, vikaooni au vipi

Tunawatakia kila la kheri katika kuitafuta haki, hata hivyo haki inaambatana na ukweli

Madai ya kupata kiti ni madai ya kuvunja muungano. Hilo sina tatizo kama litaamuliwa na wananchi
Tatizo ni sababu zisizo na kichwa wala miguu ambazo nyingi leo tunajua ni uzushi tu dhidi ya Tanganyika
Kwamba, ZNZ inanyonywa kiuchumi! upi huo na nani anaweza kumkamua ng'ombe asiye na ndama
Unatumia sindano za kujitoa ufahamu na dripu za ukijani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar tuacheni ubaguzi tunafikiri tukitenganisha zanzibar na tanganyika ndio tutapata maendeleo...wala! Hatutapata hamtaweza ndio maana rais wenu karume aliona kuwa kuna haja ya kuungana

Umoja ni nguvu kama kuna mahali hapako sawa tuparekebishe na sio kuua muungano

Sent using Jamii Forums mobile app
bila shaka ww si mzanzibari ww ni mamluki kutoka Tanganyika
 
kama unaweza kufundishwa kumchukia nduguyo, mpuuzi ni wewe unayefunzwa si mwalimu
Na kama ndugu hao wamerudi kuwa wamoja na kumtambua adui yao basi mwalimu anabaki na upuuzi wake.
 
Back
Top Bottom