Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Rejesheni tanganyika yenu sio kukaa na kuanza lawama,hii mbeleko ya muungano mnayo itegemea kuna siku mtakuja kulia machozi ya damu,muda utaongea.
Onyesha mbeleko inayotumiwa na Tanganyika kwa jambo moja tu

Hapa ndipo kuna unafiki mkubwa. Wazanzibar ndio waliokataa rasimu ya Warioba iliyotaka kutenga nchi hizi. Kwa Watanganyika haikuwa na madhara, kwa wznz walinusa matatizo wakakataa

Tanganyika ikiwepo kama serikali, mbeleko ya muungano kwa wznz itakuwa hadithi

Ndani ya vikao vya tume ya Wariona, waliosisitiza mashirikiano ya lazima kati ya nchi mbili ni wazanzibar
Walisema iwepo haki ya ardhi kwa kutumia neno mtu anaweza kuishi popote
Wakasema iwepo haki ya ajira, kwamba mtu anaweza kufanya kazi popote

Wakasema ushirikiano uwe katika ulazima wa kwamba nchi moja ikiwa na tatizo la KIUCHUMI isaidiwe na mshirika. Hapa walijihani kwasababu tatizo la uchumi wa Tanganyika haliwezi kutatuliwa na ZNZ

Leo tungekuwa na bunge dogo la watu 50 la shirikisho na kupunguza gharama za Wabunge zaidi ya 100 kutoka ZNZ wanaokuja Dodoma kwa mambo si zaidi ya 7 , mengine wakisubiri posho

Wizara ya serikali za mitaa, kilimo, uvuvi, umwagiliaji, mawasiliano, afya, elimu ya juu na chini, biashara, zinawahusu wznz katika eneo gani? Kwanini wawe na kura au maamuzi ya vitu visivyo vya muungano

Unafiki wa pili ni kukimbiza mafuta na gesi kutoka katika muungano. Hatuwasikii wakiondoa elimu ya juu

Mara tukasikia waliokataa rasimu ni CCM siyo wazanzibar, wznz wenyewe walitaka serikali 3
Hii ilikuwa lugha nyepesi na laini kwa maana ya wale kutoka na wale wa kuzaliwa...

Unafiki mwingine ni ule wa mkataba wa muungano. Hivi mkataba huo utasaidiaje Tanganyika
I mean kupitia mkataba huo Tanganyika itanufaika na kitu gani.

Of course znz itanufaika ndio maana ya upuuzi wa mkataba. Hilo halitawezekana hata kwa bahati mbaya. Ikitokea vinginevyo kila mtu na njia yake. Hakuna kuweka vishikizo
 
Kujifurahisha kisheria kwa vijikesi kesi na vijipetition rukhsa, hala hala msije kuwachangisha watu pesa za wakili, kwa sababu hakuna kesi hapo!.

  1. Tanzania is one country, URT, a sovereign state, hakuna anayeweza kuingilia mambo yetu ya ndani, sio mahakama yoyote ya nje sio UN.
  2. Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania.
  3. Jamuhuri ya Tanganyika is dead, haiwezi kufufuliwa, na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pia is dead, haiwezi kufufuliwa.
  4. Zanzibar iliyopo sio nchi, ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani, hakuna sehemu yoyote ya JMT, inayoweza kwenda popote, kudai kutaka kujimega toka JMT!.
  5. Muungano wetu sio wa merger, yaani sio wa kuunganisha, kiasi utasema tutaumega, muungano wetu ni wa fussing, kama chemical reaction ya two chemical zika undergoes a chemical reaction na kuunda a new compound, hakuna tena process ya kuirudisha into its original forms.
  6. Muungano wetu ni wa milele, zile articles of union, zili provide kuungana tuu na hakuna kuachana!.
  7. Kwa vile muungano haukufanyiwa ratification kwa upande wa Zanzibar, then jengeni hoja ya kufanya ratification sasa kupitia BLW, ndipo likatae ku ratifying mseme Zanzibar wamekataa.
  8. Kwa vile muungano ni wa watu, na Zanzibar wana sheria ya kura ya maoni, wawaulize Wanzanzibar, wakisema hawautaki muungano, then watumieni wawakilishi wenu kupitia BLW litoe azimio, mlilete kwenye Bunge la JMT, lijadiliwe, na sisi Tanzania tuulizwe, tukikubali, ndipo sasa itungwe sheria ya kuuvunja muungano, tugawane fito.
  9. Muungano unaweza kumalizwa kwa kuundwa mahakama ya katiba ndio yenye uwezo wa kuuzungumza muungano wetu na sio UN.
  10. Kwa vile kiasili Zanzibar, ni sehemu ya Tanganyika/Tanzania iliomegeka miaka mingi nyuma, then ni Tanzania pekee ndie mwamuzi wa mwisho, airuhusu Zanzibar iende au la sio UN.
Rejea.
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!. - JamiiForums

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. - JamiiForums

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani? - JamiiForums

P.
Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania
.Hivi kwa nini kuna Tanzania BARA na kuna Zanzibar amabayo nilitarajia kuitwa Tanazania viswani? pia tumekuwa na bendera ya Zanziba na ya Tanzania??
 
Onyesha mbeleko inayotumiwa na Tanganyika kwa jambo moja tu

Hapa ndipo kuna unafiki mkubwa. Wazanzibar ndio waliokataa rasimu ya Warioba iliyotaka kutenga nchi hizi. Kwa Watanganyika haikuwa na madhara, kwa wznz walinusa matatizo wakakataa

Tanganyika ikiwepo kama serikali, mbeleko ya muungano kwa wznz itakuwa hadithi

Ndani ya vikao vya tume ya Wariona, waliosisitiza mashirikiano ya lazima kati ya nchi mbili ni wazanzibar
Walisema iwepo haki ya ardhi kwa kutumia neno mtu anaweza kuishi popote
Wakasema iwepo haki ya ajira, kwamba mtu anaweza kufanya kazi popote

Wakasema ushirikiano uwe katika ulazima wa kwamba nchi moja ikiwa na tatizo la KIUCHUMI isaidiwe na mshirika. Hapa walijihani kwasababu tatizo la uchumi wa Tanganyika haliwezi kutatuliwa na ZNZ

Leo tungekuwa na bunge dogo la watu 50 la shirikisho na kupunguza gharama za Wabunge zaidi ya 100 kutoka ZNZ wanaokuja Dodoma kwa mambo si zaidi ya 7 , mengine wakisubiri posho

Wizara ya serikali za mitaa, kilimo, uvuvi, umwagiliaji, mawasiliano, afya, elimu ya juu na chini, biashara, zinawahusu wznz katika eneo gani? Kwanini wawe na kura au maamuzi ya vitu visivyo vya muungano

Unafiki wa pili ni kukimbiza mafuta na gesi kutoka katika muungano. Hatuwasikii wakiondoa elimu ya juu

Mara tukasikia waliokataa rasimu ni CCM siyo wazanzibar, wznz wenyewe walitaka serikali 3
Hii ilikuwa lugha nyepesi na laini kwa maana ya wale kutoka na wale wa kuzaliwa...

Unafiki mwingine ni ule wa mkataba wa muungano. Hivi mkataba huo utasaidiaje Tanganyika
I mean kupitia mkataba huo Tanganyika itanufaika na kitu gani.

Of course znz itanufaika ndio maana ya upuuzi wa mkataba. Hilo halitawezekana hata kwa bahati mbaya. Ikitokea vinginevyo kila mtu na njia yake. Hakuna kuweka vishikizo
Kama hoja ni unafiki kwenye muungano huu basi tanganyika(ccm) ndio bingwa wa unafiki,wameifuta tanganyika lakini wanasheherekea uhuru wa tanganyika kila mwaka.
 
Suala la Wazanzibari kuwasilisha petition kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutaka kurejeshewa kiti chake na mamlaka yake yaliyoporwa na Taifa la Tanganyika kwa kisingizio cha kuwepo kwa Muungano uliokosa misingi ya kisheria katika kuanzishwa kwake, ambapo hivi sasa suala hilo liko Mahakamani kwa kuhojiwa kisheria. petition hiyo, itawasilishwa kwa utaratibu maalumu wa kisheria za kimataifa mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ili nae aiwasilishe mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa iweze kujadiliwa kwa mujibu wa utaratibu wa baraza hilo.

Hata hivyo, wasimamizi wa suala hili wanawaomba Wazanzibari walio ndani na nje ya Zanzibar waendelee kufuatilia hatua zinazoendelea kuchukuliwa kwa misingi ya sheria za kitaifa na kimataifa ili kwa muda mfupi ujao nchi yetu irejee kuitumia haki yake ya uhuru,uwanachama wake wa kudumu UN na mamlaka yake kitaifa na kimataifa, na kuwa na ushirikiano wa kirafiki na watu na Mataifa ya jirani Tanganyika, Kenya, Uganda, Burundi, Ruwanda, Sudani na nchi zote za Umoja wa Afrika na ulimwengu mzima.

Kwa heshima ya sheria za kimataifa za ushirikiano bila ya ubaguzi wa aina yoyote, kazi hii inaendelea kufanywa na viongozi wetu wanao simamia hizi kesi, na baadhi ya wanasheria wa ndani ya Zanzibar na nje ya Zanzibar kwa manufaa ya Wazanzibari wote.
# AjendaYaZanzibar
Muungano una dosari nyingi mno na dosari hizo ni neema kwa wengi wanaoupigania.Najiuliza pale tunapoambiwa kuna serikali ya muungano na ile ya mapinduzi kuwa iko wapi ile ya tanganyika?Ina maana kuwa baada ya muungano serikali ya tanganyika ilikufa lakini ikabaki ile ya mapinduzi Zanzibar.Hivi mimi siwezi kuishi visiwani na kumiliki ardhi?Siwezi kuishi visiwani na kumchagua sheha,mjumbe wa wawakilishi,rais wa smz?Kwa nini kuna utofauti wa haki?Wazanzibar wanataka waone bendera yao pale New york kwa sababu wana Serikali yao.Hawa watu wamegundua kuwa kile chama cha njano na kijani kimejenga kasumba ya kupitisha wagombea wa urais wa Muungano kutokea bara kwa kutumia wingi wa wajumbe.Nawaunga mkono,wssikate tamaa kutafuta haki.
 
Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania
.Hivi kwa nini kuna Tanzania BARA na kuna Zanzibar amabayo nilitarajia kuitwa Tanazania viswani? pia tumekuwa na bendera ya Zanziba na ya Tanzania??
Mkuu Mhagos, muungano wetu ni very unique duniani kwa sababu ni muungano wa kipekee, kwa nje ni union, kwa ndani ni fereration.

Miungano mingine yote ni ama ni miungano ya union, ama ni miungano ya federation. Miungano ya union ni nchi mbili zinaungana zinakuwa nchi moja, nchi hizo mbili zilizoungana, xote mbili zinapoteza utaifa wake, yaani sovereignty na kuipa nchi mpya kama ilivyotokea kwa Tanganyika na Zanzibar, zote zimepoteza utaifa wake likaundwa taifa jipya la Tanzania.

Miungano mingine ni federation, ambao nchi zilizoungana, zinakuwa taifa moja, lakini nchi hizo zikimaitain utawala wake wa ndani.

Muungano wetu ni wa kipekee kwa sababu kwa upande mmoja muungano wa union, lakini ndani ya hiyo union, kuna ka federation cha Zanzibar, chenye utawala wake wa ndani. Huo utawala wa ndani wa Zanzibar mwisho Chumbe. Ndani ya muungano, Tanzania ni nchi moja yenye sehemu mbili, Tanzania Bara, na Tanzania Visiwani, au Tanzania-Zanzibar, hivyo kwa ndani muungano wetu ni federation, yenye nchi mbili za Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, yenye serikali mbili, ya JMT ambayo ni ya muungano na SMZ ya Zanzibar na yenye marais wawili, rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Nje ya muungano, Tanzania ni nchi moja ya Union, yenye serikali moja ya JMT na rais mmoja, na amiri jeshi mkuu. Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya JMT. hivyo ile bendera ya Zanzibar, wimbo wa taifa wa Zanzibar, vikosi vya SMZ ni mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayatambuliki nje ya Zanzibar au kimataifa.

Muungano wetu ni sawa na ndoa, wanandoa ni kitu kimoja na wanaishi nyumba moja kwa nje wanatambulika kwa jina moja, nyumba ya bwana fulani, lakini kwa ndani, kuna watu wawili, baba na mama, baba ndie mkuu wa nyumba anaitawala nyumba nzima, lakini ndani ya nyumba, mama ndie mtawala wa jikoni na chumbani, ndiye huamua apike nini, au atandike shuka za rangi gani, kwenye mambo ya ndani, mama ana uhuru wake, avae nini, apike nini, ajirembe vipi na hapaswi kuingiliwa. Zanzibar ina utawala wake wa ndani, kama mama, haipaswi kuingiliwa, lakini yakija masuala ya nje na ya kimataifa, ni baba, Tanzania.

P.
 
Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania
.Hivi kwa nini kuna Tanzania BARA na kuna Zanzibar amabayo nilitarajia kuitwa Tanazania viswani? pia tumekuwa na bendera ya Zanziba na ya Tanzania??
Ibara ya 4 ya mkataba wa Muungano imeiruhusu serikali ya muungano kuyasimamia mambo 11 tu ya muungano.
Halafu ibara hiyo hiyo ya 4 imetoa ruhusa
kwa serikali ya muungano kuyasimamia
na kuyaendesha mambo ya Tanganyika.
Je kwa katiba gani?. Je muungano wetu
umekuwa ni wakala na kitumishi cha
kuitumikia serikali ya Tanganyika?
Tena akawa Rais wa Tanganyika ndio
Rais wa Muungano, na Bunge la Tanganyika likawa ndio bunge la Muungano?
Na katiba ya Tanganyika ikawa ndio katiba
ya Muungano?
Dhamira ya haya munaijuwa tokea kuasisiwa kwake, bahati mbaya wenzetu munaumwa na chama kuliko nchi. Endapo akitokezeya mtu kuyasema haya na mengine utasikia Hizbu uyo hautakii mema Muungano wetu. Kumbe BT inafanya kazi yake.
Wenzetu wa ndio mzee tulikubaliana mengi yenye maslahi kwa Zanzibar na Wazanzibari mlitugeuka basi leo kuita watu madogi si suluhisho. Pako pahala tumekosea. Alhamdulillah kwa kila mwenye nia thabit na Zanzibar bado
 
Muungano wowote unaweza kuvunjika kutokana na sababu nyingi tu
Endapo nchi moja inaweza kugawanyika kuwa mbili sembuse muungano
 
Kwa mtazamo wangu maisha yatasonga na itakuwa business as usual ingawa kutakuwa na adjustments kwenye government and its 3 branches of power;

The executive: JPM ataendelea kuwa head of state. Atateua mawaziri wapya kuziba nafasi za akina prof. Mbarawa

Legislative: wabunge wa Mrima wataendelea na majukumu yao

Judiciary: Chief Justice ataendelea na majukumu yake
Kwa KATIBA gani JPM aendelee KUWA Rais? wakati alikuwa Rais Wa Muungano na Muungano HAUPO? Shein ana Haqi ya kuendelea kutawala sababu alichaguliwa na wazanzibari!
 
Back
Top Bottom