Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Tatizo upande wa bara kuna mbuni aliyeona dhoruba ana-dodomeza kichwa shimoni; upande wa pili kuna mtu anakula keki taamu anayotaka hiyo keki yenyewe (ya Dodoma) iendelee kuwepo!
 
Kwanini UN na siyo Dodoma?
Iko wapi petition ya Wazanzibar iliyowakilishwa Dodoma, tukijua wana wabunge wao
Iko wapi petition iliyowasilishwa baraza la wawakilishi ikiwa ndani ya baraza ni wao peke yao

JokaKuu Mag3
Kesi ya nyani umpe nyani?
 
Tuzanzibari tuchache .... ndio tunaleta figisu hizo....kama vp zipigwe kura
.....tuone
 
Kujifurahisha kisheria kwa vijikesi kesi na vijipetition rukhsa, hala hala msije kuwachangisha watu pesa za wakili, kwa sababu hakuna kesi hapo!.

  1. Tanzania is one country, URT, a sovereign state, hakuna anayeweza kuingilia mambo yetu ya ndani, sio mahakama yoyote ya nje sio UN.
  2. Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania.
  3. Jamuhuri ya Tanganyika is dead, haiwezi kufufuliwa, na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pia is dead, haiwezi kufufuliwa.
  4. Zanzibar iliyopo sio nchi, ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani, hakuna sehemu yoyote ya JMT, inayoweza kwenda popote, kudai kutaka kujimega toka JMT!.
  5. Muungano wetu sio wa merger, yaani sio wa kuunganisha, kiasi utasema tutaumega, muungano wetu ni wa fussing, kama chemical reaction ya two chemical zika undergoes a chemical reaction na kuunda a new compound, hakuna tena process ya kuirudisha into its original forms.
  6. Muungano wetu ni wa milele, zile articles of union, zili provide kuungana tuu na hakuna kuachana!.
  7. Kwa vile muungano haukufanyiwa ratification kwa upande wa Zanzibar, then jengeni hoja ya kufanya ratification sasa kupitia BLW, ndipo likatae ku ratifying mseme Zanzibar wamekataa.
  8. Kwa vile muungano ni wa watu, na Zanzibar wana sheria ya kura ya maoni, wawaulize Wanzanzibar, wakisema hawautaki muungano, then watumieni wawakilishi wenu kupitia BLW litoe azimio, mlilete kwenye Bunge la JMT, lijadiliwe, na sisi Tanzania tuulizwe, tukikubali, ndipo sasa itungwe sheria ya kuuvunja muungano, tugawane fito.
  9. Muungano unaweza kumalizwa kwa kuundwa mahakama ya katiba ndio yenye uwezo wa kuuzungumza muungano wetu na sio UN.
  10. Kwa vile kiasili Zanzibar, ni sehemu ya Tanganyika/Tanzania iliomegeka miaka mingi nyuma, then ni Tanzania pekee ndie mwamuzi wa mwisho, airuhusu Zanzibar iende au la sio UN.
Rejea.
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!. - JamiiForums

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. - JamiiForums

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani? - JamiiForums

P.
Pasco umesema kweli kwa maneno. Lakini najiuliza haya uliyoyapendekeza yanawezekanaje Tanzania ya sasa na iliyopita? Hakuna BLW litakalojadiliwa kwani hii ni ajenda ya CCM. Hakutaundwa mahakama ya katiba kwani inajulikana wazi matokeo ya kuundwa kwa mahakama hiyo. Hili la kuwa Tanzania pekee ndie mwamuzi wa mwishi ndio hasa moja ya sababu kwanini Wazanzibari wanaenda UN.
 
Wazanzibar wangeachiwa waamue wenyewe hatma ya mambo yao,wapewe Uhuru wautakao wajiendeshe wenyewe tuungane kwenye mengine, iweje nchi moja zenye kodi tofauti, Znz nafuu ukija bara unalipa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao walishaamua kama wananchi tatizo ni kiapo cha maraisi, kuwa nitaulinda muungano. Hilo neno ndio huwa kifungu. Kumbuka kiapo ni kiapo hilo ndio tatizo.
Kingine ni mtazamo wa chama tawala juu ya Muungano.. kwani kuna maoni ya wananchi ambayo kiuhalisia sio ya kuvunja muungano lakini kwa sababu mtazamo wa chama uko tafauti basi ndio inakuwa tatizo

mwanza kwetu
Mkuu mbona weshaamua zamani lakini hawasikilizwi. Watawala wao wanasema Zanzibar ikiachiliwa ni tishio kiuchumi na kiusalama. Na hili wanalisema mchana kweupe!
 
Kwanini UN na siyo Dodoma?
Iko wapi petition ya Wazanzibar iliyowakilishwa Dodoma, tukijua wana wabunge wao
Iko wapi petition iliyowasilishwa baraza la wawakilishi ikiwa ndani ya baraza ni wao peke yao

JokaKuu Mag3
Wee jamaa huwa wa kwanza kuchangia once ukidondoshwa uzi kuhusu Wazanzibari .. . yakhe vipi yakhee wapemba washamega mzigo nini?
 
Wazanzibar wangeachiwa waamue wenyewe hatma ya mambo yao,wapewe Uhuru wautakao wajiendeshe wenyewe tuungane kwenye mengine, iweje nchi moja zenye kodi tofauti, Znz nafuu ukija bara unalipa tena
Hakuna sababu, wakiondoka ni jumla

Kuungana nusu nusu ni ili iwe nini.
 
Mkuu mbona weshaamua zamani lakini hawasikilizwi. Watawala wao wanasema Zanzibar ikiachiliwa ni tishio kiuchumi na kiusalama. Na hili wanalisema mchana kweupe!
Lini walifanya hayo?
Unakumbuka bunge la katiba, waliokataa serikali 3 ni wao na huo ungekuwa mwanzo mzuri kwao

Hawa wznz wana aina zao. Walio Dodoma si wzn halisi, wanaoingia NEC ya CCM ni wazawa wa Mkuranga. Walio Baraza la wawakilishi uzanzibar wao una walakini.
Hao wa UN ndio wznz halisi! Uzanzibar una sifa zake ati
 
Wanasema wangekuwa mbali sana kimaendeleo Bila muungano
Muungano umezuia nini kwao?

Sasa hivi wanalalamika maziwa yanatozwa kodi. Wanalalamika magari na TV zinatozwa kodi
Bara ndilo soko lao na uchochoro unabanwa. Kama wana uwezo kwanini wasiuze Somalia na Djibout

Hivi wangekuwa mbali zaidi ya sasa ambako hawana bill hata za umeme, soko la ajira bure bara, ardhi n.k. Bara ndio wanawaweka maana idadi yao ikirudi znz ni shida!

Nini wanachochangia kiasi cha kudumaza uchumi wao

Kwani wamezuiwa kufanya kipi hadi sasa kiasi cha kuona hawawezi kuendelea

Hata sasa wanaweza kurudi kwao wakajenga nchi yao, hawalazimishwi kuishi bara
 
Back
Top Bottom