Wazanzibari kuwasilisha petition UN

Wazanzibari kuwasilisha petition UN

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
833
Reaction score
1,212
Suala la Wazanzibari kuwasilisha petition kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutaka kurejeshewa kiti chake na mamlaka yake yaliyoporwa na Taifa la Tanganyika kwa kisingizio cha kuwepo kwa Muungano uliokosa misingi ya kisheria katika kuanzishwa kwake, ambapo hivi sasa suala hilo liko Mahakamani kwa kuhojiwa kisheria. petition hiyo, itawasilishwa kwa utaratibu maalumu wa kisheria za kimataifa mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ili nae aiwasilishe mbele ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa iweze kujadiliwa kwa mujibu wa utaratibu wa baraza hilo.

Hata hivyo, wasimamizi wa suala hili wanawaomba Wazanzibari walio ndani na nje ya Zanzibar waendelee kufuatilia hatua zinazoendelea kuchukuliwa kwa misingi ya sheria za kitaifa na kimataifa ili kwa muda mfupi ujao nchi yetu irejee kuitumia haki yake ya uhuru,uwanachama wake wa kudumu UN na mamlaka yake kitaifa na kimataifa, na kuwa na ushirikiano wa kirafiki na watu na Mataifa ya jirani Tanganyika, Kenya, Uganda, Burundi, Ruwanda, Sudani na nchi zote za Umoja wa Afrika na ulimwengu mzima.

Kwa heshima ya sheria za kimataifa za ushirikiano bila ya ubaguzi wa aina yoyote, kazi hii inaendelea kufanywa na viongozi wetu wanao simamia hizi kesi, na baadhi ya wanasheria wa ndani ya Zanzibar na nje ya Zanzibar kwa manufaa ya Wazanzibari wote.
# AjendaYaZanzibar
 
Kwanini UN na siyo Dodoma?
Iko wapi petition ya Wazanzibar iliyowakilishwa Dodoma, tukijua wana wabunge wao
Iko wapi petition iliyowasilishwa baraza la wawakilishi ikiwa ndani ya baraza ni wao
Pengine maswali hayo hayo uliyoyauliza kuhusu Zanzibar tujiulize na sisi Tanganyika vivyo hivyo kwa nini imekuwa hivyo.
 
Kwanini UN na siyo Dodoma?
Iko wapi petition ya Wazanzibar iliyowakilishwa Dodoma, tukijua wana wabunge wao
Iko wapi petition iliyowasilishwa baraza la wawakilishi ikiwa ndani ya baraza ni wao peke yao

JokaKuu Mag3
sioni umuhimu wa muungano zaidi ya kuibana tanganyika isipumue,wapeni kinchi chao tubaki na tanganyika yetu..ajenda za kijinga za kuimeza zbar kama hazikutimia kipindi cha giza miaka 54 iliyopita haziwezi kutimia sasa
 
Kujifurahisha kisheria kwa vijikesi kesi na vijipetition rukhsa, hala hala msije kuwachangisha watu pesa za wakili, kwa sababu hakuna kesi hapo!.

  1. Tanzania is one country, URT, a sovereign state, hakuna anayeweza kuingilia mambo yetu ya ndani, sio mahakama yoyote ya nje sio UN.
  2. Muungano wetu ni union, sio federation, tumeungana tumekuwa kitu kimoja, URT, hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika, hakuna nchi inayoitwa Zanzibar, zote zili surrender their sovereignty na kuunda nchi moja ya Tanzania.
  3. Jamuhuri ya Tanganyika is dead, haiwezi kufufuliwa, na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pia is dead, haiwezi kufufuliwa.
  4. Zanzibar iliyopo sio nchi, ni sehemu ya JMT, yenye utawala wake wa ndani, hakuna sehemu yoyote ya JMT, inayoweza kwenda popote, kudai kutaka kujimega toka JMT!.
  5. Muungano wetu sio wa merger, yaani sio wa kuunganisha, kiasi utasema tutaumega, muungano wetu ni wa fussing, kama chemical reaction ya two chemical zika undergoes a chemical reaction na kuunda a new compound, hakuna tena process ya kuirudisha into its original forms.
  6. Muungano wetu ni wa milele, zile articles of union, zili provide kuungana tuu na hakuna kuachana!.
  7. Kwa vile muungano haukufanyiwa ratification kwa upande wa Zanzibar, then jengeni hoja ya kufanya ratification sasa kupitia BLW, ndipo likatae ku ratifying mseme Zanzibar wamekataa.
  8. Kwa vile muungano ni wa watu, na Zanzibar wana sheria ya kura ya maoni, wawaulize Wanzanzibar, wakisema hawautaki muungano, then watumieni wawakilishi wenu kupitia BLW litoe azimio, mlilete kwenye Bunge la JMT, lijadiliwe, na sisi Tanzania tuulizwe, tukikubali, ndipo sasa itungwe sheria ya kuuvunja muungano, tugawane fito.
  9. Muungano unaweza kumalizwa kwa kuundwa mahakama ya katiba ndio yenye uwezo wa kuuzungumza muungano wetu na sio UN.
  10. Kwa vile kiasili Zanzibar, ni sehemu ya Tanganyika/Tanzania iliomegeka miaka mingi nyuma, then ni Tanzania pekee ndie mwamuzi wa mwisho, airuhusu Zanzibar iende au la sio UN.
Rejea.
Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!. - JamiiForums

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. - JamiiForums

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani? - JamiiForums

P.
 
sioni umuhimu wa muungano zaidi ya kuibana tanganyika isipumue,wapeni kinchi chao tubaki na tanganyika yetu..ajenda za kijinga za kuimeza zbar kama hazikutimia kipindi cha giza miaka 54 iliyopita haziwezi kutimia sasa
Kuibana Tanganyika tena!!
 
Back
Top Bottom