Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
69,855
137,242
Habari za weekend.....

Wauzaji wa bidhaa za forever living, kwanza hongereni kwa kufanya hiyo biashara inayohitaji kipaji cha hali ya juu kuweza kuongea sana na kumshawishi mteja, ni kipaji kwakweli.

Back to topic, mmekua mnatumia mbinu za uongo na kulazimisha sana mteja ili mtangaze biashara aaagrrrr hii mbinu yenu Inakera sana,inaboa sana

Mfano 1: siku za karibuni nikialikwa mahali, nikaambiwa ni semina nauliza semina ya nini nikaambiwa semina tu nihudhurie napigiwa simu za kusisitiza nikaona isiwe tabu ngoja niende nikaahirisha vitu vya muhimu kwenda semina, kumbe ni kwenda nyumbani kwa mtu kuoneshwa bidhaa za forever, wtf? Kwanini umdanganye mtu? Can you imagine nilikua nafeel vipi wakati naoneshwa hizo bidhaa? Mxyu nilikua nimekasirika sana

Mfano 2: dada mmoja kwenye group la whatsapp alitoa mwaliko, jaman karibuni kwangu sehemu flani kuna shughuli, msosi na bia vipo mtakula mtakunywa mtasaza, tunauliza ni nini ubarikio, engagement au nini mchango vipi anakomaa nyie njooni tu eeeh walaji na wanywaji wakaenda eneo la tukio wamevaa suti kumbe ni kuoneshwa bidhaa za forever, Wiki nzima group kimya hakuna anaeongea kumbe watu wamenuna

Mfano 3: Wauzaji wa online, mtu anasema una mtaji wa laki njoo whatsapp tufanye biashara ukiuliza biashara gani unaambiwa njoo whatsapp, unaenda whatsapp anakutumia video la mb 100 kutangaza forever.

Hii ni mifano michache, hivii hamuoni mnakwaza watu? Hakuna mbinu nyingine za kutangaza bidhaa zenu bila uongo??? Au bila kudanganya hamuuzi? Mnakera sanaaaaa
Ni hayo tu
 
Ni kweli aisee, wanaboa sana.

Kuna siku wamenitoa Mbezi mpaka Makumbusho nikajua bonge la mchongo.

Mwisho wa siku nakuta ni ishu za forever Living, nili mind sana aisee, basi tu utu uzima nikaamua kupotezea.

Hawa jamaa wanaboa sana, usiombe wakapata namba yako ya simu, utakoma
 
Ha ha ha ha ha pole sana
Yani huko nlikoenda nlikuta bidhaa zimefichwa chini ya meza, meza imefunikwa na khanga
Nilikua nimekasirika mwanzo mwisho
 
Hii mbinu ya kuwaita watu na kuwapa vinywaji na chakula watawapata wengi kumbe..
mimi siku zote nikiona kitu sikielewi elewi huweni kunishawishi

eti semina halafu hujui semina inahusu nini....na unaenda?

Hizi mbinu wanazopewa hizi kama mkeo yuko huko na akili za kushikiwa 'watamlamba hadi basi'
manake wauzaji wote wa bidhaa za mtandao wako so desperate kushindana kuleta member wapya
na kuuza bidhaa....
 
Ha ha ha nlienda sio kwa uzumbukuku nop niliheshimu tu alienialika, plus simu za kila dakika nilivofika kabla sijaingia nikauliza sio mambo ya forever, hata yeye hajui anasema sidhani..... Kuja kuoneshwa bidhaa anatoa macho tu
 
Da! Nilikasirika sana aisee, Wiki kama mbili napigiwa simu kuna jambo la muhimu sana Mbagala kwa mshikaji wangu nisikose Jumapili. Mzee nikajitosa nikaenda, tukaanza kunywa na kula halafu baadae jamaa akatuletea watu wanaanza kuongelea mambo ya Forever utafikiri anahubiri neno la Mungu, kwa kweli nilichukia hadi jamaa akajua na baadae akaniomba msamaha. Ni upuuzi sana huu.
 
Okay nimekupata.
_____________
Hii ni Gari aina ya Jeep Grand Cherokee ya Kimarekani yenye thamani ya zaidi ya milioni 90 za Kitanznaia mpya kabisa yaani 0 km iliyonunuliwa na dada Huyu Blandina Njau kama wiki sita zilizopita naye anafanya biashara hii ya Forever Living.
Aghrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom