Tamu na chungu baada ya kujiunga na forever living products

kekule benzene

JF-Expert Member
Sep 28, 2016
1,240
2,987
Habarini za weekend wakuu, leo nimepitia nyuzi mbalimbali zinazohusu forever living products, nikaamua na Mimi niweze kushare kitu kuhusu hii kampuni.

Kwanza nakiri kuwa niliwahi kujiunga na biashara hii na nikadumu kwa miaka miwili tu Kisha nikaacha. Yafuatayo ni miongoni mwa niliyoyapata kuyafahamu

1. FL company sio utapeli
- ni biashara ya mtandao inayojihusisha na uuzaji wa virutubisho lishe (food supplements) ambavyo husaidia kuimarisha afya ya mwili.
_ ni biashara ya kuuza na kununua Kama biashara nyinginezo, juhudi zako na uwezo wako wa kuuza ndio utakupa uhai katika biashara

2. Biashara ya FLP ni biashara inayohitaji elimu kwa kiwango kikubwa
_ Inahitaji uwe msomaji haswa, ujue products Zina nini?? Zinasaidia nini?? na ujue kuziuza

3. Biashara ya FLP Inahitaji muda mwingi kuijenga

_ TOFAUTI na watu wanavyoaminishwa na uplines wao kwamba ukijiunga tu utafanikiwa haraka haraka

_ Hii ni trick tu ya kukutaka uingie haraka bila kujiuliza uliza
_ biashara hii Inahitaji ujipe muda na uzoefu angalau miaka mitatu

4. Bidhaa za FLP ni ghari Sana, unaweza ukakuta Kuna package hadi ya 1M

5. Watu wengi huwa wanajiunga na kushindwa kumaster biashara hiyo
_ watu wengi wanaojiunga kwa kutegemea slope ya kupata pesa hufeli mapema mno na hatimaye kuacha Kama mimi😂😂

6. Kuna watu wengi wamefanikiwa na wanafanikiwa kwa biashara hii

_ ili ufanikiwe unahitajika uwe smart Sana, kujifunza na kufanyia kazi

_ Kuna watu nawafahamu kila mwezi wanapiga 5M+ kwa biashara hii

_ Kuna watu nawafahamu wameacha kazi kwa biashara hii

7. Kuna watu wengi wameumizwa na biashara hii

_ Kuna watu waliojiunga wakatoa gharama ya kuanza kununua products za mwanzo (za kujiunga), Kisha wakalipia matangazo fb (ads), kulipia bando kwa ajili ya matangazo na online meeting, kuhudhuria mikutano nk mwisho wa siku usiuze hata bidhaa moja ndani ya miezi au mwaka

8. 80% ya wanaojiunga na biashara hii huamua kuacha kutokana na kushindwa kumaster biashara hii (Hii no kutokana na data rasmi ambazo nilisikia kutoka kwa viongozi wakubwa kwenye mkutano wao pale Millennium tower - makumbusho

9. Watu wengi waliofanikiwa kwenye biashara hii wamepitia machungu ila hawasemi

_ watu wengi waliofanikiwa kwenye biashara hii wamepitia machungu mengi na changamoto nyingi I'll huwa wanataja upande wa mazuri tu bila kutaja hizo changamoto
10. Bidhaa za forever ni nzuri Sana ila wauzaji wengi hawazijui mwisho mteja huona bidhaa hazifanyi kazi

- wauzaji wengi hulazimisha kuuza hata kwa mtu ambaye anajua haitomsaidia, unakuta mtu ana kisukari anauziwa multimacca ila atibu nguvu za kiume, ni kitu ambacho hakiwezi kutokea hata kwa miujiza, lazima mtu aweze kudeal na kisukari kwanza (diabete reversion/remission) Kisha ndio aweze kupata nguvu za kiume

10. Bidhaa za FLP sio kwa ajili ya kila mtu

- ni kwa ajili ya watu wanaojali afya zao, watu ambao wanajua umuhimu wa afya zao na wanahitaji kuzipambania kwa gharama yoyote ile.

11. Biashara hii si kwa ajili ya kila mtu
_ Ni kwa ajili ya watu wenye uthubutu, wachapakazi, wavumilivu, wanaoweza kuoambania ndoto zao

11. Ni biashara nzuri, kwani haihitaji movement nyingi

_ Ni swala la kukaa nyumbani tu , mtu anakutumia pesa , unatuma ofisini Kisha wao wanamtumia

12. Unaweza kuifanya pasi na mtaji wa kununua bidhaa
- kinachotakiwa uweze kuuza bidhaa ndani ya miezi miwili (1.3M) ili uweze business owner rasmi (assistant supervisor)

_ Kuna watu wapo sharp wanawapata watu pamoja na kuanza kutengeneza faida ndani ya muda huo (miezi miwili) ila ni wachache

SABUBU ILIYONIFANYA NIACHE
_ Niliingia kwenye biashara nikiwa Sina Shaka kwani mtu aliyeniingiza ni collegemate na mamjua vizuri, na mabadiliko yake ya kiuchumi nayafahamu toka ajiunge na kampuni hii
_ Niliacha kazi hii kwa sababu haikuonesha matunda kwangu

_ To be honest Mimi sio mtu wa kuongea sana, sio mtu wa shobo, sio mtu wa kupend kuwafuatilia fuatilia watu. Mambo yote hayo ni hayaendani na falsafa ya biashara.

USHAURI KWA WANAOHITAJI KUJIUNGA

_ FLP ni biashara hai na ipo hai ila Inahitaji watu smart wanaohitaji kujifunza na kufanya kazi

_ Hakuna pesa za kudownload
 
Hizi kampuni zote za network markerting kama hiyo ya forever ni utapeli mtupu, wanafanya biashara zao kwa kulazimisha mtu kununua bidhaa bila kujali huyo mtu atapataje soko.

Kwanza bei za bidhaa zao ni kubwa ukilinganisha na bidhaa yenyewe, pia ni kwanini wampangie mtu kiasi cha bidhaa za kununua, kama sio utapeli wangemuacha mtu achague mwenyewe anataka bidhaa ngapi kulingana na pesa aliyonayo na sio kupanga kiasi cha chini cha kununua bidhaa.

Wanaofanikiwa ni wachache sana ukilinganisha na wanaokwama naweza nikasema ni chini ya asilimia kumi ndiyo wanaofanikiwa.

Haya makampuni yanauza bidhaa zao kwa kuforce zaidi kuliko kujitangaza kutokana na ubora wa bidhaa zao.
 
Hizi kampuni zote za network markerting kama hiyo ya forever ni utapeli mtupu, wanafanya biashara zao kwa kulazimisha mtu kununua bidhaa bila kujali huyo mtu atapataje soko.

Kwanza bei za bidhaa zao ni kubwa ukilinganisha na bidhaa yenyewe, pia ni kwanini wampangie mtu kiasi cha bidhaa za kununua, kama sio utapeli wangemuacha mtu achague mwenyewe anataka bidhaa ngapi kulingana na pesa aliyonayo na sio kupanga kiasi cha chini cha kununua bidhaa.

Wanaofanikiwa ni wachache sana ukilinganisha na wanaokwama naweza nikasema ni chini ya asilimia kumi ndiyo wanaofanikiwa.

Haya makampuni yanauza bidhaa zao kwa kuforce zaidi kuliko kujitangaza kutokana na ubora wa bidhaa zao.
Nadhani uliyoyaongea yanafanana na niliyoyasema


ila point ya msingi sio utapeli, ni biashara Kama biashara nyinginezo ambazo nazo watu hufeli

Binafsi simshauri mtu ajiunge hasa akiwa anataka mafanikio ya muda mfupi bila kutoa jasho
 
FL Nilikosana na mtu mpaka leo kisa nilikataa.

Kuna hii Neolife nayo nilichomoa,
Ila nilichogundua Sio kwamba hizi biashara (specifically hii neolife ambayo kuna rafiki yangu anaifanya, hivyo naona) zote ni utapeli full, ila utapeli unakuja pale ukiwaamini kwenye mafanikio ya haraka bila jasho...

Yule Dada niliyemchomolea hio Neolife, kiuhalisia anauza, na hii ni kutokana na wateja wake HASA WAKULIMA, ila Amesota Mwaka wa pili huu ndio naona anazungusha, dawa zake na bidhaa zinamatokeo mazuri inshu ni bei...


Ni nyingne ni nzuri zaidi ukiwa na duka la Dawa, pembejeo za kilimo Au Vipodoezi.....
 
Kuna Mpori pori anatafutwa hapa kupigwa.
Kwa kifupi hiyo FL inakufanya uwe Machinga Msomi. Ni Utumwa Mamboleo unaoratibiwa Kisomi mnooo na pesa unapigwa pia.
Epuka huu Utumwa
Tatizo la JF kila mtu mjuaji sana

Kuna sehemu nimeandika natafuta downline??

Nimejaribu kutoa experience yangu kuhusu FLP

Binafsi nimepoteza pesa hili sifichi, na nimepoteza muda wangu


Ila sitokuja kusema forever ni utapeli au forever ni umachinga (huo ni uongo)

Ninachoweza kusema ni kwamba sijaweza kuimaster hii biashara, nimeshindwa ila Kuna watu wanauza products kila siku

Ukitaka ujue watu wanafanya hii biashara serious, tarehe 29,30,31 nenda pale ofisini kwao makumbusho uone watu wanavyojaa kufunga mwezi
 
Unaposema 80% wanaacha, hela zao wanarudishiwa? Hizo bidhaa zinaenda wapi?
Kinachofanyika unatakiwa ujiunge kwanza ili uweze kupata faida

Hatua ya mwanzo inaitwa (novus customer) ambapo hapa ni baada ya kujisajili tu bila kununua bidhaa, na hapa hupati faida

Ili uwe full member inabidi ununue package ya almost 1.3M

Hii package ni bidhaa ambazo unaweza unanunua kwa matumizi yako binafsi, au ukanunua Kisha ukauza au ukampata mteja ukamuuzia directly

Cha msingi ufanye manunuzi ya 1.3M either kwa pesa yako au ya mteja

Hapo unakuwa member kamili (assistant supervisor)


Pesa hairudishwi
 
Kwamtu mgeni na hii biashara lazima apigwe,umeeleza kiufundi sana na lazima uokote mtu hapa
Kweli katika watu wanne mmoja ni tahira

Inaonekana wewe ni mmoja wapo

Hakuna sehemu nimeandika namtaka mtu na nimeshasema nimeacha kufanya biashara hii na sababu nimetoa
 
Kinachofanyika unatakiwa ujiunge kwanza ili uweze kupata faida

Hatua ya mwanzo inaitwa (novus customer) ambapo hapa ni baada ya kujisajili tu bila kununua bidhaa, na hapa hupati faida

Ili uwe full member inabidi ununue package ya almost 1.3M

Hii package ni bidhaa ambazo unaweza unanunua kwa matumizi yako binafsi, au ukanunua Kisha ukauza au ukampata mteja ukamuuzia directly

Cha msingi ufanye manunuzi ya 1.3M either kwa pesa yako au ya mteja

Hapo unakuwa member kamili (assistant supervisor)


Pesa hairudishwi
ok. Bidhaa ukishindwa kuuza tafsiri yake imekula kwako.?
 
ok. Bidhaa ukishindwa kuuza tafsiri yake imekula kwako.?
Hapo ni sawa na kwenda kununua mzigo Kariakoo na ukashindwa kuuza😃😃😃


Shida bidhaa Zina gharama kubwa

Asili ya bidhaa zinatengenezwa Marekani, na zinauzwa kwa dollars

Shida ukibadilisha kwenye pesa yetu ndio shida inaanza
 
ok. Bidhaa ukishindwa kuuza tafsiri yake imekula kwako.?
ila sio lazima ununue bidhaa, unaweza unatafuta mteja kwanza ukimpata ndio ukanunua kwa pesa yake


Kipengele kumpata Sasa, na Kama ukiweza kuwapata mwanzoni basi hata huko mbele kutoboa ni simple tu
 
Back
Top Bottom