Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
48,782
2,000
Habari za weekend.....

Wauzaji wa bidhaa za forever living, kwanza hongereni kwa kufanya hiyo biashara inayohitaji kipaji cha hali ya juu kuweza kuongea sana na kumshawishi mteja, ni kipaji kwakweli.

Back to topic, mmekua mnatumia mbinu za uongo na kulazimisha sana mteja ili mtangaze biashara aaagrrrr hii mbinu yenu Inakera sana,inaboa sana

Mfano 1: siku za karibuni nikialikwa mahali, nikaambiwa ni semina nauliza semina ya nini nikaambiwa semina tu nihudhurie napigiwa simu za kusisitiza nikaona isiwe tabu ngoja niende nikaahirisha vitu vya muhimu kwenda semina, kumbe ni kwenda nyumbani kwa mtu kuoneshwa bidhaa za forever, wtf? Kwanini umdanganye mtu? Can you imagine nilikua nafeel vipi wakati naoneshwa hizo bidhaa? Mxyu nilikua nimekasirika sana

Mfano 2: dada mmoja kwenye group la whatsapp alitoa mwaliko, jaman karibuni kwangu sehemu flani kuna shughuli, msosi na bia vipo mtakula mtakunywa mtasaza, tunauliza ni nini ubarikio, engagement au nini mchango vipi anakomaa nyie njooni tu eeeh walaji na wanywaji wakaenda eneo la tukio wamevaa suti kumbe ni kuoneshwa bidhaa za forever, Wiki nzima group kimya hakuna anaeongea kumbe watu wamenuna

Mfano 3: Wauzaji wa online, mtu anasema una mtaji wa laki njoo whatsapp tufanye biashara ukiuliza biashara gani unaambiwa njoo whatsapp, unaenda whatsapp anakutumia video la mb 100 kutangaza forever.

Hii ni mifano michache, hivii hamuoni mnakwaza watu? Hakuna mbinu nyingine za kutangaza bidhaa zenu bila uongo??? Au bila kudanganya hamuuzi? Mnakera sanaaaaa
Ni hayo tu
 
Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
10,764
2,000
Yaan ulipotajs edmark umegusa patamu awa jamaa walinifanya nikope pesa ya nauli na chakula kutoka mbagala mpaka masaki wakaniambia wanatoa ajila baada ya kuwauliza hawakunijib majibu yanayoeleweka mzee nikajitupa kufata ajila nilicho kikuta aisee kidogo nianzishe timbwil
Hahahaha ungeanzisha tu mkuu kwani shi ngap
 
major2

Member
Sep 21, 2016
18
45
Forever living ndio mpango mzima.Acheni kuongea mambo msiyoyajua.Acheni wanaojua tufanye.Tatizo wabongo majungu na tuna Black Mind asilimia kubwa.
 
dihimba

Member
Dec 12, 2016
6
45
Hahahaha ungeanzisha tu mkuu kwani shi ngap
Mkuu waliniambia 160,000 alafu wanipe bidhaa nianze kutembeza wakajalibu kunishawishi uongo WA kiwango cha lami alafu wanavyouzi sasa wanaona mtu kachukia wao wanaendelea kuongea porojo zao eti magar mala nyumba yaani ilimladi visa tu
 
Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
10,764
2,000
Mkuu waliniambia 160,000 alafu wanipe bidhaa nianze kutembeza wakajalibu kunishawishi uongo WA kiwango cha lami alafu wanavyouzi sasa wanaona mtu kachukia wao wanaendelea kuongea porojo zao eti magar mala nyumba yaani ilimladi visa tu
Yani wanaboaga kinomaa ..eti mfano unakuta mjinga m1 anakwambia mimi nimeacha kazi cjui bank mara nilikuwa engineer wa kampuni flan lakin nmeacha nkajiunga na hii biasharaa. ..eti ndani ya muda mfup tu utakuwa ni bilionea ...mara utaenda sjui marekani, sjui China mara unaskia singapoo, kuna miwatu naifahamu kabisa mpk leo mwaka wa nne toka wajiunge wapogo tuu amna cha marekan wala nin ..
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,511
2,000
Bado tu watu hawakomi kujiunga na hizi pyramid scams?
Deci
Amway
ICN
Forever Living
Organo Coffee
Kryptocoin
GLN sijui GLC
 
2030

Member
Dec 26, 2016
33
70
Yani wanaboaga kinomaa ..eti mfano unakuta mjinga m1 anakwambia mimi nimeacha kazi cjui bank mara nilikuwa engineer wa kampuni flan lakin nmeacha nkajiunga na hii biasharaa. ..eti ndani ya muda mfup tu utakuwa ni bilionea ...mara utaenda sjui marekani, sjui China mara unaskia singapoo, kuna miwatu naifahamu kabisa mpk leo mwaka wa nne toka wajiunge wapogo tuu amna cha marekan wala nin ..
una uhakika?
 
doughter

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
452
500
Hii mbinu ya kuwaita watu na kuwapa vinywaji na chakula watawapata wengi kumbe..
mimi siku zote nikiona kitu sikielewi elewi huweni kunishawishi

eti semina halafu hujui semina inahusu nini....na unaenda?

Hizi mbinu wanazopewa hizi kama mkeo yuko huko na akili za kushikiwa 'watamlamba hadi basi'
manake wauzaji wote wa bidhaa za mtandao wako so desperate kushindana kuleta member wapya
na kuuza bidhaa....
mm mkaka aliniita makumbusho kila nikimuuliza ni kaz gan hesemi..mana nlimwambia nimemaliza chuo si mda npo home tuu akasema kama uko serious njoo ofisini makumbusho basi kufika nkakutna na ile wanaitaje sijui ambayo unachangia laki tano alafu wanakupa limzigo hilooo..sasa nkajiuliza nauzaje na napata wapi hiyo laki tano wanayotamka kirahisi utadhani mia saba hamsini..yaan kila nliemuona pale nkimuuliza alikua hajui nn kinaendelea.....
nilikaa wee mbka njaa ikauma na msosi haukuepo. Naikumbuka bidhaa yao moja inaitwa c24/7 nyingine ni my choco.
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
3,454

Aim Global.
Pale ukienda watakupa story tu hata kutwa nzima ila kula kwenu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom