Wauzaji wa bidhaa mtandaoni sio ndugu zako.Watu wa mikoani mtapigwa sana na watoto wa mjini kisa ubishi na kupenda vitu vya bei rahisi

Kariakooking1978

JF-Expert Member
Jul 11, 2023
552
1,060
Hellow members,Leo nimekuja na tukio lililotokea leo asubuhi baada ya moja ya mteja wangu kuingia mkenge kwenye rada za matapeli.

Ipo hivi mimi najihusisha na kununua/kufuata,kufunga na kusafirisha mizigo kutoka Dar es salaam kwenda mikoa yote Tanzania kila siku na hivyo basi nimeweka Matangazo yangu mengi kwenye mitandao ya kijamii.
Sasa leo asubuhi nilipigiwa simu na mwanadada mmoja akitaka kujua natoaje huduma yangu.Mimi bila kusita nikampa maelekezo yote.
Basi baada ya kuridhika akasema kuwa ana muuzaji wake wa instagram anataka anunue simu aina ya samsang S9 mpya full box na huyo muuzaji kamwambia kuwa anapatikana china plaza,hivyo basi anaomba niifate hiyo simu,niifunge kisha niisafirishe hadi mkoa x.
Sasa baada ya haya makubaliano nikahitaji kujua thamani ya simu ili nimpe tatol cost ya kusafirisha hadi mkoani kwake kwa njia ya basi.Nilipata mshangao baada ya kuambiwa bei ya simu ni 120k (Laki na 20).
Nikamwambia sister kuwa serious basi hii ni kitu ya thamani hivyo taja thamani halisi ili ikitokea imeharibikia mikononi mwetu tukulipe fedha halisi tusije kukulipa 120k ukaanza kusema thamani ya simu ipo juu zaidi.
Baada ya mabishano kidogo,yule sister akaamua kunitumia screenshoot za chatings zake na muuzaji,basi mimi nikasema isiwe kesi ila nikamuonya kuwa kwa aina ya simu na bei nina wasiwasi unaenda kupigwa na kitu kizito,yeye kanijibu hata nisijali.

Baada ya dakika kama kumi hivi nikampigia kumwambia gharama za usafirishaji zitagharimu Tsh 15k kutoka dsm hadi mkoa x na service fee yangu ni Tsh 10,000/= hivo jumla itakuwa 25k.
Yule dada kusikia hizi gharama akanza kuwaka kwamba mimi nina gharama za juu sana ni bora muuzaji wake afunge na kutuma mwenyewe maana kamwambia kutuma ni Tsh 7,000/= tu.Basi mimi nikaona isiwe kesi nikamwambia dada fanya upendalo,akanijibu powa halafu akakata simu.

Toka tumemaliza kuongea yamepita kama masaa 3 hivi yule dada akanipigia simu kwamba kamtumia hela muuzaji wake ila baada ya kupokea hela tu kablock instagram,whatsapp na call za kawaida ko akimpigia hapatikani.
Mimi nikamuuliza kwahiyo unatakaje dada,akasema anaomba msaada wangu niende hapo china plaza nikamtafute yeye atanilipa service fee yangu ya Tsh 10k.
Mimi bila kupindisha maneno nikamwambia dada hiyo hela ushatapeliwa huyo mtu hayupo china plaza wala nini ni kheli ungekubali tumlipe wakati ananikabidhi simu ona sasa umepigwa kisa ubishi.Yule dada aliendela kulalamika mara hela yenyewe kakopa kwenye kikundi mara sijui mume wake atamuelewa vipi.

NB:Mimi kama mzoefu wa kuagiza mizigo kuja huko mikoani,niwaombe tu watu wa mikoani msipende vitu vya bei rahisi wala msipende kukwepa gharama ndogo ambazo zitakahakikisha usalama wa pesa yako au ubora wa bidhaa uliyonunua.
Wauzaji wa mtandaoni sio ndugu zako wakuuzie kitu cha 300k+ kwa 120k.AMKENI AMKENI LASIVYO MTAPIGWA SANA.


Anyway,
Kama una Mzigo wako upo dsm,wewe nicheki tu nitaufuata popote ulipo,nitafunga kisha nitakusafirishia kwa haraka sana.

0745645035-PIGA/SMS/WHATSAPP
 
Simu ya tsh 600K mtu anaambiwa alipie tsh 150K nayeye kama mbuzi mee analipia kweli. Acha tu tuendelee kuitwa wa mikoani.

Kuna wale watu uwaambii kitu kuhusu bidhaa inayotokea dar, kwa mfano the same product ipo mkoa aliopo mhitaji kwa bei rahisi kabisa (dar 200K bila gharama za usafiri, na mkoani 180K ambapo n rahisi kwa ukaguzi na kufikika), hapa wengi wanachagua kutoka dar na mara nyingi wengi hawana mtu wa kuwasaidia kwenye hili kama itatokea changamoto. Sijui sababu n nini?
 
Simu ya tsh 600K mtu anaambiwa alipie tsh 150K nayeye kama mbuzi mee analipia kweli. Acha tu tuendelee kuitwa wa mikoani.

Kuna wale watu uwaambii kitu kuhusu bidhaa inayotokea dar, kwa mfano the same product ipo mkoa aliopo mhitaji kwa bei rahisi kabisa (dar 200K bila gharama za usafiri, na mkoani 180K ambapo n rahisi kwa ukaguzi na kufikika), hapa wengi wanachagua kutoka dar na mara nyingi wengi hawana mtu wa kuwasaidia kwenye hili kama itatokea changamoto. Sijui sababu n nini?
Watu wengi wanakwama hapa.Anashindwa kupiga hesabu ndogo kama hizi
 
Guarantee/security ya mzigo tunakuaminije kaka? Umesajiliwa na TCRA KUSAFIRISHA vifurushi MIKOANI? una leseni? LATRA wanakutambua?
Kampuni zote ninazozitumia kusafirisha mizigo ya wateja wangu zina kila kitu ulichokitaja hapo.

Karibu.
 
Back
Top Bottom