Wauza kahawa wanabeba siri nzito sana sema basi tu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,550
2,000
Baadhi ya wauza kahawa wakichoka kutembea huwa wanafanya mambo ya ajabu sana ilmradi wasitupoteze wateja wao!

Yale mabegi mgongoni yana kila kitu, yana beba mkaa, kiberiti, kashata, Katanga, kopo la kahawa,vikombe n.k

Hiyo ni mbinu za kuhakikisha kahawa inawafikia wateja masaa yote 24 na kuhakikisha moto hauzimiki kama ilivyo mbio za mwenge.

Kwasababu hakuna kazi isiyokosa kasoro, pia hii kazi ina pesa lakini shurti uzingatie masharti.
 1. Sharti la kwanza la kuuza kahawa ni marufuku kupanda daladala au Gari binafsi hata kama utapewa lifti.
 2. Sharti la pili usiwe na haraka na safari .
 3. Usipite kilinge bila kuwasalimia
 4. Usichangie mada mbalimbali za kwenye vilinge n.k
 5. Pitia site na rindo za wateja wako mda muafaka .
CHANGAMOTO
Zipo changamoto mbalimbali za kazi hii ingawa hii ina faida kubwa!
 • Wakati wa jua Kali wateja hupungua,
 • Mabirika ya kahawa ni mazito lakini yanazoeleka
 • inabidi kuweka moto kidogo kidogo ili kutunza joto.
 • Upatikanaji wa maji ni mgumu hasa kahawa inapoisha huko njiani hivyo hulazimika wakati mwingine hujazia kwa maji ya kwenye mitaro au yale yale ya kuoshea vikombe -Haizuru..
 • kwenda miguu na kurudi kwa miguu.
  Screenshot_20190220-195848.png
 

Sergei Lavrov

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
6,998
2,000
Bahati nzuri situmiagi kahawa za kutembezwa japo nawachangia hawa wauza kahawa kwa kuwanywesha kijiwe
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,969
2,000
Upatikanaji wa maji ni mgumu hasa kahawa inapoisha huko njiani hivyo hulazimika wakati mwingine hujazia kwa maji ya kwenye mitaro au yale yale ya kuoshea vikombe -Haizuru.
Sinywi tena upuuzi huu!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,550
2,000
Mh, kula uchafu, maji ya mitalo DSM kazi kubwa ni mavi toka septic tanks!
Kuna watu huzama chumvini kudeki!!!. sasa hayo maji ya mtaro yakichemshwa si bora zaidi!, yaani muuza kahawa akose pesa kisa hana maji? atatia chochote almradi kahawa ipatikane!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom