Baadhi ya wauza kahawa wakichoka kutembea huwa wanafanya mambo ya ajabu sana ilmradi wasitupoteze wateja wao!
Yale mabegi mgongoni yana kila kitu, yana beba mkaa, kiberiti, kashata, Katanga, kopo la kahawa,vikombe n.k
Hiyo ni mbinu za kuhakikisha kahawa inawafikia wateja masaa yote 24 na kuhakikisha moto hauzimiki kama ilivyo mbio za mwenge.
Kwasababu hakuna kazi isiyokosa kasoro, pia hii kazi ina pesa lakini shurti uzingatie masharti.
Zipo changamoto mbalimbali za kazi hii ingawa hii ina faida kubwa!

- Sharti la kwanza la kuuza kahawa ni marufuku kupanda daladala au Gari binafsi hata kama utapewa lifti.
- Sharti la pili usiwe na haraka na safari .
- Usipite kilinge bila kuwasalimia
- Usichangie mada mbalimbali za kwenye vilinge n.k
- Pitia site na rindo za wateja wako mda muafaka .
Zipo changamoto mbalimbali za kazi hii ingawa hii ina faida kubwa!
- Wakati wa jua Kali wateja hupungua,
- Mabirika ya kahawa ni mazito lakini yanazoeleka
- inabidi kuweka moto kidogo kidogo ili kutunza joto.
- Upatikanaji wa maji ni mgumu hasa kahawa inapoisha huko njiani hivyo hulazimika wakati mwingine hujazia kwa maji ya kwenye mitaro au yale yale ya kuoshea vikombe -Haizuru..
- kwenda miguu na kurudi kwa miguu.