Tanga: Mjamzito afariki dunia kituo cha afya kwa kukosa Tsh. 150,000

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

Pia soma > Watumishi 3 wasimamishwa kazi kwa kusababisha Kifo cha Mjamzito kisa hajatoa Tsh. 150,000
 
Mungu wangu, chozi limenitoka! Kufiwa kupo ila sio kwa kukosa namna ya kumsaidia mwanao, hasa kifedha!

Mungu ampe mama yake marehemu faraja.

Wahusika wachukuliwe hatua kali kwa haraka!

Hakuna sababu ya kutosheleza ya kusababisha kifo cha mama na mtoto kwa ukosefu wa fedha.
 
Mama mjamzito, Mariam Zahoro (30) Mkazi wa Kijiji cha Mumbwi Wilayani Handeni, Tanga amefariki dunia akiwa kwenye Kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilayani humo ikidaiwa kuwa alikosa huduma ya upasuaji baada ya kushindwa kulipa Tsh. 150,000 alizotakiwa kutoa kwa ajili ya huduma hiyo.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 11 kwenye Kituo hicho ambapo Mama mzazi wa marehemu, Hadija Athumani amesema Wahudumu hawakumfanyia Mwanae operesheni kwa kudai hela ya matibabu.

“Nilinyanyasika nikatukanwa kama mbwa alitakiwa kufanyiwa operesheni hawakuweza kumfanyia kwasababu hatukuwa na hela na Mimi ni fukara, Mwanangu aliniita akasema Mama njoo hapa nakufa sasa Mimi sina uwezo nikaka pale akawa anasema Mama nishike mkono, amama nishike kichwa, nililala chini sikuwa na cha kufanya akanipa mkono akaniambia Mama nakufa ndipo alipofariki”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Albert Msando amesema Serikali inalifanyia uchunguzi jambo hilo ili kubaini chanzo cha tukio.

Ujauzito sio Dharura, Huyo mjamzito alikua ana Miezi 9 ya kujiandaa kifedha.
 
Kwa hakika pesa imefanywa kipaumbele kwenye vituo vya huduma za kijamii.
Yaani badala ya kuwa na roho ya utu na ubinadamu watu wanatanguliza maslahi.
Kwa hakika wote waliohusika katika hili nafsi ya huyo mama itawatesa mpaka wanaondoka duniani.
 
Back
Top Bottom