Ripoti: Kifo cha Mjamzito Tanga ni uzembe wa Watoa Huduma na sio Tsh. 150,000

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro imesema kifo hicho kilitokana na uzembe wa Wataalamu wa Afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000.

Kifo cha Mariam Zahoro kilitokea November 11, 2023 katika Kituo cha Afya cha Kabuku Mkoani Tanga baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa kwa huduma ya dharura ya upasuaji.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kabuku Waziri Ummy amesema tayari Baraza la Madaktari pamoja na Wauguzi na Wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.

"Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa Watumishi wa Afya wazembe"

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dkt. Ali Said amesema chanzo cha kifo ni kutokana na uzembe wa Wataalamu hao kushindwa kuchukua hatua za haraka Ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari “Mwanamke huyo alichelewa kupatiwa huduma ya upasuaji kutokana na kukosekana kwa Mtaalamu wa dawa ya usingizi ambaye hakuwa anapatikana huku Daktari wa upasuaji akishindwa kutoa maamuzi ya rufaa kwa wakati kwenda kwenye Hospitali ya Wilaya"
 
Hawa wanatufanya sisi wajinga! Huyo mama angekuwa na pesa, ni dhahiri angefanyiwa upasuaji fastaaa!
 
"Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa Watumishi wa Afya wazembe"
Huu wimbo ni wa enzi na enzi ni zilipendwa,

Je mama wa marehemu aliyesema ameombwa rushwa ya 150K naye alidanganya? Kwanini hajachukuliwa hatua kama alidanganya?
 
Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro imesema kifo hicho kilitokana na uzembe wa Wataalamu wa Afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000.

Kifo cha Mariam Zahoro kilitokea November 11, 2023 katika Kituo cha Afya cha Kabuku Mkoani Tanga baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa kwa huduma ya dharura ya upasuaji.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kabuku Waziri Ummy amesema tayari Baraza la Madaktari pamoja na Wauguzi na Wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.

"Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa Watumishi wa Afya wazembe"

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dkt. Ali Said amesema chanzo cha kifo ni kutokana na uzembe wa Wataalamu hao kushindwa kuchukua hatua za haraka Ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari “Mwanamke huyo alichelewa kupatiwa huduma ya upasuaji kutokana na kukosekana kwa Mtaalamu wa dawa ya usingizi ambaye hakuwa anapatikana huku Daktari wa upasuaji akishindwa kutoa maamuzi ya rufaa kwa wakati kwenda kwenye Hospitali ya Wilaya"
CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE IMEISHA HIYOOO. CCM
 
Japo maisha siyo kutesa kila siku, ila pesa ndiyo kila kitu... Mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Je, ni hospitali gani ya Serikali ambayo inatoa huduma za afya nzuri na bora hapa nchini??
Msiwalaumu watu hawa kwani huo ndio utaratibu wa kawaida wa utendaji wao wa kazi wa kila siku.
 
Yaani kiufupi pesa ndyo iliyochelewesha. Hapo hakuna uzembe.
broh inawezekana isiwe pesa ila taasisi za serikali zina upungufu mkubwa wa wafanya kazi...

hilo ni tatizo kubwa sana nilishawahi kwenda zahanati moja hivi kwenye hiyo zahanati dokta ndio huyo huyo mkunga... ikitokea mjamzito anataka kujifungua dokta anaacha wagonjwa wengine anaenda kuzalisha😭😭😭😭​
 
Hili nalo ni tatizo. Serikali inashindwa vipi hata kuajiri watumishi wengine hata kwa mkataba maalum tu ili kukidhi mahitaji ya watanzania?
 
tunaongozwa na majambazi hawana uchungu...sisi tunatakiwa tujifie wajilie neema za Nchi 😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom