Kigoma: Ripoti ya CAG yawafikisha Watumishi 11 Mahakamani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118

Jumla ya Watu 11 wakiwemo Watumishi tisa wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na Maafisa wawili wa Wizara ya TAMISEMI wamefikishwa Mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma na kusomewa mashitaka 11 ikiwemo shitaka la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kiasi cha shilingi milioni 463.5, ikiwa ni matokeo ya Kamati ambayo iliundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Kigoma, Hassan Momba, Washitakiwa hao ambao hawakutakiwa kujibu chochote pia wamesomewa mashtaka ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kugushi nyaraka, kutakatisha fedha, kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. milioni 463.5 na matumizi mabaya ya madaraka.

Waliopandishwa kizimbani na kusomewama mashitaka ambao walikuwepo Mahakamani hapo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Athumani Msabila ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya Igunga ambaye ni Mshtakiwa wa kwanza.

Wengine ni Washtakiwa wanane Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambao ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Ferdinand Filimbi, Mweka Hazina wa Manispaa hiyo, Salum Saidi, Kombe Salum Kabichi, Frank Nguvumali, Jema Mbilinyi, Moses Zahuye, Joel shirima na Bayaga Ntamasambilo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma.

Washtakiwa wawili Watumi wa TAMISEMI waliofikishwa Mahakamani hapo ni Aidan Mponzi na Tumsifu ambao walisafirishwa kutoka Dodoma hadi Kigoma kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao wakielezwa ndiyo waliohusika kupelekwa kwa fedha hizo Kigoma.

Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2023 imeahirishwa hadi tarehe 20 mwezi huu kwa ajili ya kutajwa sambamba na kutoa uamuzi mdogo kwa Washtakiwa watano kama wanaweza kupata dhamana ambapo Washtakiwa wote wamarejeshwa rumande.

Itakumbukwa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Kigoma, Septemba 20-22, mwaka huu, Waziri Mkuu alipata taarifa ya uwepo wa fedha zilizoingizwa kwenye akaunti ya Amana ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kutoka TAMISEMI na kisha fedha hizo kuondolewa baada ya muda bila maelekezo maalum wala kujua zilitumikaje na akaunda Kamati ya uchunguzi.
 
Huyo DED bado yupo kwenye kiti huko alikohamishiwa? Au ni mtoto wa majina yale
 
Back
Top Bottom