Watu wenye umri mkubwa wanataokea Moshi, mikoa mingine hawatangazwi au hakuna?

Wachagga, wabarbagh, wamaasai na makabila yote yanayothamini nyama nyekundu huishi mda mrefu. Sisi wengine tumeshaathiriwa na blur blur blur za hawa madaktari uchwara. Mara nyama nyekundu Ina cholesterol Mara inaongeza uzito sana na theories za kusadikika... Nyie madaktari uchwara kama mna uwezo fanyeni research na mje na chanjo ya Coronavirus
 
Vile vitu ambavyo dini zenu zinawadanganya kuwa ni vibaya ndio wanavyotumia na kuishi miaka mingi yenye mafanikio makubwa

1. Unjwaji wa pombe

2. Unywaji wa damu za wanyama

3. Ulaji wa nyama bora zaidi kuliko zote duniani nyama ya NGURUWE

4.Kufanya kazi masaa yote ni zaidi ya mazoezi ya wale wa DAR wanaokimbia na headphone au kwenye mashine gym badala ya kutumia nguvu hizo kwenye uzalishaji

5.SALA huo ndio msingi mkubwa sana
 
Wanakufa kwa sababu ya ulaji wa kitimoto na mapombe..watu wa huko wanasifa hiyo kubwa hivyo magojwa kama kisukari..hypertension ni kawiada kwao..hivyo korona ikiingia ni dakk zero wamekwenda na maji.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeelewa alichokiandika mleta mada Au umekimbilia ku justify uzezeta wako?!
 
Wanakufa kwa sababu ya ulaji wa kitimoto na mapombe..watu wa huko wanasifa hiyo kubwa hivyo magojwa kama kisukari..hypertension ni kawiada kwao..hivyo korona ikiingia ni dakk zero wamekwenda na maji.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona umelipukia mada kama Bomu la Hiroshima na Nagasaki. Rudi kasome post ya mleta mada uielewe.

Kwa taarifa Bibi wa mke wangu alifikisha miaka 120 ulijumlisha miaka 109 ya toka kubatizwa ilikutwa kwenye cheti za kubatizwa kanisani. Alibatizwa na umri mkubwa miaka 11. Alizeeka mpaka akawa mdogo kama mtoto unambeba sema mifupa mizito. Hakuwahi kuugua na alikufa tu kawaida mnashtuka tu ameshakufa mwenyewe peaceful. Ila toka mke wangu akikua Bibi yake vyakula vyake vilikuwa kama ifuatavyo:
1. Kuchemsha
2. Vyakula vya kupika Kwa magadi _Wachagga mnavijua vyote
3. Chumvi kidogo Sana
4. Mafuta kidogo au bila Mafuta
5. Sukari hakuna kabisa
6. Nyama nyekundu kwa nadra Sana. Naambiwa hapa hata samaki hakuwa anakula. Kifupi protein zake zilikuwa za mmea zaidi kuliko wanyama.
Katika yote alikuwa anasali Sana na hakuwa na kinyongo na mtu.

Hivyo basi mtindo wa maisha yetu ndiyo utaamua mambo mengi ya maisha yetu.
 
Back
Top Bottom