Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 2,915
- 4,791
Habari za mchana wana JF.
Hali ya sintofahamu imeendelea kwa siku mbili sasa katika kijiji cha Handa kilichopo katika Wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma karibu na mpaka na Wilaya ya Ikungi ambayo ipo katika Mkoa wa Singida. Ni karibu pia na Mpaka na Wilaya ya Hanang katika mkoa wa Manyara.
Hali hiyo imesababishwa na watu wanaojitambulisha kama Askari wa Jeshi la Polisi na wengine wakijitambulisha kama Askari wa Misitu. Watu hao wamefika katika kijiji hicho siku ya tarehe 6/11/2023 na kuanza kuchoma moto makazi ya wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za kilimo na ufugaji katika kijiji hicho.
Madai yao ni kwamba eti eneo walililopo halipo katika Wilaya ya Chemba bali lipo katika Wilaya ya Ikungi. Wananchi hao walipata ardhi hiyo baada ya kugawiwa na halmashauri ya kijiji.
Huu ni uonevu wa hali ya juu kwa wananchi ambao ni raia wa Tanzania wanaojishughulisha kiuchumi. Eneo kutokuwa katika Wilaya ya Chemba inawaohusu nini wananchi? Au Mkoa wa Singida ni Jamhuri inayojitegemea? Huo mkoa na Wilaya ina uraia wake tofauti na huu wa Tanzania? Na kama kuna mgogoro kati ya vijiji, kwanini usitatuliwe kwa misingi na sheria?
Kwanini wananchi wachomewe mali zao zikiwepo mazao yaliyohifadhiwa, makazi yao ya kujihifadhi, mavazi na malazi?
RPC mkoa wa Singida, OCD Ikungi, RPC Dodoma, OCD Chemba, RC Mkoa wa Singinda, RC Mkoa wa Dodoma, DC Wilaya ya Ikungi, DC Wilaya ya Chemba wanahitajika kwenda kuwaokoa hao wananchi kwa misingi ya sheria na kuwawajibisha wote waliojichukulia sheria mkononi kwa kuwachukulia hatua kali.
Wananchi wapewe fidia ya upotevu wa mali zao na kutibiwa kwa waliomizwa kwa vipigo kwa watenda jinai hao. Kama kuna mgogoro wa mipaka ya wilaya au vijiji utatuliwe haraka kwa misngi ya sheria.
Mtanzania ana haki ya kwenda popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupata hifadhi, kufanya kazi ya kujipatia kipato bila kuvunja sheria.
Uchunguzi pia ufanyike ili kujua kama kuna anayelitumia jeshi la polisi wilaya ya Ikungi kwa manufaa yake binafsi.
Haki itendeke kwa walioumizwa. Hadi leo watu hao wanaendelea kuteketeza makazi, malazi, mavazi, chakula na mifugo kwa moto kwa madai kwamba wamelivamia eneo hilo.
Kwanini wanajichukulia sheria mkononi? kwanini wananchi wanyonge, wakulima wadogo na wafugaji wanyanyaswe na watu wanaojiita jeshi la polisi?
Usalama wa Raia uko wapi kama watu walioaminiwa ndio wanaovunja sheria?
Naomba pia wabunge Mohammed Mmuni wa Chemba, Ramadhani Ighondu wa Singida Kaskazini, Miraji Mtaturu wa Ikungi Mashariki na Mbunge wa Hanang' Mhandisi Samwel Hhayuma wawasaidie wananchi hao wanyonge ili waweze kutendewa haki.
Majibu ya Serikali, soma hapa - Mamlaka ya Misitu (TFS) yatoa ufafanuzi kuhusu zoezi la kuwahamisha Waliovamia Msitu wa Mgori