Mamlaka ya Misitu (TFS) yatoa ufafanuzi kuhusu zoezi la kuwahamisha Waliovamia Msitu wa Mgori

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
DSC_0045.JPG

Baada ya memba wa JamiiForums.com kulalamikia mchakato wa kuwaondoa Wananchi walio ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Mgori mamlaka zimejibu na kutoa ufafanuzi, soma hapa hoja ya Mdau - Watu wanaodhaniwa Askari wa Polisi na Maafisa Msitu wawapiga Wananchi, kuchoma moto makazi na mazao Wilaya ya Chemba na Ikungi

Maelezo ya TFS
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Kanda ya Kati, Mathew Kiondo anafafanua: "Kinachofanyika ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa wavamizi waliopo katika Msitu wa Mgori.

“Rais alipokuwa akiwasili Singida katika ziara akasema wakati akiwa anawasili aliona msitu mzuri lakini unaharibiwa, kwa tamko hilo maana yake ni maelekezo ya Mkoa na Wilaya.

"Kamati ya Ulinzi na Usalama ikatoa tangazo watu wahame katika Hifadhi ya Msitu wa Mgori, siku ya kwenda kupeleka tangazo hilo Wananchi waliovamia msitu huo wakawashambulia watu wa usalama akiwemo Mkuu wa Wilaya kwa kutumia mishale, mawe, rungu na nyinginezo.

"Baada ya kujipanga tukarejea na kwenda kufanya zoezi la kuwaondoa wavamizi hao, hatukutumia nguvu, kwa kuwa wao waliona tumeongozana na Watu wa Usalama, Askari wa FFU, Mgambo hawakufanya fujo, zoezi ni endelevu na litafanyika kwa siku 14.

“Tulichofanya tuliharibu makazi yao ya muda ambayo yapo ndani ya Msitu, wanafanya hivyo kujenga makazi ya muda kwa kuwa wanajua sio sehemu sahihi kwao.

“Kilichoharibiwa ni makazi yao lakini mazao, chakula na mifugo vyote havijachukuliwa wamekabidhiwa na kutakiwa kurejea kwenye vijiji ambavyo vipo kando ya Misitu.

"Lazima tuwe na ubinaadamu, kisheria ilitakiwa hata mifugo yote tuitafishe lakini tuliwaachia waondoke nayo.

“Pamoja na hivyo zipo taarifa zisizo rasmi kuwa baadhi ya mifugo ambayo inaingizwa ndani ya Hifadhi ni ya watu wenye nafasi katika siasa, hivyo hawa Wananchi wanatumika tu.”
 
Hawa jamaa wa misitu huwa wanatumia nguvu nyingi na ukatili kuliko hata FFU, imeshazoeleka. Ila ifike muda watz tutumie akili na si nguvu tena, mwakani siyo mbali.

Ifike muda tuchoke kunyanyasika, tuwe na lengo moja, haiwezekani kila siku mwanasiasa atuzidi nguvu.
 
Sema na wananchi walizingua kuwashambulia maafisa misitu in first place ndo mana wametumia ubabe round ya pili,
Wangetumia akili mwanzoni pengine isingefika huko
 
View attachment 2807601

Habari yako ni ya upande mmoja. Wale wananchi wamehojiwa? Msitu wa Mgori ni msitu uliohifadhiwa? Kwa GN namba ngapi?
Misitu ipo mingi na sio kila msitu umehifadhiwa.
Vipi madai kwamba wale wananchi wengi wao wamegawiwa ardhi na halmashauri ya kijiji ambayo kwa mujibu wa sheria ndio wenye ardhi.
 
Mpaka wanajenga serikali ilikuwa wapi?
 
Hawa jamaa wa misitu huwa wanatumia nguvu nyingi na ukatili kuliko hata FFU, imeshazoeleka. Ila ifike muda watz tutumie akili na si nguvu tena, mwakani siyo mbali.

Ifike muda tuchoke kunyanyasika, tuwe na lengo moja, haiwezekani kila siku mwanasiasa atuzidi nguvu.
Wananchi wote hawawezi kushiriki jinai. Waliohusika wangekamatwa na kuchukuliwa hatua. Kosa la watu wachache haliwezi kuchukuliwa kama la kijiji kizima.
 
Na wanadiriki kusema makazi ya muda mfupi. Wanajitoa ufahamu tu. Wale wananchi hawawezi kujenga nyumba nzuri za matofali ya block au kuchoma. Wanaishi katika mbavu za mbwa, kuezeka kwa bati au nyasi. Hadi makanisa ya kuabudia waliojenga yalichomwa moto.
 
Sema na wananchi walizingua kuwashambulia maafisa misitu in first place ndo mana wametumia ubabe round ya pili,
Wangetumia akili mwanzoni pengine isingefika huko
Ni kinyume na sheria ndiyo, lakini nadhani majibu ya hawa askari ni kiashirio tosha ni aina gani ya tabia na way of execution hawa askari huitumia kwa wananchi hawa askari wapo tayari na wana uwezo kiasi gani kufika/kuwafanyia wananchi
 
Sema na wananchi walizingua kuwashambulia maafisa misitu in first place ndo mana wametumia ubabe round ya pili,
Wangetumia akili mwanzoni pengine isingefika huko
Askari ni wa kwanza kutii sheria na ndiye mtetezi wa sheria.
 
Back
Top Bottom