Watozwa 35,000 faini ya kula mabaki ya chakula cha mbunge-Singida

Wananchi 15 wanaoishi Kitongoji cha Kahomwele,Kijiji cha Doroto,Tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Mkoa wa Singuda, wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 35,000/= kila mmoja kwa madai kuwa walikula chakula kilichobaki ambacho kiliandaliwa kwa ajili mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi (CCM) Bwana John Paul Lwanji. Baada ya Mbunge kula na kuondoka wananchi wakachukua chakula kilichobaki Mezani wakala, Chakula hicho kiliandaliwa kwa michango ya wananchi wenyewe kwa ajili ya ziara ya Mbunge. Ila wamegeukwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji kuwa wamesababisha uvunjifu wa Amani na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha. Kwa mantiki hizo zitachangwa 525,000. Watetezi wa haki za binadamu saidieni hilo huko Singida..
Mkuu mtu aliyeko karibu nao awashauri hiyo kesi waipeleke mahakamani, huyo mtendaji na mwenyekiti washitakiwe kwa unyanyasaji na usumbufu walipe na damages!!

Ningelikuwa na EMAIL ya Tundu Lissu basi ningelimuambia kwenda kuwaambia wananchi wasilipe na atakayewashitaki basi watapambana naye Mahakamani.

Ikibidi basi viongozi wa Juu wa Chadema waanze kumuandaa mtu kwenda kulichukua hili jimbo maana wapuuzi nchi hii ni wengi na ili kuwadhibiti, inabidi tuanzie kwenye mashina.
 
Aisee,,hata makombo pia wanalipishwa??sasa wanalipishia kwa uhalali upi??

Na kwanini wakawasubiri wale kwanza then wawape hoja hizo??hao wanachi wakilipa watakua mazuzu tuh,wao washakula washashiba washike zao majembe wakalime,,hao wanaojifanya wameumia sana wakashitaki,,makombo na manawi nayo yana gharama??

Ebo...!!
 
Hahaha vitu vingine hadi vichekesho, halaf 15,000 per person ni nyingi sana jamani, kwa sahani moja dah huo ni uonevu na wakilipa hiyo hela inaenda mifukoni mwa watu tu!
Ni thirty five thousand (Tshs 35,000/=) mkuu, mradi huo wa katibu kata na mwenyekiti huo.

kwanza nani kasema walipe? maana mahakama peke yake ndio ina mamlaka ya kufanya hayo.
m/kiti wa kijiji na afisa mtendaji wanatoa hukumu wao kama nani?
 
Wananchi 15 wanaoishi Kitongoji cha Kahomwele,Kijiji cha Doroto,Tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Mkoa wa Singuda, wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 35,000/= kila mmoja kwa madai kuwa walikula chakula kilichobaki ambacho kiliandaliwa kwa ajili mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi (CCM) Bwana John Paul Lwanji. Baada ya Mbunge kula na kuondoka wananchi wakachukua chakula kilichobaki Mezani wakala, Chakula hicho kiliandaliwa kwa michango ya wananchi wenyewe kwa ajili ya ziara ya Mbunge. Ila wamegeukwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji kuwa wamesababisha uvunjifu wa Amani na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha. Kwa mantiki hizo zitachangwa 525,000. Watetezi wa haki za binadamu saidieni hilo huko Singida..

we isango ni muongo tunakujua sana.topic zako nyingi ulizowahi kuweka hapa hazina ukweli.hii habari imekaa kizabina zabina mno
 
vijijini inatumika katiba nyingine ya nchi, watu wanaonewa sana na serikali ya vijiji, yani wenyeviti kwenye serikali za vijijini ndiyo kama marais, wana kila aina ya madaraka na ole wako usilipe.
 
kwani hicho chakula kilikuwa cha nini? Wamekipeleka mahali pake-dhambi kama wangemwaga!! waache mambo ya aibu haya!!
 
Hahaha vitu vingine hadi vichekesho, halaf 15,000 per person ni nyingi sana jamani, kwa sahani moja dah huo ni uonevu na wakilipa hiyo hela inaenda mifukoni mwa watu tu!

Hujaelewa vizuri, ni wananchi 15, wanalipishwa 35,000 kila mmoja. Chakula walichangishwa wao ili Mbunge aje kula, amekuja kijijini amekula kidogo akabakiza, alipoondoka wananchi wakaona nao ni fursa ya kumalizia kilichobaki, ndo wakakumbwa na tuhuma ya kuvunja amani na kutakiwa kulipa 35,000/
 
Wananchi 15 wanaoishi Kitongoji cha Kahomwele,Kijiji cha Doroto,Tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Mkoa wa Singuda, wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 35,000/= kila mmoja kwa madai kuwa walikula chakula kilichobaki ambacho kiliandaliwa kwa ajili mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi (CCM) Bwana John Paul Lwanji. Baada ya Mbunge kula na kuondoka wananchi wakachukua chakula kilichobaki Mezani wakala, Chakula hicho kiliandaliwa kwa michango ya wananchi wenyewe kwa ajili ya ziara ya Mbunge. Ila wamegeukwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji kuwa wamesababisha uvunjifu wa Amani na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha. Kwa mantiki hizo zitachangwa 525,000. Watetezi wa haki za binadamu saidieni hilo huko Singida..
hahahaahahaa hili nalo neno. Sasa si wangemwambia mmoja wao hapo angemlipia huyo mheshimiwa akala tu hotelini. Huo msosi ulikuwa wa gharama kubwa kiasi hicho. Halafu nimechungulia kwa Mhasibu pale halmashauri kuna mtu alipewa hela za kugharamikia safari ya Mbunge, iweje tena watu wakachanga? na hizo za halmashauri zinakwenda wapi?
 
Je kuna mwongozo juu ya kitendo kama hicho? M/Kiti na VEO walitaka kuuza hayo makombo, hivyo wakaamua kuwachaji waliokila. Raia wana njaa, kila siku wanakula ugali maharage; wananchangia Mbunge mwenye mshahara mnono; Mbunge anakula na kusaza; raia masikini wakila makombo wanalipishwa. Mhhh... Mungu wangu, msaada wetu utatoka wapi? Je umungu mtu utaisha lini? Muda si mrefu wale watu wanaookota/kula majalalani watalipishwa.
 
Heri yao wenye kumtegemea mungu maana atawaongoza kwenye mema.
 
Back
Top Bottom