Watozwa 35,000 faini ya kula mabaki ya chakula cha mbunge-Singida

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
195
Wananchi 15 wanaoishi Kitongoji cha Kahomwele,Kijiji cha Doroto,Tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Mkoa wa Singuda, wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 35,000/= kila mmoja kwa madai kuwa walikula chakula kilichobaki ambacho kiliandaliwa kwa ajili mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi (CCM) Bwana John Paul Lwanji. Baada ya Mbunge kula na kuondoka wananchi wakachukua chakula kilichobaki Mezani wakala, Chakula hicho kiliandaliwa kwa michango ya wananchi wenyewe kwa ajili ya ziara ya Mbunge. Ila wamegeukwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji kuwa wamesababisha uvunjifu wa Amani na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha. Kwa mantiki hizo zitachangwa 525,000. Watetezi wa haki za binadamu saidieni hilo huko Singida..
 
MTENGETI

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,510
2,000
Jesus! hivi yametokea Tanzania hii inayosifiwa kwa utawala bora? wamelipa hizo faini? natarudi hivi punde.
 
Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,947
2,000
Halafu anasimama mtu anadai "Tanzania ni Kisiwa Cha Amani"... wanadhani amani ni kutokuwa na vita tu...!!
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,927
2,000
hao wananchi na wenyewe watu wa ajabu sana,watamchangiaje mbunge ale mapochopocho wakati wenyewe njaa zinawauma.??
 
Makene

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,476
1,195
kwani huyo mbunge alikula chakula cha shs ngapi mpaka kibaki chakula chote hicho.
Si bora wangemlipia hotelini tu. Nafikiri tu.
 
Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,960
2,000
Uzuri wamekula jasho lao wenyewe walilo changa au afisa wa kijiji alitaka afaidi mwenyewe mapaja?
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,069
1,750
ha!!!!!!!!!!! mh kama mimi nisingelipa hata iweje ebo
kwa hiyo walitaka kikatupwe?
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,069
1,750
lakini kikwete mwenyewe alishawahi kusema ukitaka kula sharti ukubali kuliwa labda ndio kanuni kwa wana ccm kwa vile ni wenyewe kwa wenyewe pengine walioambiwa kulipa watafanya hivyo. ya nyumbani kwa jirani tusiyaingilie.
 
snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,363
2,000
wangewatapisha palepale,,,faini hadi kwenye kula leftovers?khaa!!!
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Wananchi 15 wanaoishi Kitongoji cha Kahomwele,Kijiji cha Doroto,Tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni, Mkoa wa Singuda, wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 35,000/= kila mmoja kwa madai kuwa walikula chakula kilichobaki ambacho kiliandaliwa kwa ajili mbunge wa jimbo la Manyoni magharibi (CCM) Bwana John Paul Lwanji. Baada ya Mbunge kula na kuondoka wananchi wakachukua chakula kilichobaki Mezani wakala, Chakula hicho kiliandaliwa kwa michango ya wananchi wenyewe kwa ajili ya ziara ya Mbunge. Ila wamegeukwa na Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji kuwa wamesababisha uvunjifu wa Amani na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha. Kwa mantiki hizo zitachangwa 525,000. Watetezi wa haki za binadamu saidieni hilo huko Singida..

mmmmh......ebwana
 
Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,069
1,750
Halafu anasimama mtu anadai "Tanzania ni Kisiwa Cha Amani"... wanadhani amani ni kutokuwa na vita tu...!!

ni kweli kiongozi,
yani watanzania tunapumbazwa sana na hii kauli, na nasema tanzania hii wanayoiona ina amani ni kwa sababu watu wake wengi wamelishwa unga wa ndwele wakila unga wa rutuba hii amani wanayodai ipo na namna mambo yanavyoenda hawataisikia tena.
 
Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,611
2,000
hiyo pesa inayochangwa ni mradi wa mtu, suala la kula chakula cha hisani ni kisingizio tu
 
Dec 11, 2010
3,321
0
Hao watakuwa wamekula chakula chao walicho muandalia mbunge akakibakisha, dhambi kuu ni kuwachanganisha watu wamlishe mbunge wakati mbunge husika ana kipato kikubwa kuliko wao.
 
babe S

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
3,881
2,000
Hahaha vitu vingine hadi vichekesho, halaf 15,000 per person ni nyingi sana jamani, kwa sahani moja dah huo ni uonevu na wakilipa hiyo hela inaenda mifukoni mwa watu tu!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom