Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MBUNGE CONDESTER Atembelea Eneo Lenye Madini ya Sodalite Kukagua Utafiti Unaoendelea Kijiji cha Chindi
Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe (Mundy) ameambatana na Afisa Madini mkazi Mkoa wa Songwe, Chone Malembo, ametumia mtubwi kuvuka mto Nkana kuelekea Kijiji cha Chindi kwenda kujionea utafiti wa madini aina ya Sodalite yanayodaiwa kugundulika eneo hilo
Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) amempongeza mchimbaji mdogo wa madini ya Sodalite bwana Nickolaus Buseni kwa kuamua kufanya utafiti wa madini hayo ndani ya Jimbo lake na kueleza kuwa yupo tayari kumuunga mkono, ikiwa ni pamoja na kumkutanisha na taasisi za kifedha ili apatiwe Mkopo
Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) amewasihi wananchi wa kijiji cha Ntinga na wana Momba kwa ujumla kuchangamkia fursa ya kupata leseni kwa ajili ya uwekezaji wa madini ya Sodalite ambayo yanadaiwa kugundulika kijiji cha Chindi Kata ya Msangano.
Afisa Madini Mkazi mkoa wa Songwe, Chone Malembo, amesema madini ya Sodalite, ambayo yanafanyiwa utafiti kijiji cha Chindi Kata ya Msangano Wilaya ya Momba, yatakuwa ni madini mapya kupatikana ndani ya Mkoa huo, kwani hakuna eneo lingine ambayo yanapatikana ndani ya Mkoa wa Songwe