Kijiji cha Kinampanda (Singida) hakina umeme wiki ya pili sasa

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Singida Kijiji cha Kinampanda kuna shida ya umeme inaenda wiki ya pili sasa hii ni baada ya mvua kunyesha na kukatokea radi iliyosababisha transformer kuharibika.

Walienda wakaifungua na kuondoka nayo mpaka sasa haijulikani ni lini wanarudisha huduma ya umeme kwani hata mtaa wa pili umeme ulipi ni wakuwasha taa tu hauwezi kuwasha hata mashine za kusagia unga.

Je, wale wananchi hawana haki ya kurudishiwa umeme kwa wakati?

Au hakuna transformer za akiba?

Au ndo basi hawatafunga tena nyingine?

Kama watafunga kuna ulazima gani wa kujivutavuta?

Ni hayo tu.

Sent from my TECNO CA8 using JamiiForums mobile app
 
Jaribuni kuwasumbua, yaani eneo husika mji-organize mumlalamikie Mbunge na Diwani+Kupiga simu bila kuchoka ikiwezekana mchange hela waathirika wote muwatumie Otherwise Mtalia kwa kusaga meno. Niliweka biashara ya machine kijiji flani siku moja Arrestor 1, ya Transformer ikaungua Tulikaa wiki mbili ndo wakaja baada ya kuwalamba makalio sana. Wanafika wakasema Next time tujiongeze ikitokea shida kama hiyo.
 
Back
Top Bottom