ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Wandugu nawasalimu kwa jina la JF!
Jamani wanajf naomba tumsaidie rafiki yangu. Huyu rafiki yangu ana watoto wake wawili wanaopishana mwaka tu kati yao, mmoja ana miaka mitatu na miezi 11 na mwingine ana miaka miwili na miezi nane.
Jamaa analalamika sana kwamba watoto wake hao wawili, mkubwa wa kike na mdogo wa kiume wanatabia moja inayomsumbua sana. Kwamba hao watoto pindi wanapokuwa pamoja nyumbani muda mwingi wanapigana na kunyang'anyana vitu vya nyumbani. Imefika wakati jamaa huwa anachelewa kurudi nyumbani walau kupitisha muda ili akifika ikibidi akute muda umeenda na wanakaribia kulala. Kuna wakati aliamua kuwakamatia bakora lakini alishindwa kwani 'mtanange wa ngumi' haukupungua. Hata hivyo binafsi nilimwambia asiwachape chape hovyo inaweza ikawaletea mazoea/usugu wa bakora. Cha ajabu wote wawili hawagombani na kaka yao ambaye ana umri wa miaka 5.
Aliponiuliza sababu inaweza kuwa nini, binafsi sikuwa na la kumjibu ila nilimwambia ntajaribu kuulizia watu pengine wanaweza kutoa majibu ya kueleweka.
Wandugu nalileta kwenu hili jambo ili tuweze kumsaidia mwenzetu na wengine ambao bado watoto wetu 'tunatemebea nao' tupate ufahamu ili tutakapoyakuta huko mbeleni tusione kuwa ni jambo jipya!
Karibuni!