Watoto Wananisumbua: Wanagombana Sana

awanunulie vitu vingi vya kuchezea, inawezekana hao watoto hawana vitu vya kuchezea kama madoli etc. Lakini hiyo ni kawaida sana. Na anawaharibu zaidi anavyojifanya eti kuchelewa home ili akute wamelala, he is creating a gap ambayo atakuja kujilaumu baadaye. anachopaswa kufanya awahi home kucheza nao, wataacha tu.

Hata hivyo duuuuu watoto wanazidiana mwaka?...yaani mama kajifungua baada ya mwezi jamaa akatia mimba???!!!!

Masihara hayo, utingo, yasije yakakukuta yaliyonikuta, mweee!
 
Jamani wanajf naomba tumsaidie rafiki yangu. Huyu rafiki yangu ana watoto wake wawili wanaopishana mwaka tu kati yao, mmoja ana miaka mitatu na miezi 11 na mwingine ana miaka miwili na miezi nane..

Mkuu hao watoto bado wadogo..muombe rafiki yetu aache kutembeza bakora kwani sio vizuri. Pili muombe asitafute kizingizio cha kutorudi nyumbani mapema kukimbia kelele za watoto...Nina timu zaidi kidogo ya hiyo ambayo ilinipa kazi ya kutunga sheria ya kuangalia katuni yaani kila mtu ana muda wake...baada ya kuchoka kuwa referee wa ngumi kila siku..

Kuhusu kupigana kwa hao watoto nadhani ni dalili nzuri kuwa hao watoto kichwani wako active sana..hivyo hawawezi kutulia..ni ushindani wa kiakili zaidi kuliko Physical...Huko kupigana ni impact ya mambo yanayoendelea kichwani. Kikubwa ndugu yetu atafute interest za hao watoto..kumbuka watoto wanapishana interest..afanye "try and error" ..mpaka ajue interest zao ambazo zitafanya akili iwe busy na kuacha kufikiri kugombana..
 
Watenge kwa kuwaweka kwenye kona.watoto hawapendi kutengwa.kila mmoja muweke kwenye kona yake.watapunguza
 
Pia jaribu kuangalia selection ya games na toys unazowanunulia ziwe zenye michezo shiikishi; kila mmoja awe anamuhitaji menzake ili kufurahia mchezo!
 
Wandugu nawasalimu kwa jina la JF!

Jamani wanajf naomba tumsaidie rafiki yangu. Huyu rafiki yangu ana watoto wake wawili wanaopishana mwaka tu kati yao, mmoja ana miaka mitatu na miezi 11 na mwingine ana miaka miwili na miezi nane.

Jamaa analalamika sana kwamba watoto wake hao wawili, mkubwa wa kike na mdogo wa kiume wanatabia moja inayomsumbua sana. Kwamba hao watoto pindi wanapokuwa pamoja nyumbani muda mwingi wanapigana na kunyang'anyana vitu vya nyumbani. Imefika wakati jamaa huwa anachelewa kurudi nyumbani walau kupitisha muda ili akifika ikibidi akute muda umeenda na wanakaribia kulala. Kuna wakati aliamua kuwakamatia bakora lakini alishindwa kwani 'mtanange wa ngumi' haukupungua. Hata hivyo binafsi nilimwambia asiwachape chape hovyo inaweza ikawaletea mazoea/usugu wa bakora. Cha ajabu wote wawili hawagombani na kaka yao ambaye ana umri wa miaka 5.

Aliponiuliza sababu inaweza kuwa nini, binafsi sikuwa na la kumjibu ila nilimwambia ntajaribu kuulizia watu pengine wanaweza kutoa majibu ya kueleweka.

Wandugu nalileta kwenu hili jambo ili tuweze kumsaidia mwenzetu na wengine ambao bado watoto wetu 'tunatemebea nao' tupate ufahamu ili tutakapoyakuta huko mbeleni tusione kuwa ni jambo jipya!

Karibuni!

ni kawaida, mtu akiwa na mtoto mmoja anakuwa mzazi, wakiwa watoto wawili anakuwa refarii
 
Back
Top Bottom