Watoto Wananisumbua: Wanagombana Sana

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Wandugu nawasalimu kwa jina la JF!

Jamani wanajf naomba tumsaidie rafiki yangu. Huyu rafiki yangu ana watoto wake wawili wanaopishana mwaka tu kati yao, mmoja ana miaka mitatu na miezi 11 na mwingine ana miaka miwili na miezi nane.

Jamaa analalamika sana kwamba watoto wake hao wawili, mkubwa wa kike na mdogo wa kiume wanatabia moja inayomsumbua sana. Kwamba hao watoto pindi wanapokuwa pamoja nyumbani muda mwingi wanapigana na kunyang'anyana vitu vya nyumbani. Imefika wakati jamaa huwa anachelewa kurudi nyumbani walau kupitisha muda ili akifika ikibidi akute muda umeenda na wanakaribia kulala. Kuna wakati aliamua kuwakamatia bakora lakini alishindwa kwani 'mtanange wa ngumi' haukupungua. Hata hivyo binafsi nilimwambia asiwachape chape hovyo inaweza ikawaletea mazoea/usugu wa bakora. Cha ajabu wote wawili hawagombani na kaka yao ambaye ana umri wa miaka 5.

Aliponiuliza sababu inaweza kuwa nini, binafsi sikuwa na la kumjibu ila nilimwambia ntajaribu kuulizia watu pengine wanaweza kutoa majibu ya kueleweka.

Wandugu nalileta kwenu hili jambo ili tuweze kumsaidia mwenzetu na wengine ambao bado watoto wetu 'tunatemebea nao' tupate ufahamu ili tutakapoyakuta huko mbeleni tusione kuwa ni jambo jipya!

Karibuni!
 
22nd

JF-Expert Member
Aug 1, 2010
497
135
nimepigana sana na kaka yangu,mpaka age ya early 20's bado tulikuwa tunapigana,nina makovu kama mawili mwilini asiyofutika yanatokana na kupigana na yeye.halafu yeye alikuwa anamwili mkubwa,baunsa,ila bado nilikuwa namkunjia ngumi, nadundwaaaaa, naliaaaaaaaaaaaaaaa,na kesho tena. But I love him very much, he is very cool guy asiyependa ugomvi na makuu.

Ukiniuliza sababu ya kupigana siwezi kukujibu coz hata now najiuliza the same, kwanini tulikuwa tunapigana haliyakuwa yeye ni mpole.
tumepishana miaka 2.
 
WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,459
943
Ni hali ya kawaida kwa watoto wanaofuatana kwa karibu na hasa wakiwa "wachanga" hivyo na husababishwa na ushindani miongoni mwa watoto katika kupata attention ya wazazi.Wamezaliwa karibukaribu sana.
Ajitahidi kuwaelimisha ili watambue ni ndugu na wanahitaji kupendana.Wazazi nao wajaribu kuamulia ugomvi kwa hekima ili kuonyesha hali lakini hapohapo kuonyesha kumlinda anayeonewa bila kuchochea ushindani zaidi.
 
Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,292
765
Hii kisayansi sijui itaelezwaje, lakn kiasili ss watu wakitambo kidogo tunasema ni watoto kunyang'anyana ziwa kwa ukaribu mno; mwaka mmoja ni karibu sana, ina maana mimba ilitungwa wakaati mmoja bado ananyonya! Nakumbuka hata mimi na mdogo wangu tulipishana kidogo namna hiyo hvo tulikuwa tukigombana mara kwa mara, jambo ambalo limetuathiri mpaka ukubwani mara nyingi hoja zetu zinapingana (Japo tunapendana sana). Anachotakiwa kufanya ni kuawaonesha mapenzi sawa, bila kumpendelea mdogo wala mkubwa kwa namna yoyote ile. Kuwaepuka ni kukwepa majukumu, anatakiwa awe nao karibu zaidi na kuwa na furaha katika familia kutawafanya watoto wapendane na kujaliana!
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,181
14,319
nimepigana sana na kaka yangu,mpaka age ya early 20's bado tulikuwa tunapigana,nina makovu kama mawili mwilini asiyofutika yanatokana na kupigana na yeye.halafu yeye alikuwa anamwili mkubwa,baunsa,ila bado nilikuwa namkunjia ngumi, nadundwaaaaa, naliaaaaaaaaaaaaaaa,na kesho tena. But I love him very much, he is very cool guy asiyependa ugomvi na makuu.

Ukiniuliza sababu ya kupigana siwezi kukujibu coz hata now najiuliza the same, kwanini tulikuwa tunapigana haliyakuwa yeye ni mpole.
tumepishana miaka 2.

It was the same to me
Mpaka bro anaondoka nyumbani nilishangilia maana niliona kero imepungua
Japo sasa majukumu yote yalibaki kwangu sasa baada ya yeye kwenda boarding school
Mpaka leo ukiniuliza ni lipi tulilokuwa tunagombana na kupigana sijui
Ila ni hali ya kawaida ipo sana
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
8,240
3,589
Sawa mkuu lakini sasa nini cha kufanya ili kupunguza hiyo hali hiyo?
awanunulie vitu vingi vya kuchezea, inawezekana hao watoto hawana vitu vya kuchezea kama madoli etc. Lakini hiyo ni kawaida sana. Na anawaharibu zaidi anavyojifanya eti kuchelewa home ili akute wamelala, he is creating a gap ambayo atakuja kujilaumu baadaye. anachopaswa kufanya awahi home kucheza nao, wataacha tu.

Hata hivyo duuuuu watoto wanazidiana mwaka?...yaani mama kajifungua baada ya mwezi jamaa akatia mimba???!!!!
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,747
7,756
....dahhh, napenda topiks kama hizi ambazo zinatutoa nje kidogo ya mazowea ya kila siku kushauriana mambo ya ndoa.
hebu ngoja nijaribu kuwatumia pm baadhi ya wanachama ambao najua wanaweza tusaidia malezi ya namna hii...pole sana bana...

nitarudi na ushauri...
 
Nsiande

JF-Expert Member
Jul 27, 2009
1,649
856
Hata wangu wanapigana sana mpaka ikabidi nimwombe dada wakitoka shule awatenganishe immediately wakianza kupigana

maana wakipigana mmoja atalia mpaka nirudi namkuta sauti imekauka, so siku wakiwa hawana ugomvi wanacheza kwa furaha siku ya ugomvi mmoja anakaa chumbani kwangu kuepusha shari la kilio cha kukausha koo

Nimeshaongea mpaka nimechoka kuhusu kupigana maana wanapishana miaka 3 na mmoja anamg'ata mwenzake na kumwachia makovu , so soln wakiwa kwenye ugomvi mood wanatenganishwa nikirudi simind kumkuta mmoja chumbani anaangalia cartoon au kalala, si unajua watoto wanapenda kukaa chumbani kwa baba na mama? So asiye mgomvi ndio anakaa huko

Kama kuna njia nyingine nisaidieni lkn hiyo ndio tuliona na mume wangu immediate solution otherwise utapiga sana na utafoka sana to no avail
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Ni hali ya kawaida kwa watoto wanaofuatana kwa karibu na hasa wakiwa "wachanga" hivyo na husababishwa na ushindani miongoni mwa watoto katika kupata attention ya wazazi.Wamezaliwa karibukaribu sana.
Ajitahidi kuwaelimisha ili watambue ni ndugu na wanahitaji kupendana.Wazazi nao wajaribu kuamulia ugomvi kwa hekima ili kuonyesha hali lakini hapohapo kuonyesha kumlinda anayeonewa bila kuchochea ushindani zaidi.

Ok, kumbeeeeee! ushukuriwe sana woman of substance
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
nashukuru wakuu, ni kama jioni hii naenda kuwa mwalimu kwa jamaa yangu. raha ilioje kumbe unaweza ukajiona mbumbumbu wakati madesa yako ya kumwaga tu humuhumu jamvini, lol!
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Hata wangu wanapigana sana mpaka ikabidi nimwombe dada wakitoka shule awatenganishe immediately wakianza kupigana

maana wakipigana mmoja atalia mpaka nirudi namkuta sauti imekauka, so siku wakiwa hawana ugomvi wanacheza kwa furaha siku ya ugomvi mmoja anakaa chumbani kwangu kuepusha shari la kilio cha kukausha koo

Nimeshaongea mpaka nimechoka kuhusu kupigana maana wanapishana miaka 3 na mmoja anamg'ata mwenzake na kumwachia makovu , so soln wakiwa kwenye ugomvi mood wanatenganishwa nikirudi simind kumkuta mmoja chumbani anaangalia cartoon au kalala, si unajua watoto wanapenda kukaa chumbani kwa baba na mama? So asiye mgomvi ndio anakaa huko

Kama kuna njia nyingine nisaidieni lkn hiyo ndio tuliona na mume wangu immediate solution otherwise utapiga sana na utafoka sana to no avail

Wazee hapa ni kama nimerudi UD, yaani haya madesa nadhani yatanifanya nionekane kipanga leo, teteteteee! kumbe nilikuwa kilaza before this moment on this issue, wmeeeeee! Thanx Nsionde, hiyo solution ya kuwatenganisha ntaishusha pia ili yeye achague madesa mwenyewe.
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,132
17,109
Muulize hospitali aliozalia ilifungwa na zoezi la wizra kama iko wazi awarejeshe huko wanajua pa kuwapeleka hao
 
Strategizt

Senior Member
Oct 16, 2009
177
31
Experience niliyo nayo mimi kwa watoto wangu mmoja ana 6 na mwingine 4 wamepishana miaka miwili. Wanapigana pia ila katika analysis ya haraka haraka nimegundua mdogo siku zote ndo mchokozi na anapenda attention kwa hiyo baada ya kugundua tatizo hilo, wakigombana tu na nikaona wazi kwamba yeye ndo ameanzisha ugomvi namuweka wazi yaani namwambia ukweli kwamba yeye ndo analeta problem hivyo namwambia kwamba aombe msamaha urgently otherwise unaongea m paka unachoka!!
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
ndo maana wengine wanawapishanisha watoto miaka 3-5

Ni kweli lakini mkuu maisha yenyewe ya bongo, unamaliza shule una miaka zaidi ya 35, then kama umepanga kuzaa watoto 4 au 5 si utajikuta unalea watoto-wajukuu mkuu? Ndo maana watu wengine wanalipizia hiyo delay fater then wanaacha biashara ya kushika shika nepi/papas! teteteeeeeeeee!
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Experience niliyo nayo mimi kwa watoto wangu mmoja ana 6 na mwingine 4 wamepishana miaka miwili. Wanapigana pia ila katika analysis ya haraka haraka nimegundua mdogo siku zote ndo mchokozi na anapenda attention kwa hiyo baada ya kugundua tatizo hilo, wakigombana tu na nikaona wazi kwamba yeye ndo ameanzisha ugomvi namuweka wazi yaani namwambia ukweli kwamba yeye ndo analeta problem hivyo namwambia kwamba aombe msamaha urgently otherwise unaongea m paka unachoka!!

Okeeeeeee!, nimekuelewa ndugu, hiyo pia ni good solution, maana itajenga pia hali ya kuheshimiana na kusameheana pia kati yao. kweli kabisa
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
....dahhh, napenda topiks kama hizi ambazo zinatutoa nje kidogo ya mazowea ya kila siku kushauriana mambo ya ndoa.
hebu ngoja nijaribu kuwatumia pm baadhi ya wanachama ambao najua wanaweza tusaidia malezi ya namna hii...pole sana bana...

nitarudi na ushauri...

Thanx mkuu, naomba ntupie hayo madesa watakaypkurushia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom