Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

Bhikola naungana nawe katika hoja zako nzuri zilizoshiba. Chamsingi hao walioko KIBONDO,TANDAHIMBA nao wafikiriiwe uhamisho wasiachwe mpaka waozee huko inakuwa si vyema kbs,kila mmoja anatakiwa aende kwenye mazingira magumu. Wanacholalamika wadau ni kuwa hao watoto wanaanza kazi mpaka wanazeeka na kustafu DAR.
 
hii nchi hiii ina wenyewe! na lazima ujulikane ili kupata hizo posts! puuuuuuu kwa li-ccm na watu wake!
 
Kwani hawana sifa?
Au wao hawatakiwi kufanya kazi serikalini?

Naona Boflo hii imekaa kiuchoyo mno.!
 
Last edited by a moderator:
una vested interests na hawa watoto. Haiwezekani wote wakawekwa sehemu "nzuri" as if watoto wa maskini ambao baba na mama zao hawana majina wasiwemo. Wangapi wapo mitaani hawana ajira na wana sifa nzuri, lakini wa vigogo wote wana kazi. Hakuna haki kabisa. Unasema kama hujafikiri !
angalia avatar yake ndio utajua 'picture speak more than words ati'
 
waacheni watoto wa vigogo wafaidi matunda ya wazazi wao,hakuna cha elimu wala nini,hao wamebebwa kama walivyobebwa mama salma kikwete akikosa mshindani ccm,vivyo hivyo la ridhiwan kikwete,inamaana ndani ya ccm hapakuwa na wanachama wenye sifa kiasi kwamba hao wakakosa wapinzani?

huo ni uongo wa mchana,walioko BoT na pahala pengine wamewekwa kutokana na nafasi za wazazi wao wala hapa hakuna ajenda ya kumbagua mtu.

kama unataka ushahidi,peleka mtoto wake akafanye interview kwenye shule kubwa za sekondari hapa nchini mfano kule kifungilo na kwingineko na hapo hapo awepo na mtoto wa kigogo,utaona matokeo yake,wa kwako atakosa sifa na kigogo atapeta.
 
Tuache wivu. Tujiulize je wanauwezo wa kufanya hapo? Je wanfanya kazi ipi ma upi utendaji wao? Kingine kwa jinsi nepotism ilivyo jadi ya taifa letu, naamini hata Nyinyi wanajamvini mtakuwa au umngethubutu kuajiri ndugu zenu sehemu nzuri.
Nani ambaye hataki ndugu,kaka, mdogo kupata kazi powa.
Hili ndilo taifa sisi sote tulitakalo. Sasa tukikataa kwa pamoja aina hiibya maisha, na pia tusemezane kwenye katiba mpya kwamba nepotism au upendeleo wa aina yeyote ni mwiko "kwa pamoja" naamimi tutakuwa taifa lenye mwelekeo thabiti na bota kabisa.
 
huu ujinga wa kuwasema watoto wa viongozi kana kwamba wao hawana haki ya kuajiriwa mi sikubalianai nao kabisa, nafikiri hoja ingekuwa:
wana sifa za kushika nafasi hizo au hawana sifa?
wana uwezo wa kuendesha nafasi walizo nazo au hawana uwezo?
walizipata kwa upendeleo au walishindanishwa na wengine katika usaili kisha wakapata?
elimu yao inaruhusu kushika nafasi hizo au hapana?

haya mengine ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi mwingine, kuwa mtoto wa waziri au wa nani sijui hakukuzuii kupata haki zingine kama mtanzania ikiwa pamoja na kuajiriwa
jamani muwaache wapumue,
msiwe kama uamsho ambao kazi yao ni kulalamika tu
unahusika binafsi kuwa katika hali uliyo nayo leo, never blame someone for the situation you are in

Issue hapa si kuwa na sifa ama kutokuwa nayo, kwakuwa wote hao wana taaluma za sekta ya afya.
Swali la msingi hapa ni kwanini wajazane Dar es salaam tu, kwanini wasipelekwe huko Tandahimba, Ngara, Serengeti, Namanyere ama Malinyi? kwanini wote warundikwe jijini Dar es salaam?
 
waacheni watoto wa vigogo wafaidi matunda ya wazazi wao,hakuna cha elimu wala nini,hao wamebebwa kama walivyobebwa mama salma kikwete akikosa mshindani ccm,vivyo hivyo la ridhiwan kikwete,inamaana ndani ya ccm hapakuwa na wanachama wenye sifa kiasi kwamba hao wakakosa wapinzani?

huo ni uongo wa mchana,walioko BoT na pahala pengine wamewekwa kutokana na nafasi za wazazi wao wala hapa hakuna ajenda ya kumbagua mtu.

kama unataka ushahidi,peleka mtoto wake akafanye interview kwenye shule kubwa za sekondari hapa nchini mfano kule kifungilo na kwingineko na hapo hapo awepo na mtoto wa kigogo,utaona matokeo yake,wa kwako atakosa sifa na kigogo atapeta.
Siyo kweli, mbona St. Marian Girls Sec. School ya Bagamoyo huwa inawatema hata watoto wa vigogo wanaposhindwa kufaulu mitihani ya kujiunga? Acha propaganda na conclusions za kiujumlajumla bila ya kufanya utafiti wa kutosha wa kile unachokusudia kukielezea.
 
Tuache wivu. Tujiulize je wanauwezo wa kufanya hapo? Je wanfanya kazi ipi ma upi utendaji wao? Kingine kwa jinsi nepotism ilivyo jadi ya taifa letu, naamini hata Nyinyi wanajamvini mtakuwa au umngethubutu kuajiri ndugu zenu sehemu nzuri.
Nani ambaye hataki ndugu,kaka, mdogo kupata kazi powa.
Hili ndilo taifa sisi sote tulitakalo. Sasa tukikataa kwa pamoja aina hiibya maisha, na pia tusemezane kwenye katiba mpya kwamba nepotism au upendeleo wa aina yeyote ni mwiko "kwa pamoja" naamimi tutakuwa taifa lenye mwelekeo thabiti na bota kabisa.

Hakuna cha wivu hapa watu wanaambiwa ukweli tu. Kinachotafutwa hapa ni usawa katika kupangiwa majukumu ya kulitumikia Taifa. Kwamba watoto wa wakulima tu ndio wanapelekwa huko vijijini lakini watoto wa wakubwa wanajazana hapa mijini tu. Kwanini wasiwapeleke huko Tandahimba, Kibondo, Malinyi, Tunduru ama Kilimatinde?
 
Siyo kweli, mbona St. Marian Girls Sec. School ya Bagamoyo huwa inawatema hata watoto wa vigogo wanaposhindwa kufaulu mitihani ya kujiunga? Acha propaganda na conclusions za kiujumlajumla bila ya kufanya utafiti wa kutosha wa kile unachokusudia kukielezea.

Kwa kumbukumbu zako Mwanaasha Kikwete alistahili kuhitimu Feza Girls? unajua ni kwanini alipata nafasi ya kusoma pamoja na kwamba alikuwa na kiwango duni?
 
Siku chache baada ya kuibuka mjadala wa kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hali kama hiyo imejitokeza tena kwenye Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na manispaa zake tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, JAMHURI imebaini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Idara hiyo, wametoa waraka wakihoji namna watoto hao wa vigogo walivyoweza kushika nyadhifa kubwa katika manispaa hizo, ilhali watumishi wengine wenye sifa, ama wakiachwa au wakipelekwa mbali na Jiji la Dar es Salaam.

Katika waraka huo, ambao JAMHURI imepata nakala yake, wanatajwa baadhi ya watoto wa vigogo na nyadhifa zao kuwa ni Janeth George Kahama, ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji.

Huyu anatoka katika familia ya Mzee George Kahama, mmoja wa mawaziri wawili walio hai wa kwanza katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika huru. Mwingine aliye hai ni Job Lusinde.

Waraka huo pia unasema nafasi ya Mganga Mkuu Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam inashikwa na Dkt. Hawa Rashidi Kawawa. Huyu ni mtoto wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanganyika, Waziri Mkuu wa Tanzania, na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Hivi ni kweli watoto hawa wa wakubwa ndiyo wenye sifa tu za kushika nyadhifa hizi? Kweli, wanaweza kuwa na sifa, lakini iweje wasipelekwe Tandahimba, Kibondo au Karagwe? Kwanini Dar es Salaam tu?" Wamehoji waandishi wa waraka huo.

Wameendelea kusema kuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ni Dkt. Gunini Kate Kamba. Huyu ni mtoto wa Kamba aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza na ndani ya CCM. Wadhifa wa karibuni kabisa aliokuwa nao ni wa ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo ni Dkt. Asha Omar Mahita. Dkt. Asha ni mtoto wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omar Mahita.

Mtoto mwingine wa kigogo ni Dkt. Amani Kighoma Malima ambaye ni Mganga Mfadhiwi wa Hospitali ya Temeke. Huyu ni ndugu yake na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Dkt. Amani ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini. Mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti alikuwa Waziri wa Fedha.

Aidha, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, ingawa si mmoja wa watoto wa vigogo, lakini alikuwa na uhusiano wa karibu mno wa kikazi na aliyekuwa Mganga Watoto wengine wa vigogo waliojazwa Idara ya Afya.
Watoto wa vigogo wameshika nafasi zote za Jiji - Ilala, Temeke, Kinondoni

Mkuu wa Serikali, Dkt. Deo Mtasiwa; aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka huu kutokana na shinikizo la madaktari waliogoma.

"Haya ni majina ya baadhi tu ya watoto wa vigogo katika Idara ya Afya katika Jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake. Tunauliza, iweje watoto wa wakubwa tu ndiyo washike nyadhifa hizi kwa Dar es Salaam na si mikoani?" Umehoji waraka huo.

Wiki iliyopita, JAMHURI iliandika taarifa ya kuwapo watoto wengi wa vigogo ndani ya BoT.

-----------------------------------------------------------
Hadi sasa, majina yanayovuma ya watoto hao ni:

1. Pamela Edward Lowassa,
2. Filbert Tluway Sumaye,
3. Zaria Rashidi Kawawa,
4. Harriet Matern Lumbanga,
5. Salama Ali Hassan Mwinyi,
6. Rachel Muganda,
7. Salma Omar Mahita,
8. Justina Joseph Mungai,
9. Kenneth Nchimbi,
10. Blasia William Mkapa,
11. Violet Philemon Luhanjo,
12. Liku Kate Kamba,
13. Thomas Mongella na
14. Jabir Abdallah Kigoda.
------------------------------------------------------------------
Kuwapo kwa watoto wa wakubwa katika sehemu nyeti na nzuri kumeanza kuzua minong'ono ya upendeleo miongoni mwa wananchi.

Mmoja wa wananchi amehoji hali hiyo kwa kusema, "Ninachojiuliza na sipati majibu mpaka sasa ni hiki, kama imetokea

coincidence (bila kutarajia) BoT ikaajiri watoto 14 wa vigogo; je, coincidence hiyo hiyo inaweza kutokea kwenye Wizara ya Elimu watoto wenye majina kama hayo hayo wakapangwa kwenda kufundisha shule za kata vijijini, ambako hakuna maji wala umeme na wakaendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo wa kizalendo bila kujali kuwa mishahara imechelewa na hawajapandishwa vyeo; na wakati huo huo wakiidai serikali sikivu malikimbizo?

THATS WHY TUNASEMA KUA PRO-CHADEMONSTRATIONS NI KAMA UAMSHO MEMBERS
HIVI NI LINI MTAACHA KULALAMIKA LALAMIKA NA KUFANYA KAZI YA KUJENGA NCHI??
NILITEGEMEA KUKUSIKIA UKIHOJI KWA USHAHIDI JUU YA UHALALI WA HIVO VITOTO VYA VIGOGO KUPATA KAZI EITHER HAWANA VIGEZO OR UPO USHAHID WA KWAMBA WAMEPITA KWA UJANJA UJANJA KWENYE USAILI WAO WA HIZO KAZI
SASA KAMA MUHUSIKA ANA VIGEZO STAHIKI ASIOMBE NA KUPEWA KAZI ETI KISA MZAZI WAKE ALIKUA KIGOGO???
THATS SO NONSENSE...!!
:smile: :smile:
 
Kwa kumbukumbu zako Mwanaasha Kikwete alistahili kuhitimu Feza Girls? unajua ni kwanini alipata nafasi ya kusoma pamoja na kwamba alikuwa na kiwango duni?

alibebwa hakuwa na kiwango cha kusoma feza!
 
Kama wangekuwa wanakula vyao tusingesema, tatizo hapa wanakula vya watanzania.

mkuu ni vyao ndomana wanakula, vingekwa vya watz wasingefanya wayafanyayo,mie najilaumu 2 kwann sikuzaliwa na kigogo lol
 
Sijipendekezi wala nini,ila siku zote maji hufuata mkondo.Haina ya kujaa sumu kuhusu hili bali nasi tuwaandae watoto wetu ili nao waje wafaidi hapo baadae,cha msingi ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na ufahari usio kuwa na maana.Kiukweli hakuna mtu maskini Tanzania bali ni kujiendekeza,uzembe,kujazwa sumu zenye figure kubwa za pesa,kutokuwa na ubunuifu,majungu ambayo ndani yake hamna elimu wala uthibitisho,ubinafsi miongoni mwetu pamoja na utegemezi wa ndugu wenye pesa ili ufanyiwe kila kitu.Na kwa wale ambao wanashbikia/kuponda hii kitu kuna lao jambo na mojawapo ni kuwajaza sumu watoto wa wenzao ili kufifisha ndoto zao,kimsingi hoja hii imekaa kiunafiki kwani haina evidence na inamuonesha mleta hoja hii pengine alikwishadendwa/kutoswa na mfumo.Wivu kitu kibaya sana.
 
huu ujinga wa kuwasema watoto wa viongozi kana kwamba wao hawana haki ya kuajiriwa mi sikubalianai nao kabisa, nafikiri hoja ingekuwa:
wana sifa za kushika nafasi hizo au hawana sifa?
wana uwezo wa kuendesha nafasi walizo nazo au hawana uwezo?
walizipata kwa upendeleo au walishindanishwa na wengine katika usaili kisha wakapata?
elimu yao inaruhusu kushika nafasi hizo au hapana?

haya mengine ni ubaguzi kama ulivyo ubaguzi mwingine, kuwa mtoto wa waziri au wa nani sijui hakukuzuii kupata haki zingine kama mtanzania ikiwa pamoja na kuajiriwa
jamani muwaache wapumue,
msiwe kama uamsho ambao kazi yao ni kulalamika tu
unahusika binafsi kuwa katika hali uliyo nayo leo, never blame someone for the situation you are in
Bila shaka na wewe pia ni mmoja wao...

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Nchi inaendeshwa kisultani mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom