Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Wakuu,
Ukiwa unatumia barabara unatakiwa uchukue tahadhari hata ukiwa kwenye sehemu ya kuvukia (zebra crossing).
Kuna watu wameshajiwekea nikipita kwenye zebra lazima chombo kisimame, kwahiyo yeye hajali chochote akifika kwenye zebra ni kuvuka tu. Anasahau kwamba mambo mengi yanaweza kwenda vibaya, mtu anaweza akawa na dharura anawahi mahala fulani kuna tatizo, chombo kinaweza kufeli breki, mtu anaweza akatoka resi huko stress zimempiga hajaona mtu akaondoka na wewe, bodaboda na bajaji inaweza kuchomoka huko ikakuvaa na kadhalika.
Sasa kuna wenzangu na mimi, akiwa kwenye zebra anaona huu ndio muda wake wa kutamba, muda wa kukomoa wenye magari, kuonesha machejo, kutembea kama mlimbwende, yaani kama vile malaika amesimamisha/atasimamisha vyombo vyote ili yeye apite, my friend endelea na huu mchezo ipo siku yatakukuta.
Kuwa makini wakati wote unapokuwa barabarani, lakini pia acha hizi tabia za kijivuta na kudhani kwamba muda wote madereva watakuwa 100% sawa.