Hivi madereva huwa hamtuoni kwenye zebra tukisubiri kuvuka?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Leo ni zamu ya madereva kuwa kwenye kiti cha moto:D.

Medereva mnakwaza sana kwenye kipengele hiki. Mtu anaweza kukaa muda mrefu kwenye alama za kuvukia (zebra crossing) huku wenye vyombo vyao wanapita tu utafikiri hawaoni mtu. Tena ukiwa peke yako ndio kipengele zaidi, utakaa hapo labda mpaka upate ujasiri wa kujitanguliza kidogo ndio magari yanasimama au mpaka aje askari kusimamisha magari.

Mpaka atokee dereva anayefuata sheria na kujielewa ujajikuta umekaa muda mrefu bila sababu za msingi.

Madereva wenye tabia hii mjirekebishe, fuata sheria mambo yanyooke kweye mstari. Kuna akina sisi tunavuka kwenye zebra tu na hatuwezi hata kutanguliza kichwa mpaka gari zisimame, msitufanyie hivyo.
 
Zebra crossing kweli ni eneo maalum la watembea kwa miguu kuvukia barabara. Kinachosababisha madereva wengi kuendelea na safari kama ulivyosema hapo juu zipo sababu nyingi
1: Kwa jiji hasa la Dar unakuta magari hayo yametoka tu hatua chahche nyuma kusimamishwa na askari usalama barabarani kwa zaidi ya dakika 30 mpaka 40 hivo kumbuka na watumiaji wa magari hayo nao wana safari zao za muhimu na wanahitaji kuwahi pia.
2: wavukaji wa zebra kumekuwa na kasumba unamuacha mtu apite lakini badala ya kuvuka kwa haraka wanavuka kwa kujivuta vuta na wengine ndiyo kwanza wanachart na simu zao.mbaya zaidi unakuta umepisha unataka kuondoka mwingine mmoja ndiyo naye anakuwa kama kazinduka usingizini anataka kuvuka.

3: Zebra haimaniishi tu ukifika unavuka ndiyo maana nchi za wenzetu unakuta taa za kupeana zamu. siyo kila ukifika zebra gari zisimame kumbuka watumiaji wa magari nao wanatakiwa waendelee na safari kama wewe unayetumia kutembea.
4: Daladala au bajaj kutumia zebra kama eneo la kupakia abiria unakuta kushoto kwako lipo daladala au bajaj imesimama zebra unasimama kumbe hakuna mvukaji na hata ukikuta hamna daladala eneo hilo limekuwa kama kituo unaweza simama kumbe mtu anagonja daladala au bajaj.

5: unakuta trafiki au taa zimeruhusu gari kupita lakini watembea kwa miguu nao wanataka kuvuka muda huo huo yaani kusubiri taa ziwake nyekundu kusimamisha magari hawataki

Haya ni machache tu lakini kero zipo nyingi mno
 
wavukaji wa zebra kumekuwa na kasumba unamuacha mtu apite lakini badala ya kuvuka kwa haraka wanavuka kwa kujivuta vuta na wengine ndiyo kwanza wanachart na simu zao.mbaya zaidi unakuta umepisha unataka kuondoka mwingine mmoja ndiyo naye anakuwa kama kazinduka usingizini anataka kuvuka.
Hapa hasa ndio kwenye tatizo. Unakuta mtu anavuka kama vile barabara yote mali yake, anaringa kabisa, kisa yupo kwenye zebra.
 
Hasa madereva wa arusha ni jau tupu hawajuinhii zebra wal nin ukisema utaambiwa tafuta hela
Pale Philips wanasimama hasa wakiona mbele yao kuna wazee wa mavazi meupe ndio utakuta midereva isofata sheria ujifanya some la zebra walilielewa sana huko vyuoni
 
Wakuu,

Leo ni zamu ya madereva kuwa kwenye kiti cha moto:D.

Medereva mnakwaza sana kwenye kipengele hiki. Mtu anaweza kukaa muda mrefu kwenye alama za kuvukia (zebra crossing) huku wenye vyombo vyao wanapita tu utafikiri hawaoni mtu. Tena ukiwa peke yako ndio kipengele zaidi, utakaa hapo labda mpaka upate ujasiri wa kujitanguliza kidogo ndio magari yanasimama au mpaka aje askari kusimamisha magari.

Mpaka atokee dereva anayefuata sheria na kujielewa ujajikuta umekaa muda mrefu bila sababu za msingi.

Madereva wenye tabia hii mjirekebishe, fuata sheria mambo yanyooke kweye mstari. Kuna akina sisi tunavuka kwenye zebra tu na hatuwezi hata kutanguliza kichwa mpaka gari zisimame, msitufanyie hivyo.
Muwe mnajikusanya wengi ndio tunawasubiri mnavuka, ila mmoja mmoja tutawaburuza kwenye hizo zebra.

Pia mnapovuka kwenye zebra kwenye mataa, muache tabia magari ya upande huo yanaporuhusiwa nanyi ndo mtake kuvuka.
 
Mmesikia?Mtaburuzwa mkiwa wazembe!,Angalia Huwa yafeli breki!
 
Back
Top Bottom