Watembea kwa miguu wanagongwa sana na bodaboda Mbagala Rangitatu na Zakhiem Dar es salaam, hali ni tete. Polisi wa usalama barabarani tusaidieni

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,675
22,264
Ninaliomba jeshi la polisi usalama barabarani Dar es Salaam ikiwezekana wote mpige kambi kwa siku mbili eneo la Mbagala ili mdhibiti hili kundi la bodaboda wahalifu, ninaposema wote najua bodaboda ni wajeuri hawazuiliki.

Tatizo ni nini, tatizo lililopo ni uhalifu unaotokana na madereva wa bodaboda kuendesha pikipiki zao bila kufuata sheria za usalama barabarani, wao wanatumia barabara wapendavyo mtindo wa kupishana njia moja wakati barabara zimetenganishwa.

Hili eneo la Mbagala ni dogo lakini lina idadi kubwa sana ya bodaboda kuliko maeneo yote Dar na hii inatokana na idadi kubwa ya watu wanaopita Mbagala kuelekea mkoa wa Pwani ambao ni jirani.

Kwanini trafiki wote, madereva wa bodaboda ni wajeuri hawadhibitiki kirahisi labda kwa kuweka mageti wasiweze kupenya kwa pamoja kwa kutumia wingi wao.

Ninatoa wito huu kutokana na idadi kubwa ya ajali za watembea kwa miguu kugongwa kwa makusudi kwenye njia za watembea kwa miguu na wakati mwingine wakiwa wamesimama kando ya barabara! Ni jambo la kawaida yaani kugongwa hakuepukiki ni wakati wowote, ajali ni nyingi na madereva wahusika huwa hawasimami, wanakimbia.
 
Juzi pia kuna mtu aligongwa na bodaboda kwenye service road hapo

Mitaa ya biafra alikata moto pale pale

Ova
 
Back
Top Bottom