N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,990
- 12,019
- Mtume Boniphace Mwamposa ametamka: “Watanzania wengi ni wavivu ” Watu wakakasirika, wengine wakabaki kimya. Lakini hii si mara ya kwanza kauli hii kusemwa na mtu maarufu kama Mtume Mwamposa.
- Mwaka 2011, Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kusema waziwazi kuwa “Watanzania tumejaa visingizio, tunapenda kuwalaumu wengine na hatutaki kufanya kazi kwa bidii.” Alisema haya kwa uchungu, akisisitiza kwamba uvivu ni kikwazo kikuu kwa maendeleo yetu Watanzania wengi wavivu wa kufikiri-Mkapa
- Hii ina maana moja tu: kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, viongozi wetu wamekuwa wakituamsha kutoka usingizi wa uvivu – lakini bado tunasuasua. Tumezoea starehe kuliko jasho, lawama kuliko suluhisho.
- Hapa majuzi kila mtu anamlaumu Mchina kwamba kajaa Kariakoo amekuja hadi mikoani. Mchina huyohuyo amejaa kila eneo na anafanya "retail" business. Nani alaumiwe? Mchina, mzawa mvivu, au serikali?>
- Tuna ndoto za maisha bora, lakini hatuko tayari kulala saa 5 na kuamka saa 11 kufanya kazi. Tunataka magari na majumba, lakini hatuwezi kusimamia muda wetu wala kujifunza kwa bidii (matokeo yake hadithi zetu nyingi ni kuwahusu wenye mali nyingi na wenye magari ya kifahari-hao nao tunawaita wana utajiri wa manyoka - hatuamini katika bidii na maarifa kama chanzo cha ukwasi-TUNA SHIDA KUBWA).
- Uvivu wetu uko kila mahali: kwenye vijiwe, ofisini, mashambani, na hata kwenye ndoto zetu. Tunatamani tusifanye chochote lakini tupate kila kitu. Hii ni ndoto isiyo na mwisho (Nililima kwenye moja ya vijiji vya Tukuyu wenyeji wanataka ujira mkubwa walipwe kwa pay-day na kazi wanafanya kisoda - ikabidi niwe naenda Ileje kuwaleta Wandali wafanye kazi hapo shambani au niende Ntokela kuleta Wasafwa waje kufanya kazi hapo shamba - Tuna shida KUBWA).
- Kila siku tunakutana na vijana wenye nguvu, elimu na muda — lakini wanaishia mitaani wakisubiri miujiza. Hawajafungua biashara, hawajajitolea, hawajifunzi ujuzi wowote. Wanangoja “koneckshen” ni watu wa kulaumu na matusi, hawana nidhamu yao binafsi wala ya kazi, hawaajiriki-ukiwaajiri lazima wakuibie sana.
- Si vijana tu – hata taasisi zetu baadhi zimelemaa. Uamuzi mdogo unachukua miezi. Miradi mikubwa inacheleweshwa kwa sababu ya uvivu wa kiutendaji na kukosa uwajibikaji.
- Tumejifunza kuishi kwa “polepole,” tukikumbatia uzembe kama sehemu ya utamaduni. Lakini dunia haikusubiri – mataifa mengine yanapiga hatua kwa bidii na nidhamu.
- Kauli ya Mwamposa na ile ya Rais Mkapa zinafanana kwa ujumbe mmoja: Uvivu ni adui wa maendeleo. Na Watanzania wengi, tusipobadilika, tutajikuta tukibaki nyuma zaidi.
- Kwa hiyo leo, si lawama bali ni wito: Amka. Jitume. Tenda. Tuanze na sisi binafsi. Tufanye kazi kwa bidii, tuthubutu, tuache kusingizia serikali kila siku. Mabadiliko hayawezi kuja kama hatutayachochea wenyewe.
- Tunazo rasilimali nyingi sana zinazoweza kutukomboa. TUAMKE; TUBADILIKE.
NB: Soma kimyakimya, toa comment, matusi kwenye huu uzi pendwa hayaruhusiwi. Nyadikwa huwa ha tolerate ujinga.
Wahega