Watanzania wavamiwa na kupewa kichapo Ugiriki

Hivi kumbe huko Ugiriki kuna Wamatumbi wengi hivyo...halafu kuna kipindi nadhani 2010 nilisikia watu wanapewa uraia huko sasa sijui na nyie ndugu zetu mlibahatika kuwa wana EU
aisee hata mimi nimeshikwa na mashangao kuziona hizi sura za wamatumbi wenzangu zikiwa zimeshikwa na unyonge wa tukio husika.niwamatumbi kweli kweli hata hawajapoteza facial identity yetu.:wink:
 
Hivi hawa wa Tanzania kweli zimo nyie??? katika wakati kama huu halafu baada ya matokeo kama hayo mumejiweka katika hiyo sehemu sasa hao jamaa wakirudi tena na sila nzito mtafanya nini ? wao kwao Nchi yao imeanza kunakamia hasira zao watakumalizieni nyinyi tu ondokeni sehemu hiyo mpaka hali ya usala irudi kujifanya wajuwaji kutakupelekeni kupoteza maisha yenu.
 
Boksi la Ugiriki halilipi.

Na ndo maana watu wenyewe choka mbaya tu utadhani wanakula vumbi la bongo.

Waondoke tu huko maana wasije sasa wakaanza kuuliwa bure.

Nianza kwa kuwapo pole kwa yaliyotokea, hii si sababu ya tukio la ajali ya Mgiriki huko Dar, bali kuna kitu ambacho wamepata weak point kinachowaumiza kila kukicha. Jambo hilo lipo po pote, bahati nzuri mataifa makubwa sheria ni kali sana na ulinzi uko wa hali ya juu iwe usiku kwa njia ya telecom/siren nk kwani tukio kama hili linaonekana si dakika chache, kwa nchi kama zilizo na ulinzi wa hali ya juu wahusika wangedakwa kabla hawajafika mbali.

Nawaasa watanzania kutazama future ya homeland, kwani hali mbaya ya uchumi imeikumba dunia , wazawa wenya fikra finyu hufikiria wakuja ndio moja wapo ya kuwakosesha ajira, kwani wakuja po pote huwa makini katika kupata ajira kama bongo tunavyolalamika wageni kupata ajira kuliko wazawa stahii.

Nyani Ngabu, watanzania na waafrika wengi huweka umuhimu katika mvao tofauti na nchi za wenzetu, kwani mvao huwa ni muhimu kwa shughuli au nafasi fulani rasimi. Binafsi sijaona mchoko katika hawa, wote wanaonekana kuwa na siha nzuri tu, ila wamejirekebisha na hali ya wakazi wa nchi za ulaya na bara la Marekani kaskazini ambao utaona mivao yao ni just wear casual badala ya official tulivyozoea bongo. Bongo nikivaa kaputula yangu na dogo (kamanda wangu) kumtembeza mitaani ajue nilikozaliwa dingi wake watu wananikodolea macho kana kwamba ni uchi, mazoea hujenga tabia, kumbe ni kujiwezesha upepo mwanana unipepe na vinyoleo kupumua vizuri. Wabongo tulivyo tukienda kumpolekea mtu airport tunatazamia awe amejifunga kitanzi kinachoning'inia shingoni huku mwili umefunikwa na pambas za kimagharibi, hapo ndo utaona anakodolewa macho kwamba amejaa na kushiba na mifuko pasi shaka imenona. Wakikuona unateremka na kaputula yako top ikiwa ni t-shirt au jacket ya kujikinga na cool air ya angani, utawaona wanatazamani na kufikira jamaa si mdandiaji wa kawaida wa haya mapipa, wenye nazo huwa na kitu cha kutisha masho. Soma kwanza mazingira ya watu kabla ya kutoa tamko la hitimisho.

Ukifika hospitali nchini Marekani vigumu kumtambua daktari kwani wote ni full nursing uniform, na pengine unaona nurse aliyenawiri na kuwa na kila aina ya kufikira ndiye doctor kumbe ni msafishaji tu. Wenzetu hawako kama tuuonavyo wabongo. Kazi ni ya wote na hakuna anayeonekana kazini kuwa na mwonekano wa pekee hata kama ni mwajiri.

Nawaomba watanzania, huko tuliko tuwe na malengo ya muda mfupi na mrefu, dunia ya leo inaelekea kujirudia historia ya
dark-ages in middle ages. Tunaona ya akina Cameroon si mapya kwani yamekuwapo na kupata nguvu kwa wakati fulani ni kutokana na msukumo wa mengi katika jamii ikiwepo matumizi ya madawa yasiyostahiki kwa binadamu, hali mbaya ya uchumi na mambo ya kukatisha tamaa maisha kwani wengi wamemweka Mungu kando na kuona kumwabudu Mungu ni just life stile.

Hili la kuendeleza utamaduni wa kitanzania kumwabudu Mungu wengi wakishafika nje ni kama mbuzi mwenye njaa akifunguliwa hawasikii hili la lile, inaelekea afrika ni kasumba tu kuabudu au lifestile kwani tukishafika nje hatuna habari tena.
 
Du! Poleni saaana ndugu zetu huko mlipo. Wagiriki hawajashirikisha akili zao vizuri maana huyu mgiriki aliyeuwawa hakuuwawa kwa makusudi kama waowanavyofanya
 
This is an act of terrorism.

Sidhani kama imefikiwa kiwango hicho, nchi za ulaya vijana mitaani wamekuwa choka ile mbaya, wakishavuta ile kitu kwenye magenge yao siwezi kushagaa kwa yaliyojilia sana sana wakishahamasishana kwa kisingizio fulani kama kilichotokea Dar kwani kitakuwa kimeonyeshwa live kwenye vyobo vya habari huko kwao.
 
Kawaida tu za nchi za Ulaya Wakiwa hawataki Wageni wanafanya hivyo hata kuuwa watu wanauwa na

Serikali zao Hazisemi kitu zinawapendelea Wenye nchi kuliko Wageni tofauti na huko kwetu Serikali za Ki Afrika

Zinawakumbatia wageni Weupe na kuwaweka kipa umbele kuliko wewe Mwananchi mlala hoi. Wazungu walikuwa

wakati wa mkoloni walikuja kwetu Africa tuliwapokea na walichukuwa kila kitu chetu tukawaondowa ili tuwe na
uhuru sasa sisi tunawaendea kwao.

Hawatutaki hata kidogo Waswahili husema Mkuki kwa nguruwe ndio halali yake kwa binadamu ni mchungu.
 
Kuweni makini hasira zinaweza zikazagaa mpaka kwenye maoneo yenu ya kuishi( Residential areas za Wa TZ). kama vipi tizameni uwezekano wa kurejea nyumbani mitaji ipo siku hizi. It is only ideas and creations are what matters.
 
Mkuu luteyega

Daktari Mgiriki auwawa Tanzania..

Greek woman dies after thieves drag her on road Monday, 24 September 2012 22:52 By The Citizen Reporter Dar es Salaam. A Greek woman has died in the course of preventing her handbag from being snatched by unidentified people in a vehicle.Ms Petroula Chatzipantazi, 48, who was spending her last night in the country before travelling back to Greece yesterday, was walking by a roadside with her colleagues, she died of internal bleeding at the Aga Khan Hospital late Sunday night. The Ilala regional commander, Marietha Minangi, confirmed the incident and said investigations were
still underway.


Ms Minangi told The Citizen in a telephone interview yesterday that Ms Chatzipantazi, a medical doctor seconded to work in Tanzania as a volunteer by the ministry of Foreign Affairs of Greece, was in a group of about 30 colleagues walking down the road
going to an event at the Hellenic Centre along Ali Hassan Mwinyi road in the city centre.


But as they were walking a vehicle approached from behind but upon reaching Ms Chatzipantazi was in front of the group, one of the persons in the vehicle snatched her handbag. She held firmly as the vehicle speeded up. Because she could not let go of the bag, she ended up being dragged for some metres before letting go.


“She started breeding profusely and a preliminary report from the Aga Khan hospital indicated that she died of internal bleeding,” ACP Marietha said. The body is preserved at the Agha Khan hospital, waiting to be flown to Greece for burial. Efforts to get the ministry of Foreign Affairs and International Relations and the Consulate of Greece in Dar es Salaam to comment on the incident proved futile, but information from compatriots who spoke to The Citizen said she visited hospitals in Ifakara and Iringa districts.


“Sunday night was her last night in Tanzania because she was to travel back to Greece yesterday. She came on September 13,” a
compatriot, who preferred anonymity, told The Citizen yesterday.

hapa lazima wawaonesha wapo serious kiasi gani na raia wao ila bongo kimyaa na hapo na waonea huruma sana nyie kina MziziMkavu sijui itakuwaje upande wenu
 
Last edited by a moderator:
hapa lazima wawaonesha wapo serious kiasi gani na raia wao ila bongo kimyaa na hapo na waonea huruma sana nyie kina MziziMkavu sijui itakuwaje upande wenu
Mkuu ndetichia ni kujitetea tu wakitupa mawe na sisi tunatupa mawe vita mtindo mmoja si unajuwa imeandikwa kwenye Torati jicho kwa jicho meno kwa meno pua kwa pua wakirusha mawe na tunajibu kwa hayo mawe. Wakirusha silaha hapo itabidi tutoke mbio hakuna cha kusimama.


 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndetichia ni kujitetea tu wakitupa mawe na sisi tunatupa mawe vita mtindo mmoja si unajuwa imeandikwa kwenye Torati jicho kwa jicho meno kwa meno pua kwa pua wakirusha mawe na tunajibu kwa hayo mawe. Wakirusha silaha hapo itabidi tutoke mbio hakuna cha kusimama.




copy it mzee ila nikuomba mungu isifikie huko kwenye bunduki maana ni soo..
 
Last edited by a moderator:
Ila kiukweli Mh Said Mwema tunakuomba uwafuatilie hao vibaka wanaotumia magari na kuwaadabisha
maana wamezagaa maeneo ya Upanga,Masaki nk jijin DSM maana wanatuletea matatizo kwa watanzania wenzetu
 
Back
Top Bottom