Watanzania twendeni Congo tukawekeze Sekta ya Usafiri wa majini na mafuta

Tanzania government wawekeze nje ya mipaka mmh!.
Tumechelewa kampuni zote zinazojenga mabarabara Tanzania na Africa nzima ni kampuni za serikali ya CHINA .China inamiliki hisa asilimia 100.Ikitokea tenda popote duniani wana bid.Ndio wamejenga hadi Reli ya SGR ya Kenya.

Kenya wenyewe kampuni yao ya umeme kama ilivyo yetu ya TANESCO huwa inabid Tenda za miradi ya umeme nje ya nchi na imeshashinda Tenda za mabilioni ya dola ikiwemo ujenzi wa miradi ya umeme Djibouti.

Mashirika yetu ya umma yanatakiwa kuanza kuvuka mipaka ya nchi kutafuta tenda mashirika kama TTCL,Bandari ,Tanesco nk Hata TRA yaweza tafuta tenda za kuendesha mifumo ya kodi mataifa mengine.
 
Mkuu, shirika la reli liunde meli?
Hujui kitu na unaishi Tanzania?.Hivi wewe unaishi ubelgiji au? Hujui Tanzania kuwa shirika la reli linamiliki meli pia zote zilizoko ziwa Tanganyika,Ziwa Nyasa na Ziwa VICTORIA? Hujui kuwa wameshaunda meli mpya hapahapa nchini kwa ajili ya huko maziwani? Au wewe unavyojua na ujuaji wako TRC haina meli?

Hakuna kitu kibaya duniani kama kusoma kwa kukariri kama wewe ulivyokariri nyie ndio mnatufanya watanzania wote tuliosoma tuonekane hopeless
 
Tumechelewa kampuni zote zinazojenga mabarabara Tanzania na Africa nzima ni kampuni za serikali ya CHINA .China inamiliki hisa asilimia 100.Ikitokea tenda popote duniani wana bid.Ndio wamejenga hadi Reli ya SGR ya kenya.....
Sawa sawa mkuu, ila serikali hii hii ikawekeze nje ya Tanzania kweli mmh!
 
Hujui kitu na unaishi Tanzania?.Hivi wewe unaishi ubelgiji au? Hujui Tanzania kuwa shirika la reli linamiliki meli pia zote zilizoko ziwa Tanganyika,Ziwa Nyasa na Ziwa VICTORIA? Hujui kuwa wameshaunda meli mpya hapahapa nchini kwa ajili ya huko maziwani? Au wewe unavyojua na ujuaji wako TRC haina meli?

Hakuna kitu kibaya duniani kama kusoma kwa kukariri kama wewe ulivyokariri nyie ndio mnatufanya watanzania wote tuliosoma tuonekane hopeless
Mkuu, Umeandika mengi lakini hayana maana. Jifunze kwanza MARINE SERVICES COMPANY LIMITED (MSCL) ni nini.

Baada ya kuvunjika kwa East African Railways and Harbours Corporation mwaka 1977, TRC ilisimamia na kutoa huduma za reli na meli nchini, 1997 TRC iligawanywa na kuundwa shirika la meli (MSCL).

MSCL ni shirika linalojitemea kama ilivyo kwa Shirika la Posta na TTCL (simu) baada ya kugawanywa toka Posta na Simu (Tanzania Posts and Telecommunications Corporation ) miaka ya 1993/94 na kuwa mashirika mawili yanayojitegemea.
 
Tumechelewa kampuni zote zinazojenga mabarabara Tanzania na Africa nzima ni kampuni za serikali ya CHINA .China inamiliki hisa asilimia 100.Ikitokea tenda popote duniani wana bid.Ndio wamejenga hadi Reli ya SGR ya kenya...
Wavuke mipaka hapa ndani wameshamudu?
 
Wavuke mipaka hapa ndani wameshamudu?
Mfano Tanesco bado kidogo tu wanakamilisha kufunga umeme kila kijiji nchi nzima vimebaki vichache tu waweza anza kusaka tenda nje kazi iliyobaki sio kubwa

TTCL wangeweza kuvuka bila shida kwenda kusaka masoko nje

Shirika la bandari laweza anza tafuta tenda kuanzia za kujenga na kuziendesha za nchi kama Congo nk

Hata TANAPA waweza tafuta tenda za kuendesha mbuga nje ya nchi wakaondoka na kampuni zetu za utalii kwenda kuendesha mbuga na utalii nchi zingine kama Congo nk

SUMA JKT pia waweza wekeza nje kwenye sekta nyingi tu
 
Wafanyabiashara wenyewe serikali kuutwa kuwakalia kooni...hiyo mitaji ya kujitanua kwenda nje ipatikane wapi? Anza kwanza kuwarekwbisja hao TRA ....then tukuze biashara zetu hapa ndani...ndo tufikirie nje...
 
Tumechelewa kampuni zote zinazojenga mabarabara Tanzania na Africa nzima ni kampuni za serikali ya CHINA .China inamiliki hisa asilimia 100.Ikitokea tenda popote duniani wana bid.Ndio wamejenga hadi Reli ya SGR ya kenya...
Tatizo Wachina wanao fanya kazi na serekali yao wana uzalendo wa kweli sisi bado ni walaji wa 10%!
 
Mfano Tanesco bado kidogo tu wanakamilisha kufunga umeme kila kijiji nchi nzima vimebaki vichache tu waweza anza kusaka tenda nje kazi iliyobaki sio kubwa...
Tatizo lipo wao wana vitendea kazi kushindana nao wakati wewe vitendea kazi unaenda nunua kwao wata kushinda tu!

Sisi tulitakiwa tuwe kwanza na Kiwanda cha kuzalisha chuma aina zote kutoka kwenye chuma kitakacho chibwa haha hapa ndani ya nchi!
Vinginevyo mjomba safari ni ndefu
 
Back
Top Bottom