Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Mkuu naona bado uko kwenye jinamizi la jiwe
 
Profesa Cheeseman ambae kiumri bado kijana sana (ana miaka 42) amewahi kuandikia Daily Nation la Kenya.

Alijiuzulu kuandikia gazeti hilo kwa kudai kuna censorship.

Kila nchi ina maamuzi katika kuangalia ufanisi wa waandishi wa habari kwamba hawaandai sumu ya kuwalisha wasomaji.

Sumu hizo ni uchochezi, fake news na habari zisizo na vyanzo vya kuaminika.

Hivyo tokea sakata la Daily Nation profesa Cheeseman hawezi kuwa na mtazamo chanya juu ya Afrika.

Moja ya nyenzo muhimu kabisa kwa mwandishi wa habari ni kuwa na "reliable sources", wengi hawana akiwemo profesa Cheeseman.

Huu ni wakati wa waandishi nguli kama wewe bwana Mayalla kuanza kupika waandishi wapya kabisa na walo na maono ya kitaifa na pia kujifunza kutoka propaganda za nje.

Waandishi wa habari wenye "critical thinking" hawapo Tanzania kwa sasa.
 
Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.
Uongo ni upi hapa? mfano,unambwa mkali nyumbani anakuja jirani yako nyumbani kukudai deni anamrukia na kuanza kumlarua mbele ya macho yako, halafa mwenye mbwa uko kimya unatizama tu kinachoendelea bila kumkemea mbwa wako. Tafsiri ya majirani zako wanaoshuhudia hicho kitendo wata tafsiri nini>
  1. Kwa kuwa mbwa ametenda hayo yote mbele yako na hukuchukua hatua basi ametenda kwa ridhaa yako
  2. Kwa kuwa jirani alikuwa anakudai deni basi hukuchukua hatua ili mbwa amkomeshe asirudi tena kukudai
  3. kwa kuwa jirani anaonekana ana kiherehere na ushupavu wa kuja nyumbani kwako kukudai ulitaka ashambuliwe hadharani na maumivu yake yawe mfano na fundisho kwa wengine wanao kudai waache kukudai.
Dhana zote nzuri na mbaya zitakuwa halari kwa mwenye mbwa kwa kuwa anawajibika na matendo ya mbwa alie chini ya udhibiti wake,tofauti na hivyo anawajibu wa kutoka nje na kukemea na kama hawezi basi atoe ufafanuzi kwa nini hakukemea. huo ulikuwa mfano turudi kwenye uhalisia.
  • Kuna kosa lolote kisheria amelifanya mbowe kufanya makongamano ya kuhamasisha katiba mpya?
  • Kwa nini chama chake wanafanya makongamano na mikutano ya hadhara bila bughudha yoyote?
  • Sio kweli kuwa alituahidi kuwa atatutendea haki sisi sote bila kutubagua ni nini kimemkuta akageuka jiwe?
  • Watu hawalalamiki kuhusu miamara?
  • Je tukisema anatumia tukio la mbowe kututoa kwenye reli ya kudai katiba na miamara chechefu tunakuwa tumekosea.
  • Kwa matendo ya aina hii mnataka tusifiwe? au tukosolewe na kukemewa ili tujifunze kutokana na makosa yetu,kwani iko wazi kabisa watawala wa kiafrika ndio wanaongoza kwa kukosa uvumilivu dhidi ya wapinzani wao kisiasa.Afrika siasa ni sawa na biashara mtu anajibinafsishia hataki kugawana na wenzake.
PASCO iko hivi ndugu yangu hao tunaowaita mabeberu ndio hao hao walau wanatusemea tunapo setwa na watawala wetu,sio wana habari,wanadini maaskofu wala mashekh wala mtu yeyote anawasemea wanao nyanyaswa sisi tumegeuka kuwa nchi ya walamba miguu acha waendelee kutusemea.
Ni hayo tu ndugu yangu.
2853653_IMG_20210704_051559_619.jpg

Tusigeuke kuwa wanafiki dhidi ya taifa letu kama kweli sisi ni wazalendo tuanze na HAKI kwani haki huinua taifa.
 
Katika hili nakuunga mkono,nchi hii inafuatiliwa sana,kiukweli utawala uliopita ulileta doa kubwa huku nchi ikifuatiliwa kwa karibu kuwa na element za udikteta.Haiwezekani mdada wa CNN aielewa vyema katiba ya nchi hii,anamuuliza mchambuzi wa masuala ya kidemokrasia kwa nchi za Africa hadi nikashaangaa.CNN ni tawi la CIA na FBI.Itakuwa tunawachunguzi humuhumu wa mabeberu.Wanasiasa waliopo ughaibun nao wanaichafua nchi hii,hawezekani Lissu anasema hatutawadhamin huku akitaka waachiwe bila masharti yeyote na imekuwa hivyo,kwanini anajiamini hivi.Wanasiasa wa upinzan warudi nchini baada ya maridhiano,kuna mpasuko nchi hii.
 
Hakika....

Hakika.....

Hao jamaa kazi yao ni Kusababisha INSTABILITIES kwa nchi zinazoendelea.......

Lissu anatumikia maslahi yao.....
Lema anatumikia maslahi yao....

Wameisema RWANDA wee ,bado KAGAME yupo.....

Wameisema UGANDA wee,bado M7 yupo......

#KaziIendelee
 
Profesa Cheeseman ambae kiumri bado kijana sana (ana miaka 42) amewahi kuandikia Daily Nation la Kenya.

Alijiuzulu kuandikia gazeti hilo kwa kudai kuna censorship.

Kila nchi ina maamuzi katika kuangalia ufanisi wa waandishi wa habari kwamba hawaandai sumu ya kuwalisha wasomaji.

Sumu hizo ni uchochezi, fake news na habari zisizo na vyanzo vya kuaminika.

Hivyo tokea sakata la Daily Nation profesa Cheeseman hawezi kuwa na mtazamo chanya juu ya Afrika.

Moja ya nyenzo muhimu kabisa kwa mwandishi wa habari ni kuwa na "reliable sources", wengi hawana akiwemo profesa Cheeseman.

Huu ni wakati wa waandishi nguli kama wewe bwana Mayalla kuanza kupika waandishi wapya kabisa na walo na maono ya kitaifa na pia kujifunza kutoka propaganda za nje.

Waandishi wa habari wenye "critical thinking" hawapo Tanzania kwa sasa.
kuna propaganda gani hapo nawauliza?
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Pascal Mayalla MUNGU hadhihakiwi umetumia lugha ya maslahi yako binafsi,simama katika haki we we na rais nani wakulisemea swala La mbowe,mtahaibika nakuambia ukweli umekosea sana kuingilia hili swala na ukweli unaujua
 
Hakika....

Hakika.....

Hao jamaa kazi yao ni Kusababisha INSTABILITIES kwa nchi zinazoendelea.......

Lissu anatumikia maslahi yao.....
Lema anatumikia maslahi yao....

Wameisema RWANDA wee ,bado KAGAME yupo.....

Wameisema UGANDA wee,bado M7 yupo......

#KaziIendelee
Moja ya malengo yao makubwa kabisa ni kuona kunatokea machafuko yaani kinuke kisha waingie kwa neno kuleta amani.

Yaani kwa mfano, Mwanza kungenuka kisha kuwepo ghasia, vurugu, mauaji na uchafu mwingine.

Jambo la kukumbuka ni kwamba Tanzania ina watu ambao wamesoma haya yote.
 
Brother Pascal sijui nikitu gani kimekusibu hadi ukawa wa hivi. Anway nilikuwa shabiki yako na mfuatiliaji mkubwa wa Maandiko yako that's why nakushangaa.
Among the Journalist waliokuwa wamejijengeea Credibility hadi kufanya watu kuwa na hamu ya kufuatilia au kutamani siku ya kipindi unacho ongoza ifike haraka na muda wa kipindi chako uongezwe mlikuwa wachache sana mkiongozwa na wakilili Msomi General ulimwengu.
Kutokana na Mazingira magumu na ambayo sirafiki wenye misimamo na Taaluma zao pamoja na imani zao kwenye uandishi na kuhoji wameamua kujikalia zao kimya ilikutokupoteza imani waliojijengea kwa muda mrefu ndani ya jamii yetu na zaidi kwenye taaluma zao.

Sasa wewe Rafiki yangu kukaa kimya imeshindikana ukajaribu kujificha kwenye uzalendo ikabuma baada ya wewe kutangaza nia nabhatimae ukaambulia kura moja kama sijakosea. Na zaidi ya yote wenye mawazo huru wewe unaungana na watesi wao kuwa undermine inapotokea inapatikana ahuweni kwa sababu ya wenye mawazo huru unabadili upepo na kusema msikivu.

Sasa hebu twambie nini msimamo wako? Bahati nzuri hao unao wait a mabeberu jamii inawaelewa. Kumbuka hizi shule za kayumba zinasaidia sana kumfanya mtu alau aelewe hata sentesi moja ya kizungu na hii mitandao ya kijamii hata kwetu nyanchenche inatufikia tunaona na tunasikia.
 
Paschal Mayalla;

Hoja yako iko ktk sentensi hizi mbili;

1. CNN hawakutafuta taarifa sahihi toka "authoritative sources" juu ya sababu za kukamatwa kwa M/kiti wa CHADEMA Mh. Freeman A. Mbowe na polisi

2. CNN hawakupata taarifa sahihi kuhusu kukamatwa kwa Freeman Mbowe kutoka kile ambacho umekiita tena kama "reliable sources"

MASWALI KWAKO:

å Kwanza hebu tupe tofauti ya "authoritative sources" na "reliable sources"

å Pili, una habari kuwa kabla ya CNN na ALJAZEERA kutangaza kimataifa taarifa za kukamatwa kwa Mbowe, Tanpol kupitia msemaji wake Msiime walitoa official press release kueleza sababu ya kumakamata Mbowe kuwa ana tuhuma za ugaidi wa kuua viongozi wa serikali..?

å Tatu, ina maana wewe Paschal Mayalla huna taarifa kabisa kuwa M/,kiti CHADEMA taifa ndugu Freeman Mbowe alikamatwa usiku wa saa 8 hotelini akiwa amelala akiwa tayari kuhudhuria kikao halali cha ndani cha chama chake ili kujadili umuhimu wa Tanzania kuwa na katiba mpya ya wananchi kuanzia sasa?

å Hivi, Paschal Mayalla kwa akili ya kawaida tu isiyohitaji usomi wako huwezi kuelewa kabisa kuwa sababu ya kumkamata saa 8 za usiku ilikuwa ni "amri toka juu kwa RPC Mwanza" na ilikuwa ili kuzuia na kuhakikisha CHADEMA wasikutane kujadili mambo ya katiba?

å Hivi Mr Paschal Mayalla kwa akili ya kawaida tu, ni mtu gani mwenye akili timamu atashindwa kutambua kuwa huu ni mpango mahususi wa watawala?

å Na hivi Paschal Mayalla huoni kabisa kuwa hawa watawala ni wajinga na wapumbavu?

å Kwa sababu kama kweli Freeman Mbowe ni gaidi na wanajua hili muda mrefu kama walivyosema wenyewe, hebu jiulize ni kwanini sasa wakakosa akili na busara ya namna ya kumkamata ili kuzuia maswali kama haya kiasi cha kumkamata ktk mazingira yale...?

å Hivi Bwana Mayalla, Don't you really see that, all who planned that are desparate for something, stupid and ignorant...???

Sasa kwa taarifa hawa waliofanya hivi kwa kutumia akili hizo mbovu kabisa ndiyo viongozi wanaoongoza Tanzania hii na ndiyo hao wakabuni tozo za miamala ya simu, umeme na mafuta maana nchi yetu siyo tajiri tena...!!

å Changamoto kwako ni hii, kuwa, Kama Press Release ya polisi siyo Authoritative wala reliable sources toka serikalini, basi unaonaje sasa wewe utueleze mamlaka halali ambazo zingeweza kutupatia taarifa rasmi ni zipi iwapo polisi ambao ndiyo waliokamata siyo reliable wala authoritative sources...?

MWISHO:

##Wakati mwingine ndugu Paschal Mayalla, kama huna cha kuandika ktk jukwaa hili, basi ni vyema sana kuacha kuandika chochote cha kijinga na badala yake soma tu maandiko ya wengine wanayoandika...

## I know una haki ya kusema na kuandika lolote ukiitumia haki yako ya kikatiba ya kutoa maoni yako...

Lakini usisahau kuwa wewe ni verified member hapa na ni mwandishi wa habari unayejulikana na kila mtu. Kujaribu kuleta mambo yanayo lack authenticity hapa, ni kushusha reputation yako kwa viwango vya chini sana...

##Mathalani kwenye ishu ya kukamatwa Freeman Mbowe na polisi na sababu walizozitoa, hivi ni mtu gani mwenye akili timamu, mwerevu na anayefikiri vizuri anaweza kuamini maelezo ya polisi...?

##kwa ushahidi wa kimazingira, ni wazi kuwa the whole police arrest incident of Mr Freeman Mbowe is completely a framework from the government authorities kwa sababu wanazozijua wao...!!

## Tatizo lenu nyie wengi wa waandishi wa habari wa Tanzania ni upumbavu na ujinga mliobeba ktk bongo zenu ambazo huwasukuma kufanya shughuli zenu za uandishi wa habari kwa misukumo ya kisiasa na wanasiasa...

##Kwani nani asiyejua kuwa, wakati mwingine huwa mnaandaliwa habari na wanasiasa wenye nguvu na wanaopenda kusifiwa na kutukuzwa kisha wanawapa fedha kidogo na kuwamuuru mkarushe kwenye TV zenu au mkaandike kwenye magazeti yenu vivyo hivyo kama zilivyo na nyie foolishly na kwa kuuza utu wenu mnafanya vile...?

Nyie waandishi wa habari wa aina yako au Musiba, hamwezi kuelewa na lazima mshangae tu aina ya utoaji wa habari kwa waandishi na vyombo vya habari huru na makini kama CNN, Aljazeera, SkyNews, BBC, DW nk nk

##Serikali ya Tanzania chini ya CCM ya Samia Suluhu Hasssan inajibagaza na kujidhalilisha yenyewe kwa matendo yake maovu toka kwa watendaji wake wajinga na wapumbavu wakiwemo wengi wa maofisa wa vyombo vya dola hususani Polisi na TISS...

Hampaswi kumlaumu mtu wala CNN au Aljazera TV bali jilaumuni nyie wenyewe...

Kuna methali moja inasema;

"..Mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..."

Nyumba ya mwanamke huyu katika methali hiyo ni nchi yetu TANZANIA. Na mwanamke mpumbavu anayesemwa hapa ni Samia Suluhu Hassan na serikali yake yote chini ya Chama Cha Mapinduzi - CCM....
 
Back
Top Bottom