Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kwenye siasa

Tofauti ipo kiutendaji tu kati ya mtu mmoja hadi mtu mwingine ima ni mwanamke au mwanaume

Mifumo ya vyama vingi vya kisiasa barani Africa. automatically ni kulinda maslahi ya wanachama wake tu.hata uwe mbovu kiasi gani Kama upo kwenye system.hakuna kitakacho haribika

Kinachofata ni mwendelezo tu wa pale walipo ishia.
 
mkuu Pascal siku hizi mbona Kama unapoteana,mada za akili nyepesi siku hizi ndo unazileta,Mimi ninavyokujua toka zamani unakujaga na mada zenye logic na concrete!!siku hizi nn kimekusibu kiongozi!!
 
Yaani paskali unaacha kujadili sensitive issue kama nchi tuepukane vipi na matovo yasiyo na msingi kila uchao, unaleta mada za uchaguzi hata kabla ya semi year ya urais, kwa mtindo huu hatufiki popote.

Yaani kuna watu wanakuita mwanahabari nguli alafu more of your content zimejaa siasa za uteuzi, HOW😨?

Brother hali ni ngumu kweli ila siyo lazima uwe kiongozi, pambana huko huko kwenye tasnia.
 
Yani tufanye uchaguzi wa rais (Nafasi nyeti) , Ili kuleta ukombozi wa kijinsia? Ili iweje sasa, yani tuchague tu mwanamke Ili tufikie na kulipita lile adhimio la beijing sio?

Mtu atachaguliwa kulingana na sera za chama chake,pamoja na uwezo wake wa kuzitekeleza.

Nilikuwa sijui kama huwa una upumbavu kiasi hiki, umesoma nini Sasa? Au ndo kubadilika kuendana na beat la ngoma? Kuna ule uzi wako uliosema kwamba "kiongozi yoyote atakae gomea chanjo atakuwa ni msaliti " nilichukulia kama umeteleza tu, ila leo nasema rasmi kuwa wewe ni mpumbavu wa mwisho.

Acha kuendekeza njaa , wewe ni wa kujishusha hivyo kwa mwanamke?Aiseeeh wanaume wengine sijui mna nini tu?
Naunga mkono hoja..!
 
Mwanamke mwenyewe ni nani?.maana kama ni huyu aliyepo sasa mbona ni mapema sana kuanza kuyaongea hayo wakati ata robo ya mambo ya msingi kwa wananchi hajaanza kuyafanya.Ata hivyo kwa mtazamo wangu hii nchi bado sana kuanza kuwaza kuongozwa na mwanamke.labda kuanzia miaka ya 2080 uko ila sio zama hizi ambazo nchi bado inahitaji misingi imara ya kimfumo na maamuzi thabiti.Ingekua ni nchi yenye mifumo inayojiendesha ningewaza tofauti lakini kwa sasa ambavyo rais ni kila kitu bado sana aise.unless labda tuamue kupoteza tena hiyo miaka.Tuache unafiki.
 
Co mama yangu,,,but namchukulia kama mama yangu mzazi,,, namuheshimu pia.

Kwenye Swala la tozo hata mimi limenigusa sana babaa. Kwa upande wangu naamini ataweka sawa 2mpe muda. Ndiyo kwanzaa hajamariza mwaka. 2mpe nafac.
Ndomaana hata mimi nikasema, anatakiwa aitumie vizuri huuuda aliobaki nao. Afanye vizuri Ili ashawishi watu kumchagua tena,lakini swala la kusema eti achaguliwe kwakua ni mwanamke, aaaawapi.
 
Toka aniondolee dhulma ya loan board na kunipandisha daraja akili inaniambia Mama anafaa..

Miaka mitano iliyopita sikuwa na uhakika na nyongeza ya mshahara. Naamini Mwakani mambo yatakuwa vizuri. Cha msingi tumuombee afya,uhai,busara,hekima,utu na uzima kwa YEYE Mwenye Uwezo wa yote.
Utakuwa mwalimu wa serikali tuu wewe!!! ndomana siwezi somesha mtoto shulezenu mnadumaza akili za watoto. Rais akifanya kawajibu kidogo basi mnasiiifu hamfikirii kwa ukubwa
 
Wanabodi,

Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari.

Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, sasa katika hizo tatu, media ya Tanzania inafanya vizuri katika eneo la uhabarishaji, na kutoa burudani, lakini katika uelimishaji, bado tuna matatizo, na katika eneo la uchambuzi wa habari, news analysis ndio kabisa, media zetu nyingi hazina uwezo huo, kwasababu hazina watu wenye uwezo huo, matokeo yake, mtu akisema kitu, media zinachukua na kukirusha tuu hivyo hivyo kama kasuku, bila kukichakata na kukifanyia analysis.

Juzi kati hapa rais wetu Mhe. Mama kazuzungumzia need ya Watanzania kumchagua rais mwanamke mwaka 2025 kwa kusema tutamsimamisha Mwanamke, media zimelidaka kama lilivyo kikasuku kasuku na kuanza kulivurumisha, hivyo kuleta mjadala mkubwa kwenye media na mitandao ya jamii, mara kaanza kampeni mapema, mara kajiteua, mara ni ubaguzi wa kuwabagua wanaume, mara hivi mara vile, hivyo bandiko hili ni kuwasaidia kidogo, kuwafanyia a simple analysis ya alichokisema rais Samia.

Kwanza ni ombi kwenu Watanzania wenzangu, kwanza tuunge mkono msimamo wa rais wetu Samia kuwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2025, tuufanye, sio tuu ni zamu ya kuchagua mgombea mwanamke, bali tuifanye ndio zamu ya ukombozi rasmi wa mwanamke katika siasa, sio tuu tuchague rais mwanamke, bali tuchague wabunge na wadiwani wanawake kwa wingi na kuifikia ile 50/50 ya azimio la Beijing na hata kupita, ila kwenye urais, sio lazima ndio awe Mama Samia, anaweza kuwa yeye au mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa kwasababu mpangaji sio yeye, wala sio sisi, mpangaji na YEYE. Hivyo ikitokea, rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 aliyepangiwa na YEYE, ni yeye Mama Samia, then who are we kusema no, kama ni yeye aliyepangiwa, na YEYE, then ni yeye!.

Hivyo mimi naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwasabubu kiukweli kabisa, wanawake wana uwezo sana wa uongozi na wengine kuliko hata wanaume, ila siku zote, tumekuwa tukiwakandamiza kutokana na kutawaliwa na mfumo dume kwa miaka nenda miaka rudi, na mpaka Mungu alipoingilia kati. Kama Mungu asingeingilia kati na JPM akaendelea hadi 2025, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke, lakini baada ya Mungu kuingilia kati na Tanzania kwa mara ya kwanza tukapata rais mwanamke, na Mama Samia ameisha onyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza, then why not 2025 asiwe mwanamke sasa sio tena kwa kudra za Mwenyeenzi Mungu bali kwa chaguo la Mungu kwa Tanzania na kupata endorsement ya Watanzania kwenye sanduku la kura, kumchagua rais mwanamke na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Na hili likifanyika na likakamilika kikamilifu, uchaguzi wa 2025 tukapata 50/50 ya wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufuta viti maalum, vitakuwa havihitajiki tena, vikiendelea kubaki ni wastage of time, money and resources.

Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, Hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, Hivyo Hata Samia ni Mpango wa Mungu kwa Tanzania hadi 2025. Kama Samia ni mpaka wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema na sisi, kwasababu hata JPM. hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if ndivyo Mungu alivyopanga.

Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is shure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha lazima ni yeye, ni busara kwa rais wetu Samia, hili la ugombea wa 2025, akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na yale ya Kimungu tumuachie Mungu mwenyewe.

Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

Nenda ukanisome in between the lines, nilisema nini kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, katika mabandiko haya.

Ukiisha soma, kama una uwezo to read in between the lines, jibu utakuwa umelipata.

Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

2025 Twende na Mwanamke!.

Paskali
Heshima yako Pasco,wewe ni muona mbali nimeamini upo jikoni na hapa Huwa unakuja tu kutoa mlejesho ya nini mnaafkiana.
 
Huyu mama anapwaya sana kwenye kaliba ya uongozi wa Taifa. Tanzania ya leo imepungukiwa sana na watu wa nguvu; wanawake kama akina titi Mohammed au Sofia Kawawa au Tabitha Siwale hawapo tena katika medani hii.

Mama Samia amekuwa kila mara anaongelea kuhusu yeye kuwa mwanamke badala ya kutoa vision ya tanzania anayotaka kuacha. Ukinizingua, nitakuzingia, sitakukemea ila nitatumia kalamu yangu, vijigazeti, yaani anongea vitu vya hovyo kabisa!

Mungu amlinde mama dhid ya wabaya
 
Back
Top Bottom