Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Swala la Magufuli kwenye hii mada linatoka wapi?

Hakuna anaemchukia huyo mama yako (kama kweli wewe ni mwanae), amepata nafasi hiyo kikatiba aitumie vizuri Ili awashawishi wamchague tena 2025, aitumie vizuri Ili watanzania wengi wasimchukie kama unavyodai kwenye comment yako.

Lakini swala la kusema achaguliwe tu,eti kwasababu ni mwanamke (mama yako) hilo sio sawa kabisa.

Mkuu,umesahau kuweka namba na jina lako chini na comment yako,huwezi jua huenda akakauona.
 
Hajamaliza mwaka kelele nyiingi. Kuna waliokereka hawakutaka awe rais uyu mama kutokana na imani yake na uzanzibari. Lakini wapo wakristo wanamkubali na wanampenda sana. Wabarikiwe
Wewe hujaona sababu nyingine zinazofanya achukiwe tofauti na Dini yake?
 
AU TUNAONEKANA MAZEZETA NN.???

MAANA HAIWEZEKANI KBS RAISI WA NCHI AONGEE UTUMBO UTUMBO TU KAMA ULE....

ISHU NI KUMCHAGUA RAISI MWENYE UWEZO WA KUONGOZA NCHI HII YENYE DHIKI KUBWA , NA KUIFIKISHA KTK ENEO INAYOSTAHILI KUWEPO.

Watu kama ninyi ipo cku mukuchukuliwa na kuswekwa ndani,,, alafu muanze kumlaumu mama anawaonea mara oh katili. Ushauri wangu,, Chunga maneno yako mkuu yacje kukugarimu.
 
Vyama visimamishe wagombea ikiwemo wanawake. Wapiga kura watachagua vile itakavyowapendeza.
Pamoja na hilo, ndugu mleta mada bado unayo nafasi ya kuendelea kuwapigia kampeni wanawake, lakini maamuzi ya mwisho yatafanywa na mpiga kura.
Si vema, si busara na haiwezekani kutuwekea shinikizo la lazima eti vyama vyote visimamishe wagombea wa jinsia moja.
 
Swala la Magufuli kwenye hii mada linatoka wapi?

Hakuna anaemchukia huyo mama yako (kama kweli wewe ni mwanae), amepata nafasi hiyo kikatiba aitumie vizuri Ili awashawishi wamchague tena 2025, aitumie vizuri Ili watanzania wengi wasimchukie kama unavyodai kwenye comment yako.

Lakini swala la kusema achaguliwe tu,eti kwasababu ni mwanamke (mama yako) hilo sio sawa kabisa.

Mkuu,umesahau kuweka namba na jina lako chini na comment yako,huwezi jua huenda akakauona.

Co mama yangu,,,but namchukulia kama mama yangu mzazi,,, namuheshimu pia.

Kwenye Swala la tozo hata mimi limenigusa sana babaa. Kwa upande wangu naamini ataweka sawa 2mpe muda. Ndiyo kwanzaa hajamariza mwaka. 2mpe nafac.
 
Amefanya vizuri hapo, ila shida ni moja watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo. Kwa data za karibuni ni takribani watanzania milioni 40. Hawa Leo karibu wote wanalia kilio kikubwa kutokana na kupanda gharama za pembejeo mra mbili ya awali.
Alipaswa kuweka ruzuku kwenye pembejeo ili hawa watanzania mamilioni waache kulia.
Gunia la mahindi 25,000, alafu mbolea sasa hivi imefikia 120,000
Narudia tena, mama Samia alipaswa kuweka ruzuku kwenye pembejeo. Mwaka huu wengi watashindwa kabisaa kulima.
Ni kweli mkuu, Mimi pia licha ya Ajira nimewekeza kwenya kilimo. Nina shehena ya mahindi nimehifadhi kwenye mifuko nasubiri Bei ipande. Serikali haina budi pia lutafuta masoko ya uhakika ya mazao.
 
Wanabodi,

Kati ya maeneo magumu sana kwenye tasnia ya habari ambayo kwa sisi Tanzania tumelikosa, tunaendelea kulikosa, na kama hawatajitokeza watu wenye uwezo wa kulifanya, tutaendelea kulikosa, ni eneo la "news analysis" uchambuzi wa habari.

Kazi kuu za traditional media ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, sasa katika hizo tatu, media ya Tanzania inafanya vizuri katika eneo la uhabarishaji, na kutoa burudani, lakini katika uelimishaji, bado tuna matatizo, na katika eneo la uchambuzi wa habari, news analysis ndio kabisa, media zetu nyingi hazina uwezo huo, kwasababu hazina watu wenye uwezo huo, matokeo yake, mtu akisema kitu, media zinachukua na kukirusha tuu hivyo hivyo kama kasuku, bila kukichakata na kukifanyia analysis.

Juzi kati hapa rais wetu Mhe. Mama kazuzungumzia need ya Watanzania kumchagua rais mwanamke mwaka 2025 kwa kusema tutamsimamisha Mwanamke, media zimelidaka kama lilivyo kikasuku kasuku na kuanza kulivurumisha, hivyo kuleta mjadala mkubwa kwenye media na mitandao ya jamii, mara kaanza kampeni mapema, mara kajiteua, mara ni ubaguzi wa kuwabagua wanaume, mara hivi mara vile, hivyo bandiko hili ni kuwasaidia kidogo, kuwafanyia a simple analysis ya alichokisema rais Samia.

Kwanza ni ombi kwenu Watanzania wenzangu, kwanza tuunge mkono msimamo wa rais wetu Samia kuwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa 2025, tuufanye, sio tuu ni zamu ya kuchagua mgombea mwanamke, bali tuifanye ndio zamu ya ukombozi rasmi wa mwanamke katika siasa, sio tuu tuchague rais mwanamke, bali tuchague wabunge na wadiwani wanawake kwa wingi na kuifikia ile 50/50 ya azimio la Beijing na hata kupita, ila kwenye urais, sio lazima ndio awe Mama Samia, anaweza kuwa yeye au mwanamke mwingine yoyote aliyepangiwa kwasababu mpangaji sio yeye, wala sio sisi, mpangaji na YEYE. Hivyo ikitokea, rais wa Tanzania kwa mwaka 2025 aliyepangiwa na YEYE, ni yeye Mama Samia, then who are we kusema no, kama ni yeye aliyepangiwa, na YEYE, then ni yeye!.

Hivyo mimi naunga mkono hoja ya rais mwanamke ile 2025, kwasabubu kiukweli kabisa, wanawake wana uwezo sana wa uongozi na wengine kuliko hata wanaume, ila siku zote, tumekuwa tukiwakandamiza kutokana na kutawaliwa na mfumo dume kwa miaka nenda miaka rudi, na mpaka Mungu alipoingilia kati. Kama Mungu asingeingilia kati na JPM akaendelea hadi 2025, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke, lakini baada ya Mungu kuingilia kati na Tanzania kwa mara ya kwanza tukapata rais mwanamke, na Mama Samia ameisha onyesha na kuthibitisha pasipo shaka kuwa wanawake wanaweza, then why not 2025 asiwe mwanamke sasa sio tena kwa kudra za Mwenyeenzi Mungu bali kwa chaguo la Mungu kwa Tanzania na kupata endorsement ya Watanzania kwenye sanduku la kura, kumchagua rais mwanamke na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Na hili likifanyika na likakamilika kikamilifu, uchaguzi wa 2025 tukapata 50/50 ya wabunge na madiwani wanawake wa kutosha. Kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufuta viti maalum, vitakuwa havihitajiki tena, vikiendelea kubaki ni wastage of time, money and resources.

Marais wa Nchi Hupangwa na Mungu, Hata JPM alikuwa ni Chaguo la Mungu kwa Tanzanzia, Hivyo Hata Samia ni Mpango wa Mungu kwa Tanzania hadi 2025. Kama Samia ni mpaka wa Mungu kwa Tanzania 2025 -2030, then Mungu atasema na sisi, kwasababu hata JPM. hakuna aliyejua Mungu alipanga nini, lakini kwa utaratibu wa CCM, urais huu wa Mama Samia ulioletwa kwa kudra za Mwenyezi Mungu, hii ni awamu yake ya kwanza, hivyo kila mtu anajua uchaguzi wa 2025 ndio awamu yake ya pili ya Mama Samia but only if ndivyo Mungu alivyopanga.

Kwa vile hili ya yeye kugombea 2025, rais Samia mwenyewe aliisha liweka vizuri kabisa ile siku anahojiwa na Salim Kikeke wa BBC, baada ya kuhojiwa kama atagombea urais 2025, rais Samia alijibu vizuri kabisa kuwa "kwa sasa tufanye kwanza kazi, ya 2025 tumwachie Mungu maana no one is shure kufika 2025", hivyo hata rais Samia aliposema 2025 tutamchagua mwanamke, hajamaanisha lazima ni yeye, ni busara kwa rais wetu Samia, hili la ugombea wa 2025, akaendelea na msimamo wake ule ule wa kwenye BBC kuwa ya 2025 tumuachie Mungu. Kwa sasa, rais aendelee ku deal na haya ya Kaizari, kwa kuchapa kazi na kazi iendelee na yale ya Kimungu tumuachie Mungu mwenyewe.

Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

Nenda ukanisome in between the lines, nilisema nini kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, katika mabandiko haya.


Ukiisha soma, kama una uwezo to read in between the lines, jibu utakuwa umelipata.

Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

2025 Twende na Mwanamke!.

Paskali
Umenifurahisha namna ulivyokwepa kufanya analysis ya "vigazeti kusema hagombei". Haha ha haaaa!
 
Back
Top Bottom