Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Huyu mama anapwaya sana kwenye kaliba ya uongozi wa Taifa. Tanzania ya leo imepungukiwa sana na watu wa nguvu; wanawake kama akina titi Mohammed au Sofia Kawawa au Tabitha Siwale hawapo tena katika medani hii.

Mama Samia amekuwa kila mara anaongelea kuhusu yeye kuwa mwanamke badala ya kutoa vision ya tanzania anayotaka kuacha. Ukinizingua, nitakuzingia, sitakukemea ila nitatumia kalamu yangu, vijigazeti, yaani anongea vitu vya hovyo kabisa!
 
Zamu ya Magufuli imeshapita hata mukimtaja harudii, tunashukuru kwa mazuri aliyoyafanya.

Sasa ni wakati wa kujivunia na Mama saamiah suluh hassan. Msiempenda mutamkubali tu.

Nimefurai Rwegamalila kumuachia huru, soon na Muheshimiwa Mbowe atamuachia huru, mama ana huruma mno, hataki dhuluma wala uonevu.

Munaomchukia uyu mama mna sababu zenu co bure. Na wengine nimejionea wamejikita kwenye udini na ubaguzi. Akili za kipumbafu haswaa.

Mama ubarikiwe sana
Mwinyi ubarikiwe sana
Majaliwa ubarikie sana
 
Toka aniondolee dhulma ya loan board na kunipandisha daraja akili inaniambia Mama anafaa..

Miaka mitano iliyopita sikuwa na uhakika na nyongeza ya mshahara. Naamini Mwakani mambo yatakuwa vizuri. Cha msingi tumuombee afya,uhai,busara,hekima,utu na uzima kwa YEYE Mwenye Uwezo wa yote.
Nyongeza mshahara iwe haki na sio hisani ya mtu mmoja. Una hakika gani akishachaguliwa 2025 hamtakaa tena 6 years kupata nyongeza.

AMKA ww
 
Yani tufanye uchaguzi wa rais (Nafasi nyeti) , Ili kuleta ukombozi wa kijinsia? Ili iweje sasa, yani tuchague tu mwanamke Ili tufikie na kulipita lile adhimio la beijing sio?

Mtu atachaguliwa kulingana na sera za chama chake,pamoja na uwezo wake wa kuzitekeleza.

Nilikuwa sijui kama huwa una upumbavu kiasi hiki, umesoma nini Sasa? Au ndo kubadilika kuendana na beat la ngoma? Kuna ule uzi wako uliosema kwamba "kiongozi yoyote atakae gomea chanjo atakuwa ni msaliti " nilichukulia kama umeteleza tu, ila leo nasema rasmi kuwa wewe ni mpumbavu wa mwisho.

Acha kuendekeza njaa , wewe ni wa kujishusha hivyo kwa mwanamke?Aiseeeh wanaume wengine sijui mna nini tu?
 
Amefanya vizuri hapo, ila shida ni moja watanzania wengi wamejiajiri kwenye kilimo. Kwa data za karibuni ni takribani watanzania milioni 40. Hawa Leo karibu wote wanalia kilio kikubwa kutokana na kupanda gharama za pembejeo mra mbili ya awali...
Graduates nao vipi ambao hawana ajira? Kuongeza tozo kunasaidia nini
 
Tutoe na mifano kidogo ya viongozi akina mama.

Makinda na Ndugai. Najua zama tofauti

Suala ni utendaji tu, uanamke na uanamme sio sifa tosheleza za uongozi
Kama uanamke na uanaume sio sifa toshelezi za uongozi, kwanini mleta nada anasema 2025 tuchague mwanamke?

Alitakiwa kusema tuchague kiongozi anaefaa, au we unaona yuko sawa?

Lakini tukizingatia swala la utendaji Samia anaonekana kufeli, labda ndomaana uliyemqoute kasema wanawake hawawezi, labda ngoja tuone hiyo miaka mnne ijayo.
 
Back
Top Bottom