Chee4
Member
- May 17, 2021
- 35
- 125
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa chanjo ni salama na kamwe hawezi kuwaletea chanjo ambayo ina madhara kwa kuwa yeye ni Kiongozi Mkuu wa Nchi anayejali afya za wananchi wake.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akipata chanjo ya kujikinga na ugonjwa na Corona, ambapo amesema yeye ni Mkuu wa nchi lakini pia Mama, Mke na Bibi anayetegemewa hivyo haweki rehani maisha yake na maisha ya Watanzania kama chanjo ingekua si salama.
"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni ya wataalam na wataalam wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa' - Amesema Rais Samia
EWE Mtanzania msisikilize maneno ya akina Kibwetele ambao si wataalamu wa Afya, na kuwaamini kuhusiana na chanjo, Hakuna Serikali Duniani ambayo ipo kwa ajili ya kuwaua wananchi wake sababu ya chanjo au sababu nyingine.
Chanjo Ni Salama Ila Ni Hiari, Na Corona Ipo na Wengi Wamekufa
JikingeNaUwakingeWengine