#COVID19 Watanzania msikilizeni Rais Samia kuhusu chanjo

Chee4

Member
May 17, 2021
35
125
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa chanjo ni salama na kamwe hawezi kuwaletea chanjo ambayo ina madhara kwa kuwa yeye ni Kiongozi Mkuu wa Nchi anayejali afya za wananchi wake.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akipata chanjo ya kujikinga na ugonjwa na Corona, ambapo amesema yeye ni Mkuu wa nchi lakini pia Mama, Mke na Bibi anayetegemewa hivyo haweki rehani maisha yake na maisha ya Watanzania kama chanjo ingekua si salama.

"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni ya wataalam na wataalam wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa' - Amesema Rais Samia

EWE Mtanzania msisikilize maneno ya akina Kibwetele ambao si wataalamu wa Afya, na kuwaamini kuhusiana na chanjo, Hakuna Serikali Duniani ambayo ipo kwa ajili ya kuwaua wananchi wake sababu ya chanjo au sababu nyingine.

Chanjo Ni Salama Ila Ni Hiari, Na Corona Ipo na Wengi Wamekufa

JikingeNaUwakingeWengine
 
Hakuna Serikali Duniani ambayo ipo kwa ajili ya kuwaua wananchi wake sababu ya chanjo au sababu nyingine.

Hiyo ni kauli ya ukweli lakini Serikali sio Mungu inaweza kufanya makosa ya kibinadamu, shida ni hii; hatuna vyombo bora vya kupima ubora wa hii chanjo ikizingatiwa kwamba hapo kabla kulikuwepo na tetesi mbaya karibu duniani pote juu ya "Corona na chanjo itakayotengenezwa", (the depopulation program) mbaya zaidi kuna chanjo feki zilitengenezwa huko (Ulaya au America?) na kupelekwa India ambako zilileta madhara ya vifo nk, kwa watoto.
 
Wacha wayaone wenyewe Mtu mwenye vyeo na maslahi mengi serikalini kam dr Gwajima anamtemea mate yule zumugulu Jiwe. Wewe ni nani wa kumtetea kwamba alikuwa mzuri. He was just another Kibwetele in Afrika.
 
Kwanini hii form imeandikwa kwa lugha ya kibeberu wakati lugha yetu ya Taifa ni kiswahili? Ningumu sana kuchoma hii kitu kwasabu ya hii lugha waliyotumia kwenye hii form mm sielewi

44FC8DEA-429E-4994-9C93-5138A2C7F3FB.jpeg
 
Kujali malalamiko ya watu ya makato kashindwa ndo iwe usalama chanjo?
 
Back
Top Bottom