Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Kwamba mifano ya haja ni namna alivyochaguliwa Mh Kikwete na Mh Shibuda.

Ninaendelea kuamini kuwa kitengo cha Propaganda cha CCM kimeishiwa ubunifu wa kisiasa kushawishi wapiga kura.

Enyi wana CCM, endeleeni kutapa tapa bila kujua nini mseme ili kuchokoza mijadala ya sifa za viongozi tunaowataka kwenye jamii yetu ya karne hii ya 21.

UKAWA utaendelea kuwa mwiba unaoichoma CCM ndani ya ngozi yake.

Haya maigizo ya chagueni viongozi, msichague vyama ni kiashiria kingine kinachodhihiri namna CCM inavyomfia JK mikononi.

Rest in Hell CCM>

Hiyo ni mifano miwili tu niliyokuwekea ili kudhihirisha hoja yangu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Tanzania hakichaguliwi chama anachaguliwa kiongozi. Hata huko UKAWA mtachaguwa chama? au kiongozi? UKAWA si chama. Fikiri.
 
Udini naweza kuueleza kama msukumo wa kifikra na kimatendo pale ambapo mtu, jamii, kikundi cha watu au mtu mmoja kila alinenalo au alitendalo au aliamuwalo dhidi ya mtu au kikundi kingine, dini ya yule mtu au hicho kikundi inakuwa ndiyo kigezo cha maamuzi.

Udini hauangalii kwanza ubora au udhaifu wa mtu katika maamuzi yoyote yale bali hutazama kwanza dini ya mhusika. Mathalani mtu aliye wa imani ya dini moja hata akifanya kosa atatetewa, atasaidiwa au atatakaswa. Lakini pia yule mwenye imani tofauti ya kidini, kosa lake litakuzwa, litahusishwa na dini yake.

Pale maamuzi yoyote yale yanafanywa, kwanza huangaliwa dini ya mtu, iwe kwa uzuri au ubaya ni udini. Ndiyo maana nilisema mpo wengi lakini wewe ulinisikitisha zaidi kwa sababu ninaelewa una ufahamu wa kutosha.

Hata pale inapotokea orodha ya majambazi waliokamatwa, unaanza kuhesabu wangapi ni wakristo na wangapi ni waislam, ujue kuwa huo ni udini. Hata uteuzi wa viongozi unapofanywa, unapoanza kuangalia walioteuliwa wana majina ya kikristo au kiislam badala ya kuangalia sifa zao, huo ni udini.

Hata unaposema huyo padre wenu hawezi kuwa Rais, huo ni udini. Maana unatumia neno 'padre' kuamsha hisia za utengano kwa misingi ya imani ya dini ya mhusika. Hata wale wanaosema kuwa safari hii ni zamu ya wakristo, huo pia ni udini.

"Udini" ndiyo nini?
 
Siipigii kura yoyote Katiba inayopendekezwa si kwa sababu hiyo uliyoiweka bali ni kwa sababu haijatambuwa kiuwazi uwepo wa Mahakama ya Kadhi Tanzania. Kumbuka hilo.

Kwa hiyo hakuna atakaeipata kura yangu, si wa ndiyo wala si wa hapana.

Naheshimu uhuru wako, huoni usipopiga kura hujatekeleza wajibu wako na huitendei haki nchi yako? Ni bora upige kura ya hapana ili bunge likae upya na hiyo mahakama ya kadhi iletwe na hoja zenye nguvu zaidi na ushawishi kutoka kwa watu wengine,na wala sio akina Shehe Jongo wanaolia Nyerere kutukanwa kwa ukweli kusemwa na wala sio kulilia mahakama ya kadhi kukosekana. Iwapo watu wote watakaoona mahitaji yao hayapo wakaacha kupiga kura na ikapita, huoni hawatopata tena wakitakacho. Kupiga kura ya hapana ni kama kukata rufaa ili uende ngazi ya mbele ambapo unatarajia kupata kile unachokitaka. Wote tunajua katiba haikuwa na maridhiano na kwa kiasi kikubwa makundi mengi ya jamii hayajapata yanachokitaka au matakwa ya jamii yametajwa kwa ghiliba. Nadhani ni bora sisi wote tushirikiane kupiga kura ya hapana, tuchague viongozi bora na sio chama kama ulivyoshauri, watakaotokana na matakwa ya watu ambao watasimamia mahitaji ya umma ili bunge likikaa tena litakuwa na sura mpya, kwa kiasi kikubwa hili kundi la wanasiasa wahuni waliojazana kwenye bunge la katiba watakuwa wametoka na sheria ya BMK itarekebishwa vizuri zaidi na tutapata katiba mpya na bora. Nadhani wewe ni mmoja ya watu wanaowashangaa na kuwabeza wapinzani kwa kususia mijadala bungeni pindi wanapoona matakwa yao au ya wananchi kama wanavyojinadi yakikiukwa. Sasa wewe leo unaposusa kupiga kura huoni ni yale yale ya nyani haoni .......?

Kwa uzi wako huu uliouleta leo, unataka kusema mmebadili ule msemo wa ccm itatawala milele? (just a joke anyway)
 
Wonders never end,2105 imekuja kivyake,kwa mara ya kwanza Faiza ametoa point inayoeleweka,sijui wamamkera nini?au kuzikosa za escrow ? au mahakama ya kadhi au kikao cha Zanzibar,najaribu kukisia kwani siye Faiza Foxy tunayemjua,huyu ana busara zaidi.
 
Tumeyajua,na tumejua ni kwa nini wenye chama hawakumtaka,THEY WERE RIGHT!!!!!!HAKUTAKIWA
Mfano hai ni mwaka 1995 wakati Kikwete alipowania kuwa Rais kwa mara ya kwanza, hakuna asiyejuwa kuwa alishinda ndani ya chama lakini wenye chama hawakutaka, matokeo unayajuwa.
 
Kiukweli hata leo nimechangia uzi wako kwa bahati mbaya tu kwa sababu huwa sioni point kwenye mijadara unayoanzisha tofauti na propaganda za kuwagawa wasioelewa hasa za Udini,Ukanda na Ukabira.Kwa kifupi tu huwa nakudharau sana kwa sbb kichwa chako kimefugia nywele tu na ndio mana umekifunika nahilo tambala jeusi, lakini ndani kiko wazi.Na hivi sichangii tena kwa leo Uzi huu

= mijadala
= Ukabila
= tambara

Haya, uwe na siku njema.
 
Kwenye soccer hii wanaiita"play with handbrake". Unapoona mpinzani wako hatabiriki cheza kwa tahadhari.
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Well said!
 
Udini naweza kuueleza kama msukumo wa kifikra na kimatendo pale ambapo mtu, jamii, kikundi cha watu au mtu mmoja kila alinenalo au alitendalo au aliamuwalo dhidi ya mtu au kikundi kingine, dini ya yule mtu au hicho kikundi inakuwa ndiyo kigezo cha maamuzi.

Udini hauangalii kwanza ubora au udhaifu wa mtu katika maamuzi yoyote yale bali hutazama kwanza dini ya mhusika. Mathalani mtu aliye wa imani ya dini moja hata akifanya kosa atatetewa, atasaidiwa au atatakaswa. Lakini pia yule mwenye imani tofauti ya kidini, kosa lake litakuzwa, litahusishwa na dini yake.

Pale maamuzi yoyote yale yanafanywa, kwanza huangaliwa dini ya mtu, iwe kwa uzuri au ubaya ni udini. Ndiyo maana nilisema mpo wengi lakini wewe ulinisikitisha zaidi kwa sababu ninaelewa una ufahamu wa kutosha.

Hata pale inapotokea orodha ya majambazi waliokamatwa, unaanza kuhesabu wangapi ni wakristo na wangapi ni waislam, ujue kuwa huo ni udini. Hata uteuzi wa viongozi unapofanywa, unapoanza kuangalia walioteuliwa wana majina ya kikristo au kiislam badala ya kuangalia sifa zao, huo ni udini.

Hata unaposema huyo padre wenu hawezi kuwa Rais, huo ni udini. Maana unatumia neno 'padre' kuamsha hisia za utengano kwa misingi ya imani ya dini ya mhusika. Hata wale wanaosema kuwa safari hii ni zamu ya wakristo, huo pia ni udini.

Dini maana yake ni njia, kama ulikuwa huelewi, sasa kusema mimi nna "udini" ni kama kuniambia mimi nna njia yangu nnayoifata, wakati huo si ukweli. Mimi nnafata njia inayofundishwa na Uislam, wewe nnauhakika unafata njia inayofundishwa na Ukristo. Na kama hufati njia inayofundishwa na Ukristo wala Uislaam basi lazima una njia yako unayoifata na kama hiyo njia ni yako peke yako basi huo ndiyo "udini".

Kumwita Slaa kuwa padri huo ndiyo ukweli, kama ukweli ndiyo udini kwa maana yako basi utaniona ni mdini sana kwani sisiti kusema ukweli. Siwezi leo hii nikamwita padri Slaa kuwa ni Imamu Slaa. Ntakuwa ni muongo na ntakuwa namfanyia kejeli isiyo na msingi.

Ngao yenu ya kijinga ni hiyo yakumpachika mtu jina la udini ili tu mtimize matakwa yenu ya kupindisha mijadala. Ikiwa kwa muono wako huo finyu unaona mimi ni mdini basi kumbuka kuwa utaniona ni mdini sana, kwa sababu kila maamuzi yangu kwanza na pili na tatu huyafanya kwa Uislam wangu. Wewe una haki ya kufata njia aka dini yako uipendayo na au udini uupendao.

Kum depict mtu kuwa ni mdini ni udini mkubwa sana kuliko hizo maana finyu ulizoelezea. Ikiwa njia yako ya kuubadili mjadala ni kutumia neno udini basi hujafanikiwa, mjadala ndiyo unanoga.

Jee, wewe utachaguwa kiongozi au chama?
 
katiba tuliyonayo inatutaka tuangalie vyote viwili; wagombea na vyama vyao kwa wakati mmoja. Kwenye uchaguzi ni kweli wanaokuja kwetu ni wagombea na hujiombea kura wao kama wagombea. Hata hivyo, wagombea hao ni lazima kwanza wawe wamepitshwa na vyama vyao; pili wakishinda ni lazima waendelee kuvitumikia vyama vyao kwani vina nguvu juu yao zaidi ya wananchi waliowachagua. Vyama vinaweza kuwafukuza katika vyeo walivyogombea kwa kuwafukuza uanachama. Hapa ndo mkanganyiko wa kikatiba ulipo.

Ungetarajia kuwa; kwa kuwa mgombea ndiye anayekuja kuomba kura baada ya kupitishwa na Chama, akishapewa kura awajibike kwa waliompa kura. Hali haiko hivyo. Baada ya kushinda Mgombea anatakiwa awajibike kwa Chama kilichompa fursa ya kwenda kugombea. Nje nje inaonekana kuwa mgombea anatakiwa awajibike kwa wananchi na chama chake - lakini ukweli ni kuwa mgombea aliyeshinda sasa anatakiwa awajibike kwa chama kilichompa fursa ya kugombea. Hapa ni kuwa Chama kinajificha nyuma ya Mgombea wakati wa uchaguzi - akishashinda chama kinampora mgombea kutoka kwa waliomchagua na kummiliki chenyewe. Hali hii inaleta shida sana na kuwafanya wagombea wawe mateka wa vyama vyao badala ya kuwa chini ya wananchi waliowachagua.

Kwa mwenendo huu hata kwenye uchaguzi kimsingi inatakiwa tuvipigie kura vyama moja kwa moja. Wagombea wawe wanakuja kuviombea kura vyama vyao. Hali ndivyo ilivyo. Kusema umpigie kura mgombea kwa sasa ni bure - unadanganywa tu kuwa unayepigia kura ni mgombea. Ukweli unakipigia chama ila chama kinajificha nyuma ya mgombea. Kwa mfano, leo hii akija Mgombea X ukampigia kura; kimsingi umekipigia chama chake - baada ya huyo mgombea kuingia madarakani Chama chake ndo kinashika hatamu. Yaani bado tuko kwenye mfumo wa chama kushika hatamu za uongozi. Huu ndo mchanyato na kizungumkuti tulichonacho kwenye katiba yetu na hiyo pendekezwa ya CCM.

Ukitaka tuingie kwenye mfumo wa kuchagua viongozi; ni lazima uwe na mfumo ule unaoruhusu mgombea kuhama chama bila kupoteza haki yake ya kugombea au bila kupoteza nafasi ya uongozi aliyonayo baada ya kushinda. La pili inatakiwa uwe na utaratibu wa wananchi kumwajibisha mtu wao ili anapopotea njia wananchi waliomchagua wawe na uwezo wa kumwajibisha moja kwa moja. Kwa mfumo kama huu wagombea binafsi huwezi kuwazuia. Hata viongozi walioko madarakani wanakuwa na uwezo wa kuhama vyama vyao bila kupoteza nafasi zao. Mfumo kama huo uko kwa majirani zetu hapo Malawi.
 
Utaelewaje wakati umefaulu darasa la saba hujui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Form 6 English course nenda.

Ahsante kwa ushauri wako, sasa nimekulelewa lakini kile Kingereza chako huko juu naona kina walakin wa kueleweka.

Si unaona ukitumia Kiswahili tunaelewana vizuri kabisa.

Jee, wewe utachaguwa kiongozi au chama?
 
Nimekwambia Kenya watu hawachagui Chama bali wanachagua Watu na wanawafwata na ndio maana kuna vurugu, sisi kwetu hatuchagui Mtu bali tunachagua Chama na ndio maana (mpaka sasa) hatuna vurugu!
Sasa hilo la Ukabila na CHADEMA sikuelewi unamaanisha nini embu fafanua kwa maana ni geni kwangu!

Kumbe wewe ni Mkenya? sasa usituletee siasa za Kinyang'au hapa. Nyie mara tu mnachinjana kama kuku.
 
FaizaFoxy huwezi kutenganisha mwanachama na chama, chama ndio chenye sera na mwanachama ni lazima afuate sera, hawezi kwenda kinyume na miongozo ya chama, Mfano mzuri sera za CCM ni serikali mbili, ndio maana katika bunge la katiba wana CCM wote walisimamia hilo na wewe ukiwemo, huwezi kwenda kinyume na chama kinavyotaka uende, kikisema wauza unga hawatakiwi kuguswa itakuwa hivyo, mgombea yeyote wa CCM hafai
 
Naheshimu uhuru wako, huoni usipopiga kura hujatekeleza wajibu wako na huitendei haki nchi yako? Ni bora upige kura ya hapana ili bunge likae upya na hiyo mahakama ya kadhi iletwe na hoja zenye nguvu zaidi na ushawishi kutoka kwa watu wengine,na wala sio akina Shehe Jongo wanaolia Nyerere kutukanwa kwa ukweli kusemwa na wala sio kulilia mahakama ya kadhi kukosekana. Iwapo watu wote watakaoona mahitaji yao hayapo wakaacha kupiga kura na ikapita, huoni hawatopata tena wakitakacho. Kupiga kura ya hapana ni kama kukata rufaa ili uende ngazi ya mbele ambapo unatarajia kupata kile unachokitaka. Wote tunajua katiba haikuwa na maridhiano na kwa kiasi kikubwa makundi mengi ya jamii hayajapata yanachokitaka au matakwa ya jamii yametajwa kwa ghiliba. Nadhani ni bora sisi wote tushirikiane kupiga kura ya hapana, tuchague viongozi bora na sio chama kama ulivyoshauri, watakaotokana na matakwa ya watu ambao watasimamia mahitaji ya umma ili bunge likikaa tena litakuwa na sura mpya, kwa kiasi kikubwa hili kundi la wanasiasa wahuni waliojazana kwenye bunge la katiba watakuwa wametoka na sheria ya BMK itarekebishwa vizuri zaidi na tutapata katiba mpya na bora. Nadhani wewe ni mmoja ya watu wanaowashangaa na kuwabeza wapinzani kwa kususia mijadala bungeni pindi wanapoona matakwa yao au ya wananchi kama wanavyojinadi yakikiukwa. Sasa wewe leo unaposusa kupiga kura huoni ni yale yale ya nyani haoni .......?

Kwa uzi wako huu uliouleta leo, unataka kusema mmebadili ule msemo wa ccm itatawala milele? (just a joke anyway)

Hapa nnaongea kama mwana CCM na si CCM. CCM wana njia zao za kufikisha ujumbe wao na sera zao. Kumbuka hilo kabla ya yote.

Hapa nakumbushia ukweli ulivyo, sasa wewe ni haki yako, kunyoa ua kusuka. Uko huru.

Jee, wewe utachaguwa kiongozi au chama?
 
Back
Top Bottom