Katika mambo yote sina ugomvi na binti wewe, hata katika kuitetea CCM au Rais Jakaya kikwete, maana ndiyo mapenzi yako.
Mahali pekee ambapo huwa unaudhi kupindukia ni udini, hasa pale anapotaka kila kitu tuongelee kwa mtazamo wa uislam na ukristo. Hupo pekee, wapo na wengine. Hawa wengine hawanikeri sana maana kadiri ya maandiko yao tu unajua kuwa huyu upeo wake ni mdogo au hana kabisa.
Kwenye hoja yako ya kutaka achaguliwe mtu na siyo chama, nakubaliana nawe kiasi lakini natofautiana nawe zaidi.
Nakubaliana nawe kwenye ngazi za chini, kama vile vijiji lakini unapokuja kwenye ngazi ya Taifa ni muhimu pia kutazama sera za chama, umadhubuti wa chama katika kusimamia maamuzi, kupiga vita rushwa na ubunifu wa chama katika kuandaa sera zinazotekelezeka kutokana na ubunifu wa mipango iliyopo.
Nchi kama Singapore imefanikiwa sana kiuongozi, kiutawala na kiuchumi kwa sababu wao mfumo wao ni wa kuchagua chama, na baada ya hapo chama kilichoshinda humchagua Rais baada ya kupitia mchakato mgumu na wa kina. Kuna wakati chama kilichokuwa kimeshinda kilitamka wazi kuwa hakikuwa na mwanachama ndani ya chama chao aliyewathibitishia kuwa ana uwezo wa kutimiza ambayo chama kiliwaahidi wapiga kura. Chama kilimwomba mfanyabiashara awe mwanachama, na kisha kikamkabidhi madaraka ya Urais. Singapore wanasema, siyo rahisi mwananchi wa kule Muze (Rukwa) au Nakapanya (Ruvuma) kufahamu kwa uhakika kabisa kama Kikwete ana uwezo wa kuwa Rais bora au hapana, wao ndani ya chama ndiyo wanaojua.
Utawala wa CCM umetupa fundisho kubwa kuwa ili tupate mabadiliko hatustahili tu kumpigia kura mgombea pekee yake bali ni pamoja na chama. Mara kadhaa tumewachagua wagombea wazuri kupitia CCM lakini wakifika bungeni au wanapoteuliwa kuwa mawaziri wameshindwa kabisa kutimiza yale waliyowaahidi wananchi. Ukikaa nao mmoja mmoja watakuambia kuwa wanashindwa kuleta mabadiliko kutokana na mfumo mbaya wa CCM wa kuwadhibiti wale wanaoenda kinyume na matakwa ya chama.
Kama tunataka kuleta mabadiliko katika nchi yetu, ni lazima tuangalie ubora wa mgombea, na tutazame mgombea huyo anatoka chama gani.
Nimesoma kitabu cha January Makamba, ukitazama aliyoyasema kuhusu Tanzania mpya ni mazuri sana lakini hayatekelezeki akiwa ndani ya CCM. Yeye anataka kuleta fikra mpya, je, CCM yenyewe ina fikra mpya? Tatizo hilo alilipata sana Mkapa na Kikwete, na kuna wakati marais hawa walijaribu kutaka kuwa na nguvu katika chama kwa kuwapeleka mawaziri wao wagombee ujumbe wa halmashauri kuu ili kuleta fikra mpya kuanzia kwenye chama, wote walipigwa chini, hawakupita. Kwa sababu wale wahafidhina wamejenga umoja fulani, na umoja wenyewe ni wa uovu. Wao wanawachagua watu kwa kuangalia nani amewapa bahasha, na huyo mgombea atampa fadhila gani. wale watu wasafi kwa sababu hawawezi kuhonga au kuahidi au kutoa upendeleo kwa wajumbe wanaopiga kura, hawapiti ndani ya CCM. Wengi wa wanaopita katika kugombea uongozi ndani ya CCM ni wale watoa rushwa, na mtoa rushwa hawezi kukosa kupokea rushwa.
Nasisitiza, ni lazima tuangalie ubora wa wagombea na ubora wa chama maana kwa mfumo wetu wa Tanzania chama kina nafasi kubwa sana katika uongozaji na usimamiaji wa serikali.
Uwanja ni wako na una haki ya kubwabwaja na kuhororoja upendavyo.
Slaa alibwagwa na Kikwete na kwa maadili mabovu aliyonayo huyo atakuwa ni chaguo lako lakini nnauhakaika hatokuwa chaguo la Watanzania wengi wanaopenda maadili mema.
Mimi sitomchaguwa Slaa hata akibaki kuwa ni mgombea pekee.