Umewahi kumpigia kura mgombea wa chama kingine sababu uliona anafaa zaidi kuliko wa chama chako?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Umewahi kumpigia kura mgombea tofauti na wa chama chako kwa kuwa unaona ana sifa bora za kuwa kiongozi kuliko wa chamani kwako? Au unampigia yule tu aliyesimamishwa na chama chako hata kama unaona hafai kuwa kiongozi.

Kumekuwa na tabia ya watu kupiga kura kwa kufuata vyama, yaani kuwapigia kura wagombea waliosimamishwa na vyama vyao hata kama hawana sifa stahiki kuwaongoza, hupiga kura ili chama kishinde bila kuwaza baada ya uchaguzi kama umemchagua kiongozi asiyefaa basi utakaye pata madhara ya kuwa na kiongozi asiyefaa ni wewe na utabeba mzigo huo kwa muda wa miaka 5.

Inabidi jamii ijenge utamaduni wa kupiga kura kwa kuangalia sifa za kiongozi, sera anazonadi kama zinatekelezeka na ndio uhitaji wao na kama amewahi kuwa kioongozi alikuwa kiongozi wa aina gani alifanya vyema au lah ndipo wafanye maamuzi ya kumpigia kura au kumtupa pembeni.

Mihemko ya kichama kutaka chama unachokifuata kishinde hata kama hakina viongozi wanaofaa kuongoza kwa wakati huo husababisha jamii iwe na viongozi wengi mizigo, wasio na tija kwa Taifa na kusababisha jamii izidi kuwa duni na kusababisha hasara kubwa kwa taifa.

Je, huwa unapiga kura kwa kufuata chama au unampigia mtu mwenye sifa hata kama hatoki kwenye chama chako?
 
Back
Top Bottom