Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Kama unanisoma humu JF ungejuwa kuwa kama ningekuwa mhafidhina basi kwanza ningekuwa namsifia Nyerere na hata nisingeyaona makosa yake. Fikiri.

Tundu Lissu kwa kutokuwa mhafidhina na kwa kuweza kuyaona na kuyasema wazi makosa ya Nyerere namkubali, lakini ananikera pale anapoiga sauti za wachungaji wa Jangwani anapowasilisha hoja zake.

Ikiwa hata mtu akiiga sauti ya wachungaji wa jangwani unateseka basi hakika wewe FF una pepo mchafu. Fanya haraka ukaombewe hapo jangwani wachungaji wakiitisha mkutano.
 
Narudia, Tanzania hii hatuchaguwi vyama tunachaguwa kiongozi na tusibweteke tuoneshe mfano mwema kama tulivyouonesha mwaka 2005 tulipomchaguwa Kikwete bila kujali itikadi zetu za vyama.
hii ni itikadi na uenezi wa propaganda.UNATUMIA MFANO WA MWAKA 2005 kana kwamba 2010 hakukuwa na uchaguzi na mtu huyohuyo alishiriki,na matokea yanafamika.Usione soni na anguko lile,si la ghafla bin vu.
 
Hiyo kwa Waswahili wa pwani hujulikana pia kama bokoboko.Kuwa makini unapoandika, unabadilisha maana ya maneno hata sielewi nikujibu nini. Sasa harisi aka bokoboko lina uhusiano upi na hii mada?
weka halisi sehemu ya harisi. Jibu sasa
 
Tatizo ao viongozi awajamini kwenye izo kura za maoni kila mgombea ana makundi yke na hela za kununulia kura

Hapo ndipo inapobidi kama wanachama tuwe na nguvu zaidi ya wenye vyama.
 
lakini kumbuka mwaka 2010 ccm mliikataa ni sera ya chagua mtu mkasema ccm ndo inaleta amani hivyo chagueni ccm wapinzani wanaleta vita sasa mwaka huu mtaweza kweli?

Ikishafikia kwenye wagombea kuanza kugombea hapo ndipo unapofanya maamuzi yako kiuhakika, kama mgombea mliyeona mmemchaguwa na kumpendekeza kang'olewa na mkabambikiwa mgombea wa wenye vyama na kuiendeleza kumchaguwa tu kwa kuwa ni wa chama ukipendacho unakuwa hujajitendea haki na unakuwa hujawa ni mtu wa kuweza kujiongoza na utabaki wa kuburuzwa daima.
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

FaizaFoxy vazi linaloitwa CCM limeisha pakwa kinyesi, halitakasiki. Hebu tuambie ni kweli mtajinadi kwetu bila kutaja sera zenu na kupamba majukwaa na magari yenu bila zile bendera za njano na kijani. Hamna huo ubavu, kwani hicho chama kilijichafua chenyewe au kimechafuka kutokana na hao viongozi walio katika chama? Hao viongozi mnaosema mnao ni wepi? Nje ya ccm yes, wapo viongozi wengi sana na hapo nakupa heko.
Huo ushindi wa 2005 wa 80% kumbuka pia uligubikwa na michezo michafu. Mtihani mkubwa mnao ccm, mnawaenguaje ma-veteran wenu, patachimbika.
 
Kama unanisoma humu JF ungejuwa kuwa kama ningekuwa mhafidhina basi kwanza ningekuwa namsifia Nyerere na hata nisingeyaona makosa yake. Fikiri.

Tundu Lissu kwa kutokuwa mhafidhina na kwa kuweza kuyaona na kuyasema wazi makosa ya Nyerere namkubali, lakini ananikera pale anapoiga sauti za wachungaji wa Jangwani anapowasilisha hoja zake.
Kwa nini tusichague kiongozi kutoka Chama chenye sera nzuri? Tunaongozwa na mtu tu au na sera nzuri zinazosimamiwa na mtu mzuri?
 
  • Thanks
Reactions: 999
CCM kinabaki kuwa chama bora Tanzania mpaka hii leo, lakini kumbuka, Tanzania huwa hatuchaguwi vyama tunachaguwa viongozi na ukinisoma vizuri kwenye post namba moja nimeweka mifano hai.

Umechemsha, kwani huwa mnakuja kama wagombea binafsi. Mimi nawapa ushauri wa bure ccm, sambaratikeni kila mtu a-chukue chake mapema mjichomekechomeke kwenye vyama vingine yamkini mtaweza kuvivuruga. Isitoshe ndio mbinu mnayoitumia mara kwa mara.
 
Leo umeamka na nini? Nahisi kuna kitu kinatokota huko CCM. NO more no less
 
Mwaka huu 2015, wazo kuu ni Operation DELETE CCM KWANZA mambo mengine baadaye. Tunaondoa Ukoo wa panya kwanza halafu tutajipanga mbele kwa mbele... Hapa Habari ni UKAWA kwanza. So hata kaka UKAWA wakiweka jiwe mimi nitalipigia jiwe kuliko mhawa wezi wa CCM maana tatitzo ni Ukoo, mtoto wa Panya naye ni panya tu haijalishi ni mweupe, mweusi au mwekundu.
UKAWA SAFIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Mimi wangekuwa wanaruhusu,ningeweka tick kwa mgombea wa ukawa,cross kwa mgombea wa ccm ili akale vizuri hela ya escrow ambayo mlisema sio ya uma.
 
Tayari mshaanza kuweweseka, mwanzoni mlikuwa mnasema chagua ccm, leo mmeona ccm imeoza mbele ya macho ya watanzania mnabadili wimbo eti oo chagua mtu msichague chama.Hapo bado mtayasema mengi kwani mchuma majanga ula na wenzake.

CCM ni chama bora katika Tanzania ni chama chenye mizizi kila kona ya Tanzania.

Ukifika uchaguzi, CCM kinakuwa na sera na ni wajibu kumchaguwa tunaeona anafaaa kuzisimamia hizo sera. Si kila mgombea anaefaa.

Mfano, Slaa anaweza kukukinaisha vipi kuwa atasimamia maadili ya mtoto wa Kitanzania wakati yeye mwenyewe kashindwa kusimamia hata maadili ya kanoni aliyoisomea? Fikiri.
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Kwamba mifano ya haja ni namna alivyochaguliwa Mh Kikwete na Mh Shibuda.

Ninaendelea kuamini kuwa kitengo cha Propaganda cha CCM kimeishiwa ubunifu wa kisiasa kushawishi wapiga kura.

Enyi wana CCM, endeleeni kutapa tapa bila kujua nini mseme ili kuchokoza mijadala ya sifa za viongozi tunaowataka kwenye jamii yetu ya karne hii ya 21.

UKAWA utaendelea kuwa mwiba unaoichoma CCM ndani ya ngozi yake.

Haya maigizo ya chagueni viongozi, msichague vyama ni kiashiria kingine kinachodhihiri namna CCM inavyomfia JK mikononi.

Rest in Hell CCM>
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Kwa mara ya kwanza toka nimekufahamu wangalau leo umeongea kitu kinachoendana na umri wako na uzalendo wako. Siku zote umekuwa unaongoza kwa kuleta post zinazowagawa watz kwa faida ya chama chako. Nikuunge mkono kwa hilo huenda lile pepo baya lililokuwa limekukamata limekuachia. Ukijaribu kuangalia kwa muda mrefu sana vyama vimegeuka kuwa ndio vyenye maamuzi ya viongozi na sio wananchi. Na tatizo hili kwa kiasi kikubwa sana lilianzishwa na ccm haswa baba wa Taifa, japo wangalau yeye alikuwa na dhamira safi. Lakini mbegu hiyo iliyoanzishwa kwa dhamira safi ama udhaifu wa Nyerere leo hii imegeuka kuwa mwiba mchungu wa wananchi wa taifa hili. Na sio hilo tu baba huyohuyo wa taifa ndiye aliyekuwa chachu ya vyama vya upinzani kutokushika madaraka ya nchi hii. Mfano halisi ni matokeo ya uchaguzi kwa upande wa ZnZ haswa upande wa urais. Tatizo hilo limeendelea mpaka leo na wakati mwingine unaona mpaka umwagikaji wa damu mfano halisi tena ni mwaka 2001 mauaji ya ZnZ chini ya Mkapa ambaye atakuwa na la kujibu pindi ccm ikitoka madarakani labda aombe maridhiano ya kitaifa.

Hali hii ya watawala iliyoasisiwa na Nyerere kwa dhamira njema ama udhaifu wake kibinadamu, kuendelea kuchagulia wananchi viongozi imetumika sana na vyama hasa hasa ccm kwa dhamira mbaya kwa kuweka viongozi wala rushwa, wezi na marafiki wa watawala hasa hasa matajiri ambao sipendi kuwataja hapa, ambao wamekuwa wabunge na madiwani kwa pesa zao wakati hawajawahi hata kuchangia huko bungeni wala kwenye halmashauri zao. Nadhani kama dhamira yako inasimamia ukweli unawajua watu hao angalau kwa uchache. Ushauri huu unaoufanya wewe leo ni sahihi sana japo umechelewa kidogo, hebu niambie hao viongozi wanaochaguliwa na chama na sio wananchi ni wangapi wako tayari kwenda kwenye midahalo ya wazi kama hiyo itakayoandaliwa na ITV na Udassa? Jibu ni hakuna, na wengi watakaokacha ni wa ccm kwani huko ndio kulikobobea kwa vishoka wa siasa.

Wewe pia ni mmojawapo wa watu wanaoiunga mkono katiba hii pendekezwa na wala sio unaiunga mkono kwa kuwa ni bora, ila unaiunga mkono kwa kuwa imepitishwa na ccm na inatoa nafasi ya ccm kuendelea kubaki madarakani hasa kwa hila. Nasema hivyo kwa sababu ccm haikuwahi kutaka katiba mpya sio kwa ilani au kwa matamko yao, bali JK aliikubali mwaka 2010 baada ya wapinzani kusema wataanzisha mchakato wa katiba mpya huku yeye akiwa mshindi wa urais wenye utata. Thanks God dhamira yake ikamsuta akaamua kuanzisha mchakato. Wapinzani waliotaka katiba mpya walitaka kuwe na mgombea binafsi na hata tume ya Jaji Warioba iliweka kifungu hicho, kilochotokea ni chama chama kuleta mizengwe kwenye kifungu hicho cha mgombea binafsi ili wenye fikra huru waendelee kuwa watumwa wa vyama. Leo hii wewe unaanzisha mada kwa nia njema bila kujua hata wewe ni mdau kwa kushangilia katiba mbovu inayofanya vyama kuwa ndio wachagua viongozi na sio wananchi. Ama mama unataka vyama vishukiwe na malaika awakanye na wala sio katiba ndio itamke wazi na kwa uhuru mgombea binafsi?

Swali moja ambalo ukipenda jibu usipopenda unaweza kulipotezea, kwa udhaifu huu unaouna kwenye mgombea binafsi, kwenye kura ya maoni ya katiba mpya utapiga kura ya ndio ama hapana. Kumbuka ukisema ndio itakuwa imetoka na udhaifu huo lakini ukisema hapana tutapata mwanya wa kurekebisha udhaifu huo na kukuweka kifungu hiki cha mgombea binafsi sawa. Kuanzia hapo huu ushauri wako wa wananchi wachague mtu na sio chama itakuwa imepata ufumbuzi. Nangoja mtazamo wako. Nikupongeze kwa kuleta mada yenye tija leo. Asante
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.
Nafikiri labda haulewi maana ya Demokrasia, ngoja nikupe mwanga kidogo, unajua ni kwanini Nchi nyingi Duniani zina machafuko?
Ni kwa sababu hiyo uliyoipendekeza. Wananchi wa hizo Nchi wanachagua Watu na SIYO chama na mfano mzuri ni Kenya, Nchi hiyo ina shida kubwa ya vurugu kwa maana Wananchi wa hiyo nchi hawachagui Chama (sera) bali wanachagua Mtu/Watu!

Sisi nchini kwetu ni lazima tujione ya kuwa watu wenye Bahati sana angalau bado tunachagua Vyama kwa maana ya sera na SIYO Mtu!

Na hii inatusaidia sana pmj na matatizo yetu yote lkn hakuna mwenye hati miliki ya Watz kama unavyotaka kupendekeza, kwa mfano leo hii Wapinzani wengi wanampenda Bw.Slaa lkn wanampenda kwa maana yuko CHADEMA yaani wanapenda Sera za CHADEMA lkn Bw.Slaa akitoka CHADEMA basi ndiyo mwisho wake kwani hakuna atakayemfwata tumeona ya Zito Kabwe alipokuwa CHADEMA watu walimpenda sana lkn SIYO kwa sababu ya yeye kama ZIto Kabwe Hapana bali ni kwa sababu ya SERA za CHADEMA sasa akitoka (Zito) hakuna atayemfwata na huyo ndio mwisho wake na ndio maana amejaribu kutingisha kiberiti kuona kama CHADEMA ni yeye ama vipi lkn matokeo yake ameyaona ya kwamba CHADEMA SIYO Mtu bali ni Chama hata huko Kigoma anakotoka Wananchi wanapenda CHADEMA na SIYO Mtu(Zito), vile vile CCM watu wengi wanampenda Bw.Lowasa lkn ni kwa sababu yuko CCM na akitoka CCM ndiyo mwisho wake hakuna atayemfwata na watu watabaki CCM!

Mfano mzuri ni Mrema ndiyo watu walimpenda lkn pia Walipenda NCCR Mageuzi lkn alipotoka NCCR hakuna aliyemfwata!

Hivyo Tanzania sisi ni model ya Bara zima la Afrika kwani kwetu Siasa SIYO Mtu bali ni Chama na tunachagua Sera na hatuchagui Mtu, na hii ni bahati kubwa sana na Mungu azidi kutubariki kwa kuliona hili mapema! !
 
Back
Top Bottom