Epuka kujenga uadui na mwenzio kisa eti anaunga mkono chama tofauti na chako

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam Wadau,

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Kwa maana hii, Wananchi wamekuwa wafuasi wa Vyama mbalimbali.

Baadhi ya Vyama vina ushawishi Mkubwa na wafuasi wengi kuliko wengine.

Kumekuwa na tabia baadhi ya Wananchi (Wanachama) hasa wa Vyama vikubwa kujenga uadui kudhalilishana, kuondoana utu kwa sababu ya kuwa Vyama tofauti vya Siasa.

Tabia hii imesababisha kuleta ugumu hata kwa watu kuona mazuri ya chama kingine wakichukulia ni sawa na kumpa nguvu adui yao.

Hoja yangu hapa ni kwamba si vibaya watu kuwa na mitazamo tofauti, kupinganakwa hoja, kupingana itikadi za chama kingine lakini hii haimaanishi ujenge uadui.

Wananchi wengi wamejikuta wakichukiana na kujenga uhasama miongoni mwao wakati Viongozi wao wa Vyama vyao wakikutana wanaongea kirafiki na furaha.

Kuwa mfuasi wa chama tawala haimaanishi unapaswa kuunga Kila matendo na maamuzi ya Serikali, kuwa Chama Pinzani haimaanishi unapaswa kupinga kila kitu kinachofanya na Serikali. Kuwa mfuasi ya haki na njia sahihi. Hili linawezekana ikiwa kila mmoja wetu ataliweka matendoni.

Tambua, Siasa ni mchezo mchafu, usije ukajaa upepo kumpiga mfuasi wa chama kingine ukiamini unakipigania chama chako au kiongozi wa chama wakati yeye hapigani kwa ajili yako.

Tafakari, chukua hatua!
 
Bora niwe na rafiki ni TLP au CHAUMA kuliko CCM.

Kuna rafiki nilisoma naye ila alikuja kuwa CCM sasa Mimi mitazamo yangu na kukaa nje ya nchi na nchi yangu Kila jambo nililiona kasoro jamaa alinichukia mpaka Leo unaambiwa
 
Salaam Wadau,

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Kwa maana hii, Wananchi wamekuwa wafuasi wa Vyama mbalimbali...
Kuwa na uadui huo ndio ujue una hisia za utu na ubindamu.

Kwasababu watu wengi wanaonifanya hawavhukii mtu kwasababu za kisiasa wengi ni magwini wa UNAFIKI, Wanaoabudu pesa na wanaohalalisha kila uovu kwasababu ya siasa.

Yaani Jitu linaua watu au linadhulumu watu, weee ulichkekee chekee kwasababu eti linafanya siasa.

Au jitu linasema mambo kwa ndimi mbili mbili likiona ubwabwa au maslahi yake, ulichekee kwasababu eti linafanya siasa 🤔
 
Salaam Wadau,

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika mfumo wa Vyama vingi vya Siasa. Kwa maana hii, Wananchi wamekuwa wafuasi wa Vyama mbalimbali...
kuna jamaa huwa wanaporomosha mitusi hatari ukiwachallenge tu kidogo 🐒
 
Asante kwa ujumbe maridhawa kwa "kile chama" kinachowatumia mapolisi, usalama, TRA kuwamaliza walio tofauti nao kiitikadi!
 
Back
Top Bottom