Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.
Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.
Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.
Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.
Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.
Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.
Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.
Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.
Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.
FF sasa umeanza kujitambua, ya kwamba zama za kuchagua chama zimekwisha! Hapo ni sawa, ila kuna swala la kujiuliza ambalo kabla ya kuchagua, je huyo mgombea anatoka kwenye mfumo wa namna gani?! Mada yako inaonyesha kwamba kwenye chama fulan kuna shida, so tunatakiwa tumchague mtu personally and not the party!!!
Iko hivi, kwa Tanzania, kuna haja ya kuangalia yote mawili, i.e chama na mtu mwenyewe! Kwa mfano mgombea anaweza kuwa ni msafi na mwadilifu sana ila kutokana na chama alichopo, uadilifu wake hauonekani wala hawezi kusema lolote! Haya tumeyashuhudia hapa TZ, CCM kuna waadilifu ila wahalifu ni wengi kuliko waadilifu! Kama wahalifu ni wengi kuliko waadilifu unategemea nini?!
Kwenye scandal ya ESCROW, waadilifu ndani ya CCM tuliona walivyojipambanua, lakin kutokana na uchache wao haikusaidia lolote na wameonekana wasaliti! Maswala ya chama na mgombea hayana issue kama unavyowaza wewe! Mimi nashauri tutafute viongozi wazalendo, sio hao Mbwa mwitu walioko huko CCM.....! Hata kama anatoka chama cha kanisa/msikiti, kama sio mzalendo akafie mbali. Nashangaa kuna watu wamepandishwa mahakamani jana eti walipokea rushwa, mbona huyo mtoa rushwa hakupanda mahakamani!
FF nakushauri muwe mnamshauri JK manake anachofanya hata watoto wanamshangaa tena mno!!!! Tibaijuka kaadhibiwa kwa ukosefu wa maadili, wakati huo huo pesa alopokea ambayo ndo iliyomtoa kazin tunaambiwa sio ya umma, sasa ina maana ukipewa hela na mtu ukapokea ndo huna maadili...!? This is nonsense Faiza!!!!
Mwambie JK na genge lake hapo Ikulu, kiama chake hata kaburin kitamfuata.... They can't make us fool as such...!
Na wewe ipo siku hii ID yako itapotea humu. Huezi kutetea uovu namna hii ukategemea kuwa salam! One thing for sure, hata dola ya Rumi ilianguka. Tutafanya kila kitu kwa imani hoping that ipo siku tutaiangusha CCM. Na usidhan kwamba tunaichukia CCM, wengi wetu tunaipenda maana ni chama kilichotutoa mbali, tatizo letu ni hao Mbwa mwitu mliofuga. Kuanzia JK na cabinet yake nzima! Mbwa mwitu hawa wameamua hata kuua wale kondoo waliopo ndani ya zizi kama akina dr. Mvungi na wengine wengi tu wamepotea kisa Mbwa mwitu mnaowafuga hapo ikulu!!! Hivi kweli JK anampa mtu madaraka and then anashindwa kumwajibisha!? Huyu ni raisi goigoi kabisa tena hajui lolote.
Samahan kama utakwazika na lugha yangu..! It's that I'm fed up of you guys...!