Watanzania mlioko sasa nchini Uganda naomba Majibu ya haya Maswali yangu muhimu yafuatayo....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,032
1. Kwa Kodi ya Shilingi Milioni Moja za Uganda ( Tanzania Shilingi Laki Tano ) nitapata Nyumba ya Hadhi gani ya Kupanga?

2. Je, mfumo wa Ulipaji Kodi huko ni kama wa huku Tanzania wa Miezi Mitatu, Sita na Mwaka au unaweza ukalipia hata Kodi ya Mwezi Mwezi?

3. Gharama za Maisha kwa sasa nchini Uganda zikoje? Mfano nikiwa Sijipikii Kwangu huku nikiwa Mwenyewe tu nikitenga Shilingi Milioni Moja na Laki Tano za Uganda ( Tanzania Shilingi Laki Saba na Elfu Hamsini ) haitonitosha kwa Breakfast, Lunch and Supper?

4. Kwa Wastani kwa sasa nchini Uganda huko Gharama za Tozo za Maji ni Kiasi gani na Bili ya Umeme ( zote kwa Mwezi ) ni Shilingi ngapi?

5. Je, naweza kupata Nyumba ya Kupangisha kwa Kiasi hicho tajwa hapo juu cha UGX 1,000,000/ ( Tsh 500,000/ ) kwa maeneo ya karibu na Ofisi za Bunge au Ikulu ya Nakasero au maeneo ya Kololo, Ntinda na Muyenga?

6. Mishahara ya Mfanyakazi wa Ndani na wa Bustani kwa Mwezi huko nchini Uganda kwa Wastani huwa ni Kiasi gani?

7. Bei ya Vitanda, Magodoro, Music Systems, Flat Screens, Ving'amuzi, Vocha za Simu, Kukodi Ubber na Huduma za Intaneti kwa Wastani huwa ni Kiasi gani?

Kwa Watanzania mlioko Jijini Kampala nchini Uganda nitashukuru mno kama mtanijibu GENTAMYCINE kwa haya Maswali yangu Saba ( 7 ) tajwa hapa kwani kwa BARAKA ZAKE KUBWA MWENYEZI MUNGU ndani ya Siku 10 au 15 kuanzia leo nitakuwa nanyi huko kwa muda wa Miaka Miwili na kama DUA za Watanzania ZITANIBARIKI basi naweza Kuongezewa tena Miaka mingine Miwili.

Nimetoka huko nchini Uganda kwa mara ya mwisho mwaka 2002 hivyo kwa sasa narejea kama Mgeni japo Vijiwe vyangu vya Totooz bado navikumbuka na Lugha ya Luganda kwa baadhi ya Maneno kama NIKUAGALA NYO NYABO TUGENDE KUKOLANA ( NAKUPENDA SANA DADA TWENDE KUBANDUANA ) bado nayakumbuka hadi leo hii.

Simba SC nawaomba leo msiniangushe Kimatokeo ili nikisafiri kwenda Uganda niwe na Furaha ya SI tu Mwarabu Kufa ( Kufungwa ) bali Kutolewa kabisa Mashindanoni CAFCL.

Kila la Kheri Mamelodi Sundowns Kesho.
 
Nimetoka huko nchini Uganda kwa mara ya mwisho mwaka 2002 hivyo kwa sasa narejea kama Mgeni japo Vijiwe vyangu vya Totooz bado navikumbuka na Lugha ya Luganda kwa baadhi ya Maneno kama NIKUAGALA NYO NYABO TUGENDE KUKOLANA ( NAKUPENDA SANA DADA TWENDE KUBANDUANA ) bado nayakumbuka hadi leo hii.
Kama unaenda kama ADF jiandae kukiona cha mtema kuni.
 
Naenda peke yangu Mkuu ila kwa sasa itanilazimu nipate Shemeji yenu Official wa kutoka huko Uganda kwani Upweke sasa nimeuchoka.
huko utapata sana alafu kunapisi mix uganda na kinyarwanda .yani ni wazuri na wengine type kama za zari zipo nyingi sana.
maisha ya uganda ni mazuri hali ya hewa ni kama hupo moshi au karagwe .pili maisha ya kule yapo chini sana
 
Hiyo hesabu haiko sawa, laki 7 za tz = mil moja ya ug. Hiyo chenj ya nusu kwa nusu ilikuwa ya zamani kipindi nasoma, sasa hivi ni 7 kwa 10, means elfu 70 ya tz unapata laki moja ya ug. Kuna wakati inaenda hadi 75 kwa 100.
 
Hili jibu lako Nimelifurahia kweli kweli na natamani hata leo hii Flight Ticket yangu iwe tayari niondoke. Hapo uliposema Mademu wakali ndiyo Umenichanganya mno Mkuu.
 
Nimetoka huko nchini Uganda kwa mara ya mwisho mwaka 2002 hivyo kwa sasa narejea kama Mgeni japo Vijiwe vyangu vya Totooz bado navikumbuka na Lugha ya Luganda kwa baadhi ya Maneno kama NIKUAGALA NYO NYABO TUGENDE KUKOLANA ( NAKUPENDA SANA DADA TWENDE KUBANDUANA ) bado nayakumbuka hadi leo hii.
Janggu nikukwate kwate🤣🤣 hayo maneno uliyoyaandika yamenikumbusha mbali sana. Enzi za club silk na Ange noir.

Kampala ilinilea maisha yangu ya sekondari yote late 90's - early 2000's.
 
Hiyo hesabu haiko sawa, laki 7 za tz = mil moja ya ug. Hiyo chenj ya nusu kwa nusu ilikuwa ya zamani kipindi nasoma, sasa hivi ni 7 kwa 10, means elfu 70 ya tz unapata laki moja ya ug. Kuna wakati inaenda hadi 75 kwa 100.
Asante sana Mkuu kwa huu Ufafanuzi wako mkubwa na Elimu ya Masuala haya ya Kifedha.
 
Naenda peke yangu Mkuu ila kwa sasa itanilazimu nipate Shemeji yenu Official wa kutoka huko Uganda kwani Upweke sasa nimeuchoka.
Mission completed in Tz!!?Bandari taken si ndio!!Rwanda malori dominant Bandarini!!?Dar es salaam is part of Rwanda region economically!!?

Now unataka ukawe part ya inner cycle ya Muhooz kainerugaba atakaposhika hatam!!

We jamaa!!kinachokuondoa Tz ni nini!!?wakati ndio ulikua unajidai humu kila siku!!?

Wasalimie pale Mbarara Kuna remnant's za nyankole jombas zipo pale !!
 
Nitajie Bei ( Kodi ) ya maeneo yote Uliyoyataja hapa.
Go and get a room in one of the hostels or apartments meant for single or bachelor and university students neighbouring universities e.g MUBS, Mukono University, Kyambogo, Makerere, KIU, Kampala University, please stay in town (300K is enough, 500K it's like heaven utafurahi sana).
Kampala is the best
 
Back
Top Bottom